Shinyanga: Bodaboda wafanya vurugu, Polisi watumia mabomu kuwatawanya

Kweli TZ kuna nyumbu wengi. Hivi ameelewa alichokiandika. Bila shaka huyu ni darasa la nne failed.... Hujui alama za mkato, nukta, koma. Magufuli ana kazi kubwa sana ......:oops:
Sasa magufuli yeye anajua nini mpaka awe na kazi,yeye mwenyewe anatupa kazi.
 
Dereva Bodaboda Akiwa Amembeba Askari Adaiwa Kuigongesha Pikipiki Kwenye Nguzo na Kufariki

JUNE 7, 2017
Facebook0Twitter0Google+0WhatsAppViber


Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga leo limewatawanya madereva bodaboda zaidi ya 100 waliokuwa wanaandamana kuelekea eneo la Ibinzamata kwenye msibani kwa dereva mwenzao Joel Mamla (26) ambaye alifariki dunia jana akiwa amempakia askari wa usalama barabarani aliyekuwa amemkamata kwa kosa la kutokuvaa kofia ngumu (Helment).



Joel ambaye alikamatwa na askari waliokuwa kwenye majukumu yao ya kila siku, aliamuliwa kuelekea kituo cha polisi huku akiwa na askari amembeba kwenye pikipiki yake lakini baadaye anadaiwa kuwa alibadilisha uelekeo na kwenda Barabara ya Tinde huku akimwambia askari watakufa pamoja na kisha kuigongesha pikipiki kwenye nguzo ya alama za barabarani na baadaye kufariki dunia huku askari huyo akijeruhiwa.



Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Jumanne Murilo, amekiri kutokea kwa tukio hilo.

“Deereva bodaboda huyo baada ya kukamatwa aliamliwa apelekwe kituoni, ndipo akambemba askari PC Edmond, lakini kabla hawajafika kitunoni, ghafla alielekeza pikipiki mahala pengine huku akimwambia askari lazima wafe wote.





“Wakati pikipiki hiyo ikiwa mwendokasi, askari huyo alianza kujihami kumzuia lakini bahati mbaya hakufanikiwa na hatimaye kusababisha ajali hiyo iliyopelekea kifo,” alisema Kamanda Murilo.

Aidha alisema baada ya tukio hilo wananchi kwa kushirikiana na bodaboda walianzisha vurugu kwa kuwarushia mawe askari polisi, ndipo jeshi hilo lilipotumia nguvu ya ziada kupiga mabomu, ili kuimarisha usalama na hali ya amani ambpo hatimye kufanikiwa kuituliza.

Na:Gabriel Ng’osha/GPL
 
Hapa unahitajika uchunguzi huru, wananchi wanasema askari alimkaba boda, afande anasema boda aliwamwambia askari watakufa wote, nani mkweli hapa?
 
Sio mti ila ktk nguzo ya chuma ya kibao cha alama za barabarani kisha yeye kuangukia jabali.
 
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga leo limewatawanya madereva bodaboda zaidi ya 100 waliokuwa wanaandamana kuelekea eneo la Ibinzamata kwenye msibani kwa dereva mwenzao Joel Mamla (26) ambaye alifariki dunia jana akiwa amempakia askari wa usalama barabarani aliyekuwa amemkamata kwa kosa la kutokuvaa kofia ngumu (Helment)


Kwanini Jeshi letu bado linatumia approach ambazo ni very crude katika kukabiliana na wahalifu?
  • Kuna hili la kukaa barabarani kukamata magari ni la kizamani sana ukizingatia magari wanayokamata ni yaleyale kila siku, hapa nadhani walitakiwa kujua matatizo yaliyopo na kuweka mfumo wa kidigitali wa kutatua hayo matatizo ili wao wakapambane na wauaji wa askari Pwani
  • Hawa bodaboda ni bomu jingine, tusipokaa vizuri watakuwa ni jeshi jingine litakalopambana na jeshi la polisi, ni vyema kuainisha makosa yanayofanywa na hao bodaboda na kutafuta mbinu ya kisasa badala ya kukimbizana nao, tumeshuhudia vifo kadhaa vinavyosababishwa ha hao askari
 
Kilichofuatia ni "unyama" wa polisi.Piki piki za boda boda walizokusanya navkupelekwa kituoni z ilikuwa zinashushwa kama mchanga( kumwagwa/kutupwa chini).Ktk akili ya kawaida piki piki zina kosa gani?
 
Kwanini Jeshi letu bado linatumia approach ambazo ni very crude katika kukabiliana na wahalifu?
  • Kuna hili la kukaa barabarani kukamata magari ni la kizamani sana ukizingatia magari wanayokamata ni yaleyale kila siku, hapa nadhani walitakiwa kujua matatizo yaliyopo na kuweka mfumo wa kidigitali wa kutatua hayo matatizo ili wao wakapambane na wauaji wa askari Pwani
  • Hawa bodaboda ni bomu jingine, tusipokaa vizuri watakuwa ni jeshi jingine litakalopambana na jeshi la polisi, ni vyema kuainisha makosa yanayofanywa na hao bodaboda na kutafuta mbinu ya kisasa badala ya kukimbizana nao, tumeshuhudia vifo kadhaa vinavyosababishwa ha hao askari

Rushwa ni adui wa maendeleo
 
Wakati mwingine hawa madereva wa boda siwaelewi inaonyesha wana stress nyingi sana, ukichanganya na usumbufu wa maaskari na hali ngumu ya kupata Wateja kwa kweli wanaotumia huu usafiri ukipakiwa muombe tu mungu mfike salama.
 
Kuna siku alipita kijana wa bodaboda akitimuliwa na askari, mara askari naye huyo kapita yuko nduki.... mara kijana wa bodaboda huyo akirudi peke yake kumbe huko mbele ya safari askari kaingizwa maboya sijui aliachwa wapi.:D:D:D:D:D
 
kule morogoro kuna vodafasta mmoja anaitwa lama alishawasababishia vlema waendesha pkpk wengi kwa kuwakimbiza ovyo ila walimchkao siku alisabasha bodaboda mmoja kujiingiza kwnye gali kubwa na laia kuanza kumtembezea chichapo uyo vodafasta mwenzake baada ya kuona laiya wanazidi kumiminika akadandia daladala akakimbia na kumuacha mwenzake akiazibiwa adi leo uyo voda fasta agusi pkpk na hakuna habari ya vodafasta kukimbiza bodaboda..
Laia=Raia
 
Dereva bodaboda alikamatwa kwa kosa la kutokuwa na helmet (ambalo ni kosa kisheria), dereva huyo huyo akambeba askari kwenda nae kituoni kwa kosa la kutokuvaa helmet, je, walipopata ajali askari alivaa helmet au nae kafanya kosa lile lile?
 
Back
Top Bottom