SoC03 Shujaa mwenye nguvu asiyejua kutumia silaha zake tena ni kipofu

Stories of Change - 2023 Competition
Jan 12, 2021
9
9
UTANGULIZI
Katika makala hii utaweza kujifunza juu ya shujaa huyu mwenye nguvu asiyeweza kutumia silaha zake, tena ni kipofu.

Shujaa ni neno lililotumika kuwakilisha bara ambalo lina vyanzo vingi vya kuingiza kipato. Vyanzo hivyo vimewakilishwa na neno "SILAHA". Bara hili halioni fursa lilizonazo, ndio maana ya neno kipofu.

Makala hii lengo lake ni kuamsha bara la Afrika kutoka katika usingizi,ili liweze kuona baraka ambazo limepewa na mwenyezi Mungu. Vivutio vya Kila namna vinapatikana Afrika, madini aina mbalimbali yanapatikana Afrika.

Hivyo karibu katika makala hii na upange kubadilishwa nayo kifikra na kimtazamo

SILAHA ZA SHUJAA MWENYE NGUVU
Silaha ni neno lililotumika Kama imagination kumaanisha "utajiri unaopatikana barani Afrika". Silaha hizi ni zidi ya adui aitwaye "umaskini". Adui huyu naye ana silaha zake, Kama vile njaa, kukosa elimu, uvivu, ulafi, ufisadi, uchoyo na ukandamizaji. Silaha za shujaa ni Kama zifuatazo.

1. MADINI
Madini ni silaha ambayo bara la Afrika limepewa ili lipambane zidi ya umaskini. Afrika ni bara pekee lililobarikiwa kuwa na aina nyingi za madini Kama vile Alimasi, dhahabu, shaba, makaa ya mawe, tanzanaiti, madini ya chumvi na gesi asilia. Ajabu kubwa ni hii, pamoja na kuwa na madini ya namna hii, bara la Afrika bado ni maskini wa kutupwa.

Wahuni wajuao kutumia silaha hii iitwayo madini hutoka mabara mengine,Kama vile Ulaya, Asia, Amerika ya kusini na kaskazini pamoja na Australia. Je umewahi jiuliza mtu ambaye hana baraka hizo ndiye anayekuwahi kuona baraka zako?. Du! Hii ni hatari Sana.
Hivyo Afrika amka sasa uone silaha yako hii uliyo nayo upambane na umaskini, Wala usimuuzie mzungu ambaye yeye akupewa baraka Kama zako.

2. ARDHI YENYE RUTUBA
Bara la Afrika limebarikiwa kuwa na silaha nyingine nyeti kabisa inayoweza kumfukuza, kumkamata na kumuuwa adui umaskini ambayo ni "ardhi yenye rutuba". Ajabu kubwa ni hii Afrika kadharau ardhi yake na kuanza kuiharibu kwa kutumia mbolea kutoka Ulaya na Asia. Mbolea ambayo imetoa ubora wa ardhi ya Afrika. Je waweza kumbuka enzi za mababu zetu, mazao yalivyokuwa yanastawi na kutoa mavuno mengi?.

Afrika ikumbuke thamani ya ardhi uliyonayo na uitumie vizuri ili isiharibike. Kumbuka mzungu alivyokutia mbaloni na kukukaba koromeo lako na kuitwaa ardhi yako enzi zile na akamshinda adui umaskini. Sasa ni zamu yako kuitumia silaha hii umshinde umaskini.

3. VYANZO VYA MAJI
Vyanzo vya maji barani Afrika ni kedekede tena ni karibu Kila mahali. Silaha hii ambayo ni bora na ya thamani, Afrika kaipiga teke na kuanza kulia huku ameshika kichwa akisema maisha ni magumu. Wewe Afrika umesahau matumizi ya maji?. Kumbuka ulivyokuwa ukiwafundisha vijana wako kuwa maji yanafaida Kama zifuatazo
  • Kufua umeme,
  • kuendeshea kilimo Cha Kila aina,
  • kunywa,
  • kuendeshea mitambo ya viwandani,
  • Kuendeshea shughuli za ufugaji na
  • Kufulia nguo.
Pamoja na elimu uliyoitoa kwa Wana wako lakini bado unalia umaskini. Basi amka uitumie vizuri silaha hii kwa kuanzisha kilimo Cha umwagiliaji Kila Kona, na viwanda vifunguliwe Kila mahali.

Halafu Afrika mbona umeme unakata Kila wakati huku una silaha Kama hii. Hivyo imarisha mitambo ya uzalishaji wa umeme kwa kuwa una maji ya kutosha.

4. VIVUTIO VYA UTALII
Afrika kabarikiwa kuwa na silaha nyingine dhidi ya umaskini iitwayo vivutio vya utalii. Huenda wengi hawajui hili yakuwa hata watu wake ni vivutio tosha Kama WAMASAI na WASUKUMA ambao bado wanajali tamaduni zao. Watu wengine ni wenyeji wa DRC, wale wafupi ni vivutio vya utalii.

Mito mirefu, maziwa bahari na milima, vyote hivi vinapatikana Afrika. Hebu angalia mlima Kilimanjaro na meru, jinsi watalii wanavyovutiwa navyo.

Mbuga za wanyama ngorongoro, Serengeti, Manyara, Mpanda na mbuga zingine zinazopatikana Afrika ususani nchi yetu ya Tanzania. Afrika bado hujui kuwa hii nayo ni silaha.

Mimea inayohisi mguso maarufu Kama MIMOSA PUDIKA yote hii ni fahari ya Afrika. Pia Vyura wenye kujifungua Kama binadamu ni Mali ya Afrika. Pamoja na kuwa na vivutio hivi huna maarifa navyo, hivyo amka usingizini uione fahari yako.

5. WATU WABUNIFU(WASANII)
Watu wabunifu ni wengi barani Afrika, lakini Wala hawas thaminiwi na kupewa kipaumbele ili kumshinda adui umaskini. Watu wenye kufua vyuma, wachoraji maarufu, waigizaji mahususi, Wana mziki bora na makanika maarufu wote watoka barani Afrika. Japokuwa wanavipaji vikubwa hawathaminiwi kwa sababu ya ngozi zao nyeusi kana kwamba na vipaji vyao ni vyeusi.

Sambamba na hayo madaktari bingwa Afrika wapo na wanauchumi wazuri wapo. Afrika nakuomba thamini kilicho chako ili adui umaskini akukimbie wa asirudi tena.

MAMBO YANAYOMFANYA SHUJAA MWENYE NGUVU AWE KIPOFU
Mambo hayo ni mambo yanayomfanya Afrika asione silaha zake za mapambano dhidi ya umaskini.

1. KUAMINI KUWA WEUSI WA NGOZI NI WEUSI WA AKILI
Ngozi ya mwafrika sio akili na hivyo waafrika wenye upeo wa akili na wenye maarifa juu ya Mambo ya uchumi wapo. Kwa sababu hiyo akili ya mwanadamu haipo kwenye ngozi yake.

Kwa hiyo watu wa bunifu na wenye maarifa wapewe ufadhiri wa kutosha ili aifikishe Afrika mahali palipo bora.

2. KUAMINI KUWA AFRIKA HAIWEZI KUISHI BILA MZUNGU
Kutokana na fursa za kuinuka kiuchumi zinazopatikana Afrika zinaweza kuifanya Afrika isiwe tegemezi kutoka kwenye mataifa ya Ulaya na Asia. Hivyo misaada kutoka mabara mengine si kitu kwa Afrika kwani ni tajiri mno.

Shida ni kwamba kuanzia viongozi hadi raia wa kawaida eanafikra potofu juu ya uendeshaji wa maisha ya familia hadi ngazi ya mataifa ya bara kwa ujumla.

3. IMANI YA KUWA AFRIKA IMELAANIWA HIVYO HAIWEZI KUJIENDESHA
Bara pekee lenye utajiri wa pekee duniani kote, tena ni bara la pili kwa ukubwa eti linasemwa limelaaniwa. Huu nao ni ushamba uliokithiri kwa sababu bara hili limepewa baraka za pekee ili lishinde umaskini.

Hebu angalia watu wenye uwezo wa kufanya kazi kwa muda mrefu wanapatikana wapi? . Jibu ni Afrika, hivyo waafrika wamebarikiwa hata uwezo wa kufanya kazi na kuhimili magonjwa ya Kila namna.

4. KUBINAFSISHA UTAJIRI WA AFRIKA
Bara letu la Afrika limekuwa na kawaida ya kubinafsisha mali au utajiri uliopo. Mfano Migodi, Miradi ya Mafuta na vitu vingine vingi. Mbaya zaidi ni kuwa Watu wanaokuwa wanamiliki utajiri huo hutoa fedha kichele kwenye taifa husika. Jambo Kama hili hudidimiza uchumi wa bwana Afrika.

5. KUWA NA UTUMWA WA KIFIKRA
Afrika amekuwa mtumwa wa kifikra kwa muda mrefu pasipo yeye kujua. Mfano kupokea Kila jambo litokalo nchi za magharibi, ushoga naussgaji na kujisahau kushughulikia uchumi wake.

Basi waafrika tuamke sasa tuwe huru kuanzia fikra zetu hadi vitendo vyavkila siku. Kumbuka wewe ni mbarikiwa na sio mlaaniwa.

HITIMISHO
Silaha za mapambano dhidi ya umaskini tulizo pewa ni kwa ajili ya wazazi na watoto wa kiafrika ili wawe matajiri tena wenye nguvu. Mataifa ambayo hayana madini, vivutio vya utalii, mbuga za wanyama, vyanzo vya maji na ardhi yenye rutuba na yaje Afrika kukopa fedha. Kwa sababu bara letu lina utajiri mkubwa.

Viongozi na wenye vyeo waliopewa dhamana ya kuendeshea shughuli za nchi hadi bara wawe welevu na watambuzi wa vipaji vya raia walio nao ili bara letu liwe namba moja kwa Kila jambo.

Mwisho shukrani za dhati natoa kwa yule aliyepanga kubadilishwa na makala hii.
 
Back
Top Bottom