Katika ulimwengu wa leo, kuna kitu ambacho nimeshindwa kabisa kuelewa kinafanywaje, japo kukiri huku kunaweza sababisha wanaume wengi wasinielewe. Mie sijui kabisa kutongoza mwanamke tuliyekutana punde tu au hata yule tunaefahamiana kwa muda kwa ajili tu ya kufanya nae ngono na kila mtu aishie zake baada ya hapo - au labda ije itokee tena siku nyingine. Inaweza kunitokea kutokana na mazingira fulani tukiwa pamoja, lakini haitakuwa kwa namna ya kumbembeleza na kumwaga sera ili akubali tufanye ngono!
Sasa kwenu wanawake, hebu niambieni, hivi katika dunia ya leo bado kuna mwanaume kumtongoza mwanamke kwa ajili tu ya kufanya ngono na mwanamke akakubali?
Naelewa kwamba mahusiano ya kimapenzi yanaanza taratibu, urafiki wa kawaida ambao utakua hadi inafikia mwanaume (au hata mwanamke) kuweka wazi hisia zake na uhusiano wa mapenzi kuanza. Yaani ngono inakuwa matokeo ya uhusiano uliokuwapo au hisia zilizokuwapo tayari, sio agenda ya kuanzia uhusiano. Lakini hivi bado kweli mwanaume leo hii anaweza akakufuata na kuanza kukutongoza kwa ajili ya siku hiyo au kesho yake au hata wiki ijayo mkutane ili tu mfanye ngono tu, na wewe ukakubali? Hivi huwa hao wanaume wanawaambia nini hadi mnakubali?
Kumbuka hapa siongelei wale wanaume wanaokuambia ukiwakubalia watakupa gari, au kazi nk. Hao sio watongozaji, ni wanunuzi wa ngono, na kama unawakubalia wewe ni changudoa tu, utake usitake.