Siasa iwekwe pembeni katika maisha ya wananchi

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
958
Habarini wanajukwaa. Sasa hivi wimbo wa Taifa unakaribia kubadilika na kuwa baa la njaa. Wengi wetu wanachukulia kisiasa zaidi na wengine kinadharia zaidi. Tunaposema kuna njaa lazima tuangalie visababishi ambavyo mara nyingi huwa ni ukame, mafuriko au ugonjwa wa mazao n. k

Sasa kiuhalisia tukiweka siasa pembeni bado serikali ilitoa onyo na njia mbadala kwa hali ya chakula itakavyokuwa mwaka huu. Wizara ya hali ya hewa walitoa taarifa ya mvua kunyesha chini ya kiwango na kutokana na hilo wakulima walitakiwa kutafuta mazao ambayo yangeendana na mvua husika. Hata hivyo katika hali halisi ya mda huu huwezi kusema tanzania kuna njaa au kuna uhaba wa chakula. Kati ya mikoa zaidi 26 bado hatujapokea taarifa kamili inayosema mikoa 5 haina chakula. Kama hali hii ikiendelea hadi mwezi wa 6 ndiyo tutaweza kuanza kusema kuna uhaba wa chakula na hatimaye kuna njaa. Kila mwananchi aliambiwa weka akiba ya chakula lakini kama ilivyokawaida ya wananchi wanapuuza na kudharau. Mfano leo hii tunasikia kishapu kuna njaa ila mwaka jana wameuza mpunga, choroko, mtama bila kuweka akiba, je ni uzembe wa serikali?

Chakula kupanda bei ni hali ya kawaida katika baadhi ya miezi.
Hata hivyo katika hili iwapo baaa la njaa litatokea bado kutakuwa na wa kulaumiwa ambao ni
1. Afisa kilimo wa wilaya na mkoa (serikali)
2. Mkulima.

Maafisa kilimo walipaswa kutoa elimu kwa vitendo wakisaidiana na watendaji wao kuwaelimisha wananchi ni mazao gani wanapaswa kulima. Leo hii ikipitishwa sensa tutakuta zaidi ya asilimia 50 ya maafisa kilimo hawajulikani na wakulima.

Wakulima kutoenda na wakati na kufanya kilimo cha mazoea. Ardhi ya kanda ya ziwa inakubali mazao mengi mf. Mahindi, mpunga, mihogo, mtama, viazi, choroko, ufuta n.k. katika hayi mazao yapo ambayo yanahimili ukame na wameshindwa kuyalima kisa wanasubiri mvua ili waweze kulima kile wanachokitaka.

Pamoja na hayo yote tuombe Mungu katika maeneo ambayo mvua zinanyesha mazao yaive vizuri na wale walio na akiba kutumia vizuri.

Viongozi wa serikali pamoja na vyama vya siasa tujaribu kuweka siasa, wivuw, visasi katika maisha ya wananchi wanyonge na wasio na elimu ya kujiendesha
 
Hapo hutaweza kuona afisa kilimobakiadhibiwa sababu wao wako kama vitambulisho tu. Mtu aliye wateua kaamua kufanya kazi zao pia watakwambia hakuna nyenzo za wao kufanya kazi maana serikali inabana matumizi
 
Ulitaka kujenga hoja vizuri lakini umejivuruga. Kwanza kabisa hawa watu wanaoitwa "wakulima" kimsingi si wakulima katika maana halisi ya neno lenyewe. Kwenye Kiingereza kuna maneno makubwa mawili yanayozungumzia mtu anayetumia ardhi kufanya kilimo; kuna "farmer" na kuna "peasant". Kiswahili kinasomba tu jumla jumla. Hawa mnaowaita wakulima hapa nchini ni peasants, yaani masikini au mafukara ambao mali pekee wanayomiliki ni kipande cha ardhi anayoilima kwa jembe la mkono pasipo na ujuzi wala utaalamu wowote na kutegemea tu mvua.
Farmer ni mtu tofauti kabisa. Huyu yeye kwa kawaida ana ardhi kubwa sana, mtaji mkubwa au anakopesheka benki, ana akili ya biashara kubwa, ana vifaa, mashine, na pembejeo za kisasa, ana masoko makubwa ya mazao yake na anatumia mbinu za kisasa za kilimo ikiwemo umwagiliaji usiotegemea tu mvua.
Hawa wa aina hii ndiyo hapa Afrika utawakuta Afrika Kusini, Zimbabwe, ingawa Mugabe aliwavuruga, Kenya na nchi zingine chache. Hawa pia ndiyo utawakuta nchi zilizoendelea ulimwenguni. Tanzania hatukuwahi kufanya kilimo kuwa biashara, yaani we never embarked on commercial agriculture kutokana na sera mufilisi na za kimasikini zilizotukuzwa na Nyerere. Matokeo yake serikali zote hapa nchini zilirithi akili hizi za kijinga na sasa zikikosekana mvua tu tayari njaa inabisha hodi.
Kwa hiyo hizi tetesi za njaa si za uongo, ni kwa vile tu hali haijaathiri kila kona ya nchi ndiyo maana nadhani wengi kama wewe mnabisha kwamba kuna njaa sababu kwenu nyinyi ni mpaka ukame uzagae nchi nzima ndiyo akili zenu zisituke.
The point is kuna maeneo nchini mavuno ni sifuri na ukizingatia maelezo yangu hapo juu kuwa hawa mafukara wanaoitwa wakulima hawana maarifa yoyote ya kilimo basi njaa ni kweli ipo.
Hii ya kusema sijui wakulima wapewe elimu ni kupoteza muda tu; zitungwe sera zitakazowapa "farmers" halisi fursa ya kuendesha mashamba makubwa na kilimo cha kisasa maana tuna mamilioni ya ekari za ardhi yamekaa tu bila kutumika halafu kilimo cha biashara hakipo. Hatuna kabisa serikali zenye fikra nchi hii.
 
Nimekupa like kwa kuwa umekiri. Katika hili swala hadi mda huu ni ukweli usiopingika kwani serikali inalichukulia kuwa ni jambobla kisiasa huku baadhi ya wanasiasa wakichukulia kama mtaji wao. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa ila ni jukumu la kila mmoja kuwa mkweli na muwazi kuwa baa la njaa linakaribia nchini. Wengine watahoji mbona mavuno ya mwaka jana ndiyo yanayotumika leo bila kujua hata mazao ya mwaka huo huo huingia sokoni na ndiyo maana ukienda sokoni unaambiwa mahindi/mchele mpya huu.hii hupunguza upungufu wa chakula. Kuwaambia watu wakalime mfa huu ni uongo kwani mazao yanaanzia miezi 3 ili yaanze kuvunwa je kwa mda huo huyo mlalahoi ataishije? Na je atatumia nini kufanya apate mazao ikiwa mito mingi inategemea mvua na hakuna mvua yenyewe?
 
Back
Top Bottom