Seth Benjamin: Alikufa kishujaa au kizembe?

ndayilagije

JF-Expert Member
Nov 7, 2016
7,491
8,300
Wasalaam,
Hilo jina bila shaka linajulikana na liliwahi kuwa maarufu Tanzania. Kiufupi ni kijana aliyekufa akiunga mkono azimio la Arusha. Ninachojiuliza ni kimoja tu,kufuatia hii tabia mpya ya watanzania kuchukia nchi na viongozi wao,kutokuwepo na uzalendo hivi ni nani anayemkumbuka huyu kijana siku hizi,na je kwa mtazamo wa kisasa huyu mwenzetu alikufa kishujaa kweli au kizembe tu.
 
Huyu SETH BENJAMIN alikufa kishujaa ila taifa letu.
Ni la laana halieshimu RAIA wake waliojitoa kwa UZALENDO.
Toka KISIASA.KIUCHUMI NA KIUTAMADUNI
Tumebaki Taifa lililokufa lenye viongozi kwenye wivu kwenye kulazimisha wakumbukwe wao kwa UOVU .
 
Duh Mkuu,umegonga mule mule,ila achana na hao wazwazwa unaoita viongozi maana mie mie sijawaona,sisi wenyewe vipi? Tunajali?
 
Msomali yule alikuwa na kiherehere mambo ya Watanzania yeye alikimbilia ya nini
 
alikufa kufaje mpaka iwe kishujaa au kizembe? naomba nieleweshwe.
 
Kila kitu ni tafsiri, umasikini au utajiri, maendeleo au lolote ni tafsiri tu. Hata aliyesema Azimio lilileta umasikini pia anaweza akawa sawa kwa minajili ya tafsiri zake za maendeleo na umasikini wa taifa na watu.
 
Duh Mkuu,umegonga mule mule,ila achana na hao wazwazwa unaoita viongozi maana mie mie sijawaona,sisi wenyewe vipi? Tunajali?
Mkuu sisi wenyewe tunajali lkn inabaki kwenye fahamu ya vichwa vyetu tu.Tukifa tunaondoka navyo hakuna hifadhi maalum sio kwenye makabrasha wala kwenye mitandao.
Serikali yetu kuanzia mtaa.kijiji kitongoji wilaya mkoa NA serikali kuu wote wamekufa tunarithisha vizazi vyetu mambo makubwa ya Ulaya yetu dorooo nakupa mfano mwaka 1968 kuna mwanariadha anaitwa STEPHEN ni Mtanzania aliyekimbia Olympic bahati mbaya alianguka na kuumia lkn baada ya matibabu akaendelea kukimbia na kumaliza mbio.
Vyombo vya hbr vya nje vikamfuata kumhoji kwann aliendelea kukimbia huku akiwa mgonjwa aliwajibu nimetumwa kuja kumaliza mbio.huyu mkimbiaji bado yupo na Olympic duniani inamtambua anatumiwa ticket kila Olympic kwenda kushuhudia mm nilimfahamu kupitia TBC waliwahi kumhoji na kuonesha tukio lake lkn Taifa limemsahau halimjui WAZUNGU wanamtambua na kumuona ni shujaa.
Jiulize wako wapi? Hawa
1-juma pondamali
2-Daud salum
3-Hassan Zitto/Mohammed Kajole
4-Salim Amir
5- Jella Mtagwa
6-Mohamed Aldof Rishard/Juma Mkambi/Nick Njohole
7-Omar Hussein Keegan
8-Hussein Ngulungu/Charles Boniface
9- Peter Tino
10- Mohammed Salim
11- Thuwen Ally/Charles Albeto
Sasa hili kikosi ndo kilichotufikisha fainali za Afrika 1980 nani? Anawakumbuka hawa na kuwaheshimu Huwezi kufanikiwa eti kwa kauli "Gabon mpaka kombe la Dunia" inatia kichefuchefu na Mungu kamwe hawezi kutupa baraka kwa kuwadharau wananchi wenzetu waliokuwa WAZALENDO wa kweli kuliko wa sasa ambao ni WAPIGA DEAL wenye kutaka KUKUMBUKWA.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…