Sikio langu halisikii tena ile Amplifaya (ya Clouds Fm) niliyoivika nishani

1.Power breakfast namkubali Kipanya na PJ.
2.XXL namkubali Adam Mchomvu na Mamybaby.
3.Jahazi nawakubali wote mia kwa mia, yaani GBantu, Gardner na Kibonde.
4. Amplifaya ni Millard pekee, huyo demu anaboa kishenzi.
5. SportsExtra bila Shafii hata siwasikilizagi.
6.Ala za Roho kuna yule dem alishika nafasi ya Diva kipindi yupo rikizo, nadhani kitu kama tirarira yuko vizuri sana haigizi sauti yuko real.
N.B, Kipindi wanachotakiwa kukifanyia maboresho ni Leo Tena. Wapunguze umbea na majungu kidogo alafu wampe muda wa kutosha kicheko na chitoto wachalaze mchiriku, mnanda na singeli la kufa mtu huku wakitupia vi stori vyao vya umbea wa uswazi kidogo naamini watakua wamekitendea haki badala ya kupiga bongo fleva na nyimbo za mtoni.
 
Wabongo kwa unafiki ndo maana mnabebewa mchanga wa madini kibao mmekalia unafiki tu.Clouds nyie piga kazi achana na wanafiki hao kama vip anzisha studio zenu
 
Back
Top Bottom