Wafujo
JF-Expert Member
- Feb 10, 2021
- 451
- 1,005
Ndio!! Wala hujakosea kusoma kichwa cha habari hapo juu. Simba SC ipo katika hatua za mwisho kuingia mkataba na winga hatari AUGUSTINE OKRAH (Miaka 28) wa klabu ya Bechem Utd (Iliyoshika nafasi ya 3 msimu huu) na Timu ya Taifa ya Ghana. Mchezaji huyo hivi sasa yupo nchini na wakati wowote atatambulishwa kama mchezaji mpya wa Simba SC kwa msimu wa 2022/2023.
Mbali na kuimudu vyema nafasi ya Winga ya kulia (RW) pia ana uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mshambuliaji (CAM) au namba 10. Augustine Okrah anatumia miguu yote miwili japo anatumia hasa mguu wa kushoto. Msimu uloisha amehusika katika magoli 21 katika michezo 31 ya timu yake ya Bechem Utd na ndie mfungaji wa mda wote wa klabu hiyo akiwa na magoli 30.
Augustine Okrah ameitwa katika timu ya taifa ya Ghana katika mechi za kufuzu michuano ya AFCON na huwenda panapo majaliwa mwezi Novemba akajumuishwa tena katika kikosi cha michuano ya Kombe la Dunia, hali itayopelekea Simba SC kuweka rekodi ya mchezaji wake kushiriki michuano hiyo mwaka huu. Okrah anasajiliwa kuja kuchukua nafasi ya Bernard Morisson alieachwa na Simba SC.
Okrah ameshavichezea vilabu kama Hecken ya Sweden, Asante Kotoko na Bechem Utd za Ghana, Al Mereikh na Al Hilal za Sudan.
NB: KWA UWEZO MKUBWA ALIONAO OKRAH WA KASI, KUDRIBBLE, KUFUNGA, KUASSIST NA KUMILIKI MPIRA, WAPINZANI KAZI WANAYO MSIMU UJAO.