Shule za Dar kushika mkia matokeo ya kidato cha Nne, Makonda jitafakari na ikiwezekana jiuzulu

Hata ukichukua wanafunzi wote ambao wana akili sana ukawapa paper lazima apatikane wa kwanza mpaka wa mwisho hiyo ndio utaratibu wa evaluation

Vinginevyo hakuna maana ya mtihani tena
Examination is for evaluation and ranking haiwezekani wote muongoze lazima wa mwisho apatikane tu
Sikubaliani na hoja,
Examination is the act of giving students or candidates a test (as by questions) to determine what they know or have learned. Si kutafuta wa kwanza na wa mwisho.
Possibilities ya kuwa wote wakafaulu japo ufaulu wao uwe wa kiwango kidogo lakini wamefaulu upo.
Hapa question ni kwanini wamefeli, na kwanini shule za Dar ziongoze, tuangalie factors zilizotufikisha hapa
 
Usisahau pia mkoa wa dar es salama umetoa shule zaidi ya moja zilizoingia kumi bora kitaifa
 
Hiyo Shule ya Mbopo ipo porini huko Msitu wa Mabwepande.
watoto wanatembea na manati kilomita kadhaa.
Kuna kipindi mvua zilinyesha wanafunzi wakakwama kwenda shule.
Watoto wanaosoma ile shule wanaadhibika maana kutoka kituo cha daladala hadi kufika shule ni km kama 5 hivi.
Mkisikia Dar msidhani kote ni Posta au Ilala. Kuna vijiji huko.
Na sijui kama hata wana maabara na Maktaba hiyo shule.
Nina site kule, napajua ni shida.
Watoto wa Dar hawajazoea hizo shurba ila kwa vile no watoto wa Maskini inabidi tu waumie.
 
Hata ukichukua wanafunzi wote ambao wana akili sana ukawapa paper lazima apatikane wa kwanza mpaka wa mwisho hiyo ndio utaratibu wa evaluation

Vinginevyo hakuna maana ya mtihani tena

Examination is for evaluation and ranking haiwezekani wote muongoze lazima wa mwisho apatikane tu
Suala sio kupatikana wa kwanza na wa mwisho.
Kinachojadiliwa ni ufaulu.
Mfano ingetokea hakuna zero kabosa kwa shule zote, bado kungekua na aliongoza lakini matokeo yangeonesha wote wamejitahidi.
75% ya wanafunzi katika shule moja kupata zero sio jambo jepesi.
 
Wanafunzi "mateja"ndio ameshapata ufumbuzi.. Hakuna kujiuzuru au mtoa mada mchongo wako
 
Mkoa wa DSM umetoa shule sita za mwisho kwenye matokeo ya kidato cha nne-mitihani iliyofanyika 2016 na matokeo kutoka siku chache zilizopita.licha ya mkoa huu kuwa na makao makuu ya mamlaka zote za wadau wa elimu ,mkoa umedondokea pua.ni nini hasa kimechangia matokeo kuwa yalivyo?
 
Issue ya mkoa wake kufelisha kaizima na madawa ya kulevya.Huyu bwana Makonda alikuja na Mada yake hapa ya vijiwe vya madawa ya kulevya ndio alipopata pa kuanzia aishukuru pia JF
 
Matokeo ya form iv yametoka na 60% ya shule kumi za mwisho imetoka mkoa wa Dar es salaam.
Binafsi nilitegemea mkuu wa mkoa Bw Paul Makonda atatoka kuongelea ubovu wa matokeo kwenye mkoa anaoongoza anakuja kututangazia kuhusu watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa.Sisemi si sahihi kupiga vita biashara ya madawa ya kulevya ila nasema haikua wakati wake.Alichokitangaza hakikua cha emergency ila ilikua kutuondoa kwenye hoja ya kuhoji matokeo ya mkoa wake.Biashara ya madawa ya kulevya haikuanza jana wala juzi na utangazaji wake ungengoja issue ya matokeo ipite.Ila amefanikiwa kila mtu anongelea madawa,Wema SePetu na Tid
 
Inamaana hujui kuwa madawa ya kulevya ndo yamesababisha hizo shule kufanya vibaya???
 
SHULE ZINAZOONGOZA KUTOA WATEULE WA RAIS Ma RC, Ma DC na WABUNGE

View attachment 502651

Kitonga:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- Hakuna DIV IV- 9 DIV 0 64
Nyeburu:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- Hakuna DIV IV- 19 DIV 0 108
Masaki:
DIV I- Hakuna Div II- 2 DIV III- Hakuna DIV IV- 8 DIV 0 62
Mbopo:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- Hakuna DIV IV- 16 DIV 0 55
Mbondole:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- 3 DIV IV- 18 DIV 0-102
Somangila Day:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- 2 DIV IV- 8 DIV 0-45
Dahani:
DIV I- Hakuna Div II- 2 DIV III- 1 DIV IV- 11 DIV 0- 35
Ruponda:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- Hakuna DIV IV- 10 DIV 0- 30
Makiba:
DIV I- Hakuna Div II- 1 DIV III- 1 DIV IV- 21 DIV 0- 75
Kidete:
DIV I- Hakuna Div II- Hakuna DIV III- 1 DIV IV- 34 DIV 0- 95.
 
Back
Top Bottom