Wakati mabadiliko ya vipindi yanatokea kwa kuviua vipindi vingine na kuanzishwa vipindi vipya mjengoni Clouds fm inakosikika kidogo niandamane hasa kipindi Amplifaya kilipoipoka nafasi kipindi nilichokizoea (Afrika bambataa)...
Ujio wa Millard Ayo na kipindi chake cha "habari,muziki na matangazo" maarufu kama Amplifaya kilinisononesha mno....
Kwa kujijua kwamba sina hisa wala sijachangia kigoda cha kukalia studioni ikabidi nikae kimyaa....
Baada ya kipindi kuanza kusikika hewani nikawa nakisikiliza kwa kudonoadonoa,yaani nikizungusha "tunner" nikiusikia muziki ninaoupenda basi nashindilia kijiti kwenye tunner ili isijizungushe kupoteza hiyo chaneli (wakati huo sikuwa na radio yenye hivi vibonyezeo)....Hali ilienda hivi hadi siku moja moja najisahau kuindoa mpaka nikajikuta nasikiliza hadi hizo taarifa nilizojiapiza kutozisikiliza....Ajabu ni kwamba mpangilio wa habari uliopangiliwa kwa kupewa namba kumi hadi namba moja uliobatizwa jina la "Count down" uliniteka kiasi kwamba nikajikuta nasikiliza hadi matangazo ya biashara huku nikijilaumu kwa kujikatili kwa kukosa mtiririko murua wa kipindi kwa miezi kadhaa....nikamlaani shetani kwa pepo baya alilonivika na Mungu aliyeyaumba maskio akanisamehe,mambo yakaenda!
Millard Ayo akiwa peke yake studioni aliweza kuzigeuza habari za kawaida zikawa za kusisimua...
Millard Ayo akiwa peke yake aliweka mbwembwe kwenye matangazo ya biashara hadi unahisi ni wewe pekee kati ya watanzania wote ndo hujapata huduma ya hicho alichokitangaza...na hii ilisababisha asubuhi wateja kujazana kwenye ofisi za kampuni ambazo jamaa kazipa "promo" kuulizia bidhaa husika...KILA KAMPUNI IKAWA ANATAKA MATANGAZO YAKE YAWE YANASIKIKA KWENYE AMPLIFAYA...
Miaka ikasonga, kipindi kikiwa katika hadhi yake ileile huku maboresho kadhaa yakifanywa ili kuvuta wasikilizaji wapya...
Sijui lilikotokea "hili pepo" maskini...kipindi kikaanza kualika watangazaji wasindikizaji...ninaowakumbuka ni yule anayemuiga JK na huyu Meena Ally...
Ee Mungu uliyenibandika haya maskio,naona shetani yuleyule kaanza tena kuninong'oneza "HUONI KELELE?"...Sauti hii ya kunong'ona inanijia kila saa moja usiku inapowadia na inadumu masikioni hadi saa tatu usiku ndo inapotea....Baba,nataka nimshinde shetani huyu ila kwa kasi hii ya bombadia aliyokuja nayo,muda sio mrefu shetani atapaa na mimi wallahi tena!
Meena Ally punguza kelele kwenye kipindi...kipindi kwa sasa kipo kama kipindi cha "NIAMBIE"
shetani anarukaruka huku maana najua ananiona ninavyokunja sura ukiwasha tu Mic...
Meena Ally unamiliki kipindi utadhani wewe ndiye muongeaji mkuu....Unaongeaaa weee utadhani umekamuliwa juisi ya ndimu...na kwa kuwa unaongea bila break umejikuta unachapia kila dakika...
Habari kwa sasa hazina ule msisimko niliouzoea maana Millard akianza kuongea tu,Meena huyo....hivyo Millard anabaki kuitikia tu "Mmmm....mmmm....
Ukija kushtuka saa 3 kasoro 7 Millard kaongea maneno 22 na nusu pekee....SHUBAAMIT!
Na hii tabia ya kujiwehusha ndo kabisaa shetani wangu kaishikilia bango...huwa ananing'oneza "anayesikiliza wehu naye ni mwehu au atakuwa mwehu punde"....
Ee Mungu sitaki shetani ashinde kwenye hili,ila hapa kwenye kuitwa mwehu,wacha tu shetani apae na mimi niwe mbali na Amplifaya hii ya kolabo...
Siku hizi nanyemelea tu zile namba za vocha zinazotolewa...zoezi hili likiisha tu mimi Nduki! Na kwa kuwa Meena Ally ndo anazisoma imesababisha nisipatie hizo namba hata mara moja...Daadek!
Meena Ally nenda tu kwenye komedi mshkaji...hicho kipindi waaala....
Nduki!