Simbachewene amerogwa na nani?

nimemsikia leo akikanusha....kasema ni taarifa za uzushi na kaapa "walahi sikusema mimi".
Nimecheka hapa mpaka watu wameiangalia kwenye dalala apa. Kwa sasa kila mtu analipuka tu chochote akidhan ndo ataonekana anapiga kazi.

Hovyo kabisa ndo maana MCC 2 Imeota mbawa
 
Kuna habari nilitumiwa tu online ikisema Waziri Simbachewene amesema
kuanzia sasa serikali haita ajiri 'watu wenye vyeti vya kuunga unga' akimaanisha watu waliosoma mfano certificate...na baadae kujiongeza hadi degree au wale ambao walisoma kidogo kidogo huku wameajiriwa hadi kufika chuo kikuu..

Simbachewene huyu huyu amenukuliwa akisema wapinzani hawaruhusiwi kutekeleza sera za vyama vyao iwapo wameshinda halmashauri.

Kinachoshangaza Simbachewene mwenyewe historia yake inafahamika
alisoma kwa kuunga unga na inajulikana alikuwa 'mpiga debe'
stendi ya mabasi Dodoma kabla ya kuunga kuunga hadi kufika chuo kikuu

Ukichanganya na hili la wapinzani wasirihusiwe kutumia ilani zao wakishinda uchaguzi nimebaki najiuliza tu ameshikwa na nini?

Nini kinamfanya aongee vitu kama hivi? kuna nini hasa? mbona alipokuwa kimyaa tulimuona kama kiongozi anaeonekana ana busara.Kuna nini kinamsukuma kuongea haya?

Hivi hata Magufuli hatuwezi kusema kasoma kwa kuunga unga? Au nini tafsiri ya kusoma kwa kuunga unga?




Huyu amelogwa huyu kwasababu hakuna kiongozi ambaye ahajasoma kwa kuunga unga...Wengi wamesoma Masters na PHD kwa kuunga unga kama walikuwa na uwezo wa kifedha..............Wale waliotokea ktk maisha yasiyokuwa na fedha ndio kuunga unga hasa wamesoma...Magufuli mwenyewe kapata UDOCTOR kwa kuunga unga.
 
Wakuu wiki mbili hizi kumekuwa na Uvumi mkubwa kuhusu vigezo ambavyo Serikali yetu itaanza kuvitumia ili kuajili Watumishi mbalimbali wa Serikalini kwa mfano Juzi limetolewa Tangazo lilinasibishwa na Mheshimiwa Waziri Simbachawene kuwa wasomi wenye vyeti viwili yaani vya form 4 au form 6 hawatoajiriwa na Serikali bali Serikali itaajiri wasomi wenye cheti kimoja .

Vilevile limetolewa Tangazo lilinasibishwa na Dk Ndalichako kuhusu Serikali ya kuwa itaajiri wasomi kulingana na GPA zao 2.8 kwa Science & 3.0 kwa Arts

Kwa wanaofahamu habari hizi kwa Usahihi na Authentic Sources tunaomba Mtujuze kwa Undani.

Nawasilisha Wakuu !!!!
 
Watanzania wengi tumeshazoea kuzusha mambo,sijui huwa hizi habari za uzushi huwa tunazitoa wapi? Na sidhani kama kuna ukweli wowote hapo.
 
kwenye huu uvumi sasa hapo kwenye vyeti viwili sijaelewa ukiishia cha nne au cha sita sahau ajira serikalini au ebu tia nyama kwenye umbea huu
 
Ni uvumi mi Mara nyingi nimekuwa nikifatilia taarifa kutoka kwenye website za wizara zilizoko chini ya hao wahusika na hakuna ukweli ila ni hisia za vijiweni
 
kwenye huu uvumi sasa hapo kwenye vyeti viwili sijaelewa ukiishia cha nne au cha sita sahau ajira serikalini au ebu tia nyama kwenye umbea huu
Yaan kuna watu wame re-seat mtihani kwaiyo wabavyeti 2 vya form 4 wengine mpaka 3 na wengine wamerudia form 6 na wanavyeti 2 kwaiyo kwamujibu wa habari ile inasema eti hawa ni wasomi wa ku ungaunga
 
Kuna sehemu ni kweli ufaulu wa single seating unatakiwa. Kwa mfano kuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu kama UD. Credit za form IV au VI za kurudia mitihani hazikubaliwi
 
ila hawakukatai kwa maneno but utashangaa tu wenzio wanachaguliwa wewe upo tu unasibir awamu hizi na hizi hadi basi
 
Mmmh! Basi kama ni hivyoo wafute habari za kureseat siyo wanaongelea huko chumbani alafu nje watu wanahangaika kujenga vituo na kutafuta credits .em wawaache eboh! Hawajui kuwa mtu anaporudia mitihani kwanza anakuwa makini alaf ufanisi unaongezeka hapotezi bahati khaaa!..wajikute tuh!
 
elimu haina mwisho, ina michakato mingi,kikao kimoja kinatosha mtu kuendelea kujifunza maarifa mapya.
 
Back
Top Bottom