wanafunzi wa darasa la
sita katika Shule ya Msingi
Kitongoni, mwenye umri wa
miaka 14 na kumsababishia
maumivu makali sehemu za
siri.
Hukumu hiyo ilitolewa jana
na Hakimu wa Mahakama
hiyo, Frola Mtariania, baada
ya upande wa mashtaka
kuthibitisha kuwa
mshtakiwa alitenda kosa
hilo.
Hakimu Frola, akitoa hukumu
hiyo, alisema mahakama
inatoa adhabu kali dhidi ya
mshtakiwa ili iwe fundisho
kwake na kwa viongozi
wengine wenye tabia ya
kikatili kama yake.
Alisema upande wa
mashtaka ulipeleka
mashahidi watano, pamoja
na kielelezo cha PF3,
ambacho kilithibitisha
kwamba Sheikh Bamba
mshtakiwa alitenda kosa
hilo.
Alipotakiwa kujitetea ili
kupunguziwa adhabu,
akiongozwa na wakili wa
kujitegemea Method
Kabuguzi, mshtakiwa
aliangua kilio na kuiomba
mahakama impunguzie
adhabu kwa sababu ana
familia inamtegemea.
Pia alidai ni kosa lake la
kwanza tena shetani
alimwingilia. Hakimu Frola
alitupilia mbali utetezi huo na
kusema:
"Mshtakiwa ukiwa kiongozi
wa dini, kitendo
ulichokifanya si cha kijamii
maana wewe ndiwe
unayefundisha watu
kuachana na maovu cha
kushangaza unakuwa ndiye
wa kwanza kuyatenda
maovu.
"Sasa utakwenda gerezani
miaka 30 ili ukajifunze tabia
ya kuwa kiongozi bora wa
dini, kwa sababu huku
uraiani umeshindwa kuishi
na jamii."
Awali, akisoma hati ya
mashtaka, Wakili wa Serikali
Anita Julius, alidai kuwa
Januari Mosi, mwaka huu,
saa 4 asubuhi eneo la Ujiji
Kigoma, mshtakiwa huyo
alibaka msichana huyo.
Ilidaikwa kuwa siku ya tukio
mtoto aliyebakwa akiwa na
pacha wake, ambao baba
yao ni rafiki wa sheikh huyo,
walikwenda kwa sheikh
huyo kwa ajili ya kuombewa
duwa na kufanyiwa dawa
kwa ajili ya kufaulu mtihani
wa kuingia darasa la saba.
Kwa mujibu wa hati ya
mashtaka, baada ya kufika,
Bamba alimtuma mwenzake
aende shuleni kuchukua
mchanga na ndipo
alipomfanyika kitendo hicho
yule aliyebaki.
Mwenzake aliporejea,
ilidaiwa kuwa alimkuta
pacha wake analia na
alipomuuliza alimjibu kuwa
amebakwa na Bamba.
Umati mkubwa wa wakazi
wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji,
wakiwamo waumini wa
msikiti aliokuwa akiswalisha,
ulikusanyika mahakamani na
kushuhudia Sheikh huyo
anapelekwa jela