Habari za Ijumaa wapendwa,
Imetokea umepata mwenza anaekupa masharti kuwa mtoto wako asifike nyumbani kwenu utachukua uamuzi gani?
Yalimtokea shosti, alipata mimba akiwa form six, kichwani alike a njema na alipata na fast USDM baada ya kujifungua. Ilibidi aahirishe mwaka na wazazi waliachiwa kichanga nyumbani.
Akiwa chuo alikutana na kijana mmoja ambae alifunga nae ndoa. Ingawa kijana alifahamishwa hali halisi na alishamuona mtoto lakini hali ilikuwa tofauti pale wote walipopata ajira na mdada kutaka kumchukua mwanae amlee. Mume alipinga vibaya sana. Shosti alikuwa imara, alimwambia angalia hapa huyu mtoto bila mimi asingekuja duniani, wewe una wazazi waliokulea mpaka hapo ulipofika, kama hutaki kuishi na mwanangu na mimi ninaondoka.
Jamaa alijifiria sana, katika vikao vya kusuluhisha ndoa jamaa alijiona amechemka. Mwisho wa yote alimlea yule mtoto kwa mapenzi yote.
Binafsi naona si vema ,vinginevyo bora usimuoe mwanamke uliekuta tyr ana mtoto/watotoKuna wanaothamini ndoa na anamuacha mtoto kijijini huko yeye yuko mjini.
Mkuu una mtoto?Kuna wanaume pia wanaona soo kuoneka kuwa ameoa mwamke mwenye mtoto au aliyekuja na mtoto. Hao bado ni wavulana.
Hiyo sioni kama ni vizuri sasa itokee na huko mtoto maisha yako vizuri lakini hivyo hiyo haina utofauti na uuaji. Kitendo cha kuthamini ndoa kuliko mtoto uliyezaa kinashabihiana/kinaweza kupelekea hata uuaji. Kama umepata ujasiri wa kumwacha mtoto kwenu kwa sababu ya mume /ndoa ni rahisi kufikiria hata kuua ili upate uhuru wa ndoa.Kuna wanaothamini ndoa na anamuacha mtoto kijijini huko yeye yuko mjini.
Si wengi wenye maconfidence kama hayo. M wish wa siku unashindwa kumuendeleza mtoto uliyemleta duniani kisa ndoa.akikataa kuishi na mwanangu namtimua.. kwan shida nini.. na atakayefata akileta ujinga pia timuaaaa... wanawake wapo wengi kuliko wanaume sibabaishwi..!!!!