Aise umesikia fursa hii ya shindano kwa wewe ambaye unayependa kuwa mfanyabiashara mkubwa? MO Entrepreneurs Competition ni mradi ulioandaliwa na Mo Dewji Foundation na Darecha Limited ili kutambua na kuendeleza juhudi za vijana wajasiriamali katika kukuza biashara zao hapa nchini Tanzania. Mkurugenzi wa makampuni ya METL na Mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Mohammed Dewjii ,atawasaidia vijana kufikia ndoto zao kwa kuwapatia mitaji, na ushauri wa namna ya kukuza biashara zao.
Ukitaka kushiriki na kuwa mmoja wa vijana watakaonufaika na fursa hii unaweza kutuma maombi kwa kutembelea tovuti ifuatayo: