Siku yangu ya Kwanza kupanda Lifti za kwenye maghorofa chamoto nilikipata

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,056
62,683
Habari Wakuu!

Nimejikuta ninacheka tuu. Unajua haya mambo ya kizungu yanatutoa wengi nishai, wenge, Knockout. Yalinikuta, niliyakanyaga.

Picha linaanza uncle kanipigia simu niende ofisini kwake, katika moja ya balozi za nchi ndogo za mashariki ya Ulaya, sikuwahi kufika ofisi yake tangu hapo Kabla, huyo nikapanda Gari ruuuuu! Paap! Mpaka kituo ambacho Konda alinihakikishia ndio hapo Kwa mujibu wa maelezo niliyompa.

Nimenyuka mkanda nje, tai inaning'inia kama kishada, chini nilivaa viatu vyeusi bila soksi, suruali ikiwa inaning'iania kwenye kifundo cha miguu (Ankles). Baada ya kushuka nikajiweka Sawa nikiwa tayari nimeliona jengo nililokuwa nimeelekezwa na Uncle. Lilikuwa jengo kubwa la ghorofa zisizopungua 12 hivi.

Mwendo niliokuwa natembea nao kuingia katika jengo lile wapita njia bila Shaka walifikiri Mimi ni moja ya wafanyakazi, na wala sikujali wala nini. Majivuno ya Ujana, Ujeuri na Kiburi cha kupendeza, na sasa fahari ya kuwa eneo lile vilikuwa bega Kwa bega na Mimi. Niliifurahia Hali Ile nikiwapita walinzi waliovalia sare zenye nembo ya Kampuni Fulani maarufu hapa Jijini, sikuwasalimia wala nini,

Twa!twa! twa! twa! Hivyo yaani siogopi MTU Mimi. Wale walinzi niliwaona wakichagizwa na muonekano na utembeaji wangu. Yupo kiherehere mmoja alitaka kujaribu kuniita lakini nilivyoichomoa simu kwenye mfuko wa suruali nilimkatisha tamaa aliposikia nikisema "tayari nimetoka mjomba, ndio napanda" hapo kihede mswede na ngebe zake zikamuisha. Nami Kwa kiburi cha uzima nikamtazama kama kikaragosi kinachoweweseka Kwa upepo.

Huyo moja Kwa moja kwenye lifti. Hapo ndio kizaazaa bin kizaizai kikanipata. Sikuwahi kupanda Lifti Kwa kweli. Na Ile ndio ilikuwa siku ya kuandika historia Kwa mara ya kwanza kupanda Lifti. Nikawa naangalia vile vitufe ambavyo Kwa kweli sikujua nibonyeze kipi.

Punde Kwa sekunde, Nyuma yangu akaja mdada mrembo, Kabla hajajua kilichonisimamisha nikaamua kubonyeza moja ya vitufe vilivyokuwa pale ukutani, kimoja kilionyesha mshale kwenda Chini huku kingine kikionyesha mshale kwenda juu. Mimi nilibonyeza kitufe chenye mshale uelekeao juu. Ghafla lango likatawanyika nikazama ndani huku USO ukiwaumesawajika Kutokana na kadhia Ile. Yule Dada naye akazama ndani, lango likajifunga.

Tukawa Wawili mule ndani, Mimi na Yule Manzi. Mimi nilijua ukishaingia mule ndani basi, sikujua kuna mambo ya kubonyeza kwamba unaelekea ghorofa ya ngapi. Hata zile namba zilizokuwa kwenye kile chumba cha lifti Akili yangu ziliambia ni Fax numbers, motherfanta kudadadeki, sasa Yule Dada akanichanganya akaniambia kuwa yeye sio mzoefu wa mambo Yale lakini anaonaga Watu wakibonyeza bonyeza kwenye zile vitufe vyenye namba ambazo Mimi nilijua huenda ndio Fax numbers. Unajua Taikon tangu azaliwe anasikiaga Fax numbers lakini sikuwahi kujua zikoje na zinatumika wapi.

Sasa maneno ya Yule Dada yakazidi kunichosha, nikabonyeza Herufi G, hapo Lifti ikanguruma alafu mlango ukafunguka, nikajua labda ndio nimefika. Tukatoka na Yule Dada lakini ghafla nikawaona walewale walinzi, nikajua hakuna kitu nimefanya. Nikamwambia Yule Dada turudi, tukarudi. Sasa aibu ya ushamba Mbele ya Yule mrembo ilikuwa dhahiri na ukizingatia Taikon sikubaligi kushindwa na Nina Sifa Wakati zingine zakijinga, basi ilimradi.

Tukarudi ndani tena, Yule mdada licha ya urembo wake lakini muda ule Mimi ndiye nilikuwa Mwokozi wake. Mlango ulipojifunga siku yangu ikaita, alikuwa mjomba akiniuliza mbona sitokei. Nikamwambia soon ataniona.
Nikapata wazo nibonyeze namba ya ghorofa aliyoniambia, nikabonyeza, punde like dude likawa kama linanipa kizungumkuti, yaani kama nimelewa fulani au kueleaelea hewani. Hapo nikapata utulivu.

Muda huo nikakumbuka habari za Yule Dada, nikawa namtazama kupitia Kioo kilichomo mule kwenye Lifti. Alikuwa bonge la pisikali, kumbe alikuwa na Bahasha huenda aliitwa Usahili. Roho ya uchu wa kutaka namba za simu ikanijia, sikutaka kumuacha anipite hivihivi, hata kama nimeaibika Mbele yake. Nikaomba namba, naye hakuwa na hiyana akanipa. Lifti ikasimama na lango likafunguka kama mbengo za Aposto Mackenzie.

Tukatoka lakini eneo lile lilikuwa limefanana vilevile na kule Chini tulipotoka, sasa hapa niende wapi, Yule Dada naye akawa anababaika, nikataka kurudi tena kwenye lifti nirudi mpaka Chini kisha nipande Kwa Kutumia ngazi za kawaida, Kabla sijafanya hivyo ghafla kwenye korido ya floor Ile akatokea mjomba, aliponiona na Yule mrembo nafikiri alihitimisha kuwa ndicho kilichonichelewesha, akanichukua huku nikimuacha Yule Dada mrembo pale.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Kuuliza muhimu hahahaha.

Mimi nilizichezea sana kwenye maghorofa ya umma, kiufupi hazijawahi kunipa tabu.

Mkuu yani hata kwenye movie tu hukuwahi kuona zikitumika??
 
Kuuliza muhimu hahahaha.

Mimi nilizichezea sana kwenye maghorofa ya umma, kiufupi hazijawahi kunipa tabu.

Mkuu yani hata kwenye movie tu hukuwahi kuona zikitumika??

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ukiona kwenye movies au YouTube unaona rahisi, fanya wewe mwenyewe Kwa mara ya Kwanza ni msala.

Umenikumbusha siku nimeamua kupika chapati Kwa Kutumia YouTube, mbona zile za Yesu zilikuwa na afadhali.
 
Mara ya kwanza lift kwangu ilikua 2010 pale Mkapa tower. Haikua na mushkeli kwa sababu nilikua na wazoefu tayari na ndio nikajua kuitumia hapohapo.
 
C
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Ukiona kwenye movies au YouTube unaona rahisi, fanya wewe mwenyewe Kwa mara ya Kwanza ni msala.

Umenikumbusha siku nimeamua kupika chapati Kwa Kutumia YouTube, mbona zile za Yesu zilikuwa na afadhali.
Chapati watu wengi zina washinda πŸ˜‚πŸ˜‚,unatengeneza vzr lain ila zikipigwa na upepo zikapoa tu zinageuka ukoko ukivunja zila lia pchaaaa πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†πŸ˜†
 
Mimi ujuzi wa movie ulisaidia ila korido ndizo zilikuwa zinafanana nikajikuta napanda lift, nikishuka narudi na ngazi chini zaidi πŸ˜„πŸ˜„
 
Back
Top Bottom