Mkuu Amsha Akili, Tangazo La TCU la Wiki Hii Linasema Waombaji Wote Wa "UNDERGRADUATE" ni Lazima Waombe Kupitia TCU tu....!!
Na Ndio Mana NACTE wakasitisha Kutoa Matokeo Ya Udahili Kwasababu Hiyo Ya Kuchimbwa Mkwara na TCU kuwa Hakuna Taasisi yoyote Yenye Mamlaka Ya Kufanya Udahili wa First Digrii isipokua TCU.
Kwahiyo Kigenzo Cha Wale "DIPLOMA HOLDERS" ni Lazima Wawe na GPA ya Kuanzi 3.5 na Kuendelea.
Na TCU wamesema Wazi Kuwa Kigenzo Chochote Ambacha Sicho Kilichotolewa na TCU, basi Hakitatambulika.
Sasa hiyo GPA ya 2.8 ya NACTE ni Batili Kwa TCU na wala Haitambuliki usijisumbue.!!
Kwani Wenye Mamlaka ya Kudahili na Kutoa Sifa Za Udahili Kwa Wanavyuo Ni TCU pekee na Wala Si NACTE.
Mkuu Pitia Tangazo lao Kwa Umakini ili ufaidike Zaidi.