Serikali yadai ongezeko la Bei ya Vyakula limetokana na uhaba wa mvua

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,591
8,810
Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la bei za vyakula nchini, kutokana na upungufu wa mvua na mahitaji makubwa ya chakula ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati kukiwa na taarifa za ongezeko la vyakula kutoka kwa wafanyabiashara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Desemba 15, Naibu Waziri wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema bei za bidhaa ya vyakula yakiwemo maharage na viazi mviringo vimepanda kutokana upungufu wa mvua.

Ametoa mfano baadhi ya vyakula ikiwemo mchele hadi kufikia Desemba mwaka huu kilo moja inauzwa kati ya Sh2,200 na Sh3,500, maharagwe yanauzwa kilo kati ya Sh2,200 hadi Sh3,650, mahindi kilo yakiuzwa kati ya Sh750 na Sh1,890 huku viazi mvirigo vikiuzwa kati ya Sh688 na 1,875 kwa kilo moja.

“Wizara hii inaratibu ukusanyaji wa taarifa za bei za bidhaa muhimu kama vile bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi kupitia maofisa wa biashara mikoa na Mamlaka ya za Serikali za mitaa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeendelea kukusanya taarifa za bei kutoka katika masoko nchini lengo la kukokotoa kiwango cha mfumuko wa bei kila mwezi,” amesema Kigahe.

Kutokana na hali hiyo amesemma Serikali inachukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo kwa ikiwa pamoja na kupeleka chakula kwenye maeneo yenye uhaba.

Amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia janga la ukame kupandisha bei za bidhaa za vyakula, akiwataka wafuate maadili ya kibiashara na ufanyaji wa biashara muda wote.

“Tunawahamasisha wenzetu wa Serikali za Mitaa wahakikishe wakulima wanapokusanya mazao yao wayapeleke sehemu husika ili wafanyabiashara hao wasiendelee kununua kwenye majumba ya watu,” amesema.

Mbali na hatua hizo, amesema pia Serikali inachukua hatua za muda mrefu ikiwa pamoja na kutengeneza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili wakulima walime mazao muda wote badala ya kutegemea mvua.

Kigahe alisema ili kuleta hauweni kwa msimu wa kilimo ujao Wizara ya Kilimo imetenga zaidi ya Sh700 bilioni kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha kutoka sh 200 bilioni kwa ajili ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
“Tutahakikisha tunahamasisha vijana kulima kilimo cha biashara,” amesema.

MWANANCHI
 
Mambo mengine yana chekesha japo nchi inakila kitu.

Ukiachana na mito na maziwa ila chini ya ardhi yetu asilimia ya ifadhi kubwa ya maji hipo.

Ndio yale wakulima wanadanganywa .kwanza naomba baraza la kiswahili waondoe ili neno mkulima maana kwa kizungu ni heshima kubwa labda peasant.

Kuna wizara nyingine zipo zipo tu ili mradi wizara zinaongeza choo majumbani na maofisini.

Chekeni siku mtakuja kusikia saudia arabia analima maindi na kasaidia tz
 
Unawaambia CCM ambao mwelekeo kwa sasa haina
 
..... “Wizara hii inaratibu ukusanyaji wa taarifa za bei za bidhaa muhimu kama vile bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi kupitia maofisa wa biashara mikoa na Mamlaka ya za Serikali za mitaa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeendelea kukusanya taarifa za bei kutoka katika masoko nchini lengo la kukokotoa kiwango cha mfumuko wa bei kila mwezi,” amesema Kigahe.

Kutokana na hali hiyo amesemma Serikali inachukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo kwa ikiwa pamoja na kupeleka chakula kwenye maeneo yenye uhaba.

MWANANCHI
Kwanza bei alizowasilisha zina walakini. Maharagwe kilo ni Tsjs 4,600 rejareja mtaani.

Mchele hakuna wa 2,200. Waziri anaonekana ni muumini wa ibada za uongo

Nimequote hapo passage inayoonesha nini kinafanyika sasa as suluhisho.
  1. Wanaratibu ukusanyaji wa bei.
  2. Wanaratibu ukokotozi wa bei kujua monthly inflation
  3. Wwnapeleka chakula kwenye uhaba.
  4. Anakemea wanaopandisha bei
Hebu tuwe na tafakuri hapo. Wizara imesema mpango mkakati wake kukabiliana na hali hii.

  • Tunatoka maeneo tofauti ya nchi hii. Je ni wapi ambapo kuna chakula kimepokelewa kutoka serikalini na ugavi wake kwa wananchi unafanyikaje?
  • Wakisharatibu kukusanya bei za bidhaa kisha nini kinafuatia?
  • Wskishakokotoa monthly inflation so what is next?
  • Kwa nini serikali inakuja na visingizio kilakukicha bila aibu?
IToshe kusema kuwa CCM imefika ukomo wa kimtazamo na kifikra hivyo kilichobaki sasa ni kusimika.makuhani wa uongo kila position

Very shame kwa nchi yetu kuwa na mkwamo kiuchumi kwa wakati huu
 
Tatizo ni Bashe kufungulia mipaka
Watu tulipiga kelele sana humu tangu mwaka jana kuwa chakula kisivushwe mipaka kiholela. Huyo Bashe kwa jeuri akasema nchi ina chakula cha ziada cha kutosha. Watu toka nchi jirani wanakwenda mpaka vijijini wananunua shamba zima kabla hata mazao hayajakomaa. Tukapaza sauti hata kwa Mama kuwa amkanye mwanaye... Wapi wote wameweka pamba masikioni. Sasa watanzania tunateseka. Tunaomba 2025 ifike haraka.
 
Walisingizia vita kimewashuka saiv wanasingizia mvua wakati kanda ya ziwa mvua zinashuka za kutosha.

Tozo Tozo tatizo wamewabana sana wakulima
 
Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la bei za vyakula nchini, kutokana na upungufu wa mvua na mahitaji makubwa ya chakula ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati kukiwa na taarifa za ongezeko la vyakula kutoka kwa wafanyabiashara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Desemba 15, Naibu Waziri wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema bei za bidhaa ya vyakula yakiwemo maharage na viazi mviringo vimepanda kutokana upungufu wa mvua.

Ametoa mfano baadhi ya vyakula ikiwemo mchele hadi kufikia Desemba mwaka huu kilo moja inauzwa kati ya Sh2,200 na Sh3,500, maharagwe yanauzwa kilo kati ya Sh2,200 hadi Sh3,650, mahindi kilo yakiuzwa kati ya Sh750 na Sh1,890 huku viazi mvirigo vikiuzwa kati ya Sh688 na 1,875 kwa kilo moja.

“Wizara hii inaratibu ukusanyaji wa taarifa za bei za bidhaa muhimu kama vile bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi kupitia maofisa wa biashara mikoa na Mamlaka ya za Serikali za mitaa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeendelea kukusanya taarifa za bei kutoka katika masoko nchini lengo la kukokotoa kiwango cha mfumuko wa bei kila mwezi,” amesema Kigahe.

Kutokana na hali hiyo amesemma Serikali inachukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo kwa ikiwa pamoja na kupeleka chakula kwenye maeneo yenye uhaba.

Amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia janga la ukame kupandisha bei za bidhaa za vyakula, akiwataka wafuate maadili ya kibiashara na ufanyaji wa biashara muda wote.

“Tunawahamasisha wenzetu wa Serikali za Mitaa wahakikishe wakulima wanapokusanya mazao yao wayapeleke sehemu husika ili wafanyabiashara hao wasiendelee kununua kwenye majumba ya watu,” amesema.

Mbali na hatua hizo, amesema pia Serikali inachukua hatua za muda mrefu ikiwa pamoja na kutengeneza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili wakulima walime mazao muda wote badala ya kutegemea mvua.

Kigahe alisema ili kuleta hauweni kwa msimu wa kilimo ujao Wizara ya Kilimo imetenga zaidi ya Sh700 bilioni kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha kutoka sh 200 bilioni kwa ajili ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
“Tutahakikisha tunahamasisha vijana kulima kilimo cha biashara,” amesema.

MWANANCHI
Yaani karne hii ya teknologia na sayansi ya juu kabisa serikali imewekeza kwenye kilimo cha kudra ya mwenyezi Mungu badala ya kilimo cha umwagiliaji?
Cha ajabu hata umeme ni hivyo hivyo. Kama mvua zisiponyesha bwawa la uzalishaji umeme la nyerere ni shimo la mgodi uliokwisha vunwa.
Yaani halina maana yeyote.
 
Watu tulipiga kelele sana humu tangu mwaka jana kuwa chakula kisivushwe mipaka kiholela. Huyo Bashe kwa jeuri akasema nchi ina chakula cha ziada cha kutosha. Watu toka nchi jirani wanakwenda mpaka vijijini wananunua shamba zima kabla hata mazao hayajakomaa. Tukapaza sauti hata kwa Mama kuwa amkanye mwanaye... Wapi wote wameweka pamba masikioni. Sasa watanzania tunateseka. Tunaomba 2025 ifike haraka.
Mtafika mmechoka sana. Siyo tu ninyi mlipaza sauti, hii kitu naamini hata vyombo vya ulinzi na usalama vilishauri, hakuna kitu hufanyika bila kitengo, naamini kabisa walishauri ila hawakusikilizwa. Hapa ngoma bado mbichi sana. Tuzidi kumuomba Mungu tu
 
Serikali imekiri kuwepo kwa ongezeko la bei za vyakula nchini, kutokana na upungufu wa mvua na mahitaji makubwa ya chakula ndani na nje ya nchi.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja wakati kukiwa na taarifa za ongezeko la vyakula kutoka kwa wafanyabiashara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana Desemba 15, Naibu Waziri wa wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amesema bei za bidhaa ya vyakula yakiwemo maharage na viazi mviringo vimepanda kutokana upungufu wa mvua.

Ametoa mfano baadhi ya vyakula ikiwemo mchele hadi kufikia Desemba mwaka huu kilo moja inauzwa kati ya Sh2,200 na Sh3,500, maharagwe yanauzwa kilo kati ya Sh2,200 hadi Sh3,650, mahindi kilo yakiuzwa kati ya Sh750 na Sh1,890 huku viazi mvirigo vikiuzwa kati ya Sh688 na 1,875 kwa kilo moja.

“Wizara hii inaratibu ukusanyaji wa taarifa za bei za bidhaa muhimu kama vile bidhaa za vyakula na vifaa vya ujenzi kupitia maofisa wa biashara mikoa na Mamlaka ya za Serikali za mitaa, Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeendelea kukusanya taarifa za bei kutoka katika masoko nchini lengo la kukokotoa kiwango cha mfumuko wa bei kila mwezi,” amesema Kigahe.

Kutokana na hali hiyo amesemma Serikali inachukua hatua za dharura kukabiliana na hali hiyo kwa ikiwa pamoja na kupeleka chakula kwenye maeneo yenye uhaba.

Amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia janga la ukame kupandisha bei za bidhaa za vyakula, akiwataka wafuate maadili ya kibiashara na ufanyaji wa biashara muda wote.

“Tunawahamasisha wenzetu wa Serikali za Mitaa wahakikishe wakulima wanapokusanya mazao yao wayapeleke sehemu husika ili wafanyabiashara hao wasiendelee kununua kwenye majumba ya watu,” amesema.

Mbali na hatua hizo, amesema pia Serikali inachukua hatua za muda mrefu ikiwa pamoja na kutengeneza miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji ili wakulima walime mazao muda wote badala ya kutegemea mvua.

Kigahe alisema ili kuleta hauweni kwa msimu wa kilimo ujao Wizara ya Kilimo imetenga zaidi ya Sh700 bilioni kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha kutoka sh 200 bilioni kwa ajili ya miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
“Tutahakikisha tunahamasisha vijana kulima kilimo cha biashara,” amesema.

MWANANCHI
SASA KAMA KUNA UHABA WA MVUA , HAPO NA UHABA MAJI UNAFUATA NYUMA.
SASA UNASHAURI TUMWAGILIE KWA KUTUMIA NINI?
KWANINI WAZIRI ASIANZE NA KUPANDA KWA BEI ZA PETROLI?
Na uhaba/ughali wa mbolea mwanzoni kabisa mwa 2022.
 
Tatizo ni Bashe kufungulia mipaka

NAUNGA mkono hoja…
Halafu Kuna watu wanamkingia Kifua eti anajua Uchumi…
Yeye inawezekana akawa sahani moja na wafanyabiashara halafu anasema wacha wakulima wapate faida!
Hivi wapate faida Gani?
ana uhakika kuwa hiyo faida inamfikia Mkulima Moja kwa moja?
je Unawezaje kuruhusu Chakula kiuzwe nje ya Nchi wakati kwako huna nasema tena huna Uhakika wa Chakula?
eti anasema tuna Akiba ya Kutosha,
Yeye tumwambie awepo kwenye hiyo akiba kwenye list awe anawekewa debe 3 za mahindi Kiufupi awe anapimiwa nafaka kutoka ghalani, Tuone kama atakuwa na Amani!
Somalia kupitia Unicef,Undp ndio wanapewa chakula cha dharura mgao cha kupimiwa,Ukishafika haki hiyo hata mambo mengine hayataenda vema kama Elimu kufikiri,Amani,Nk nk.
Yeye anaweza kusema Tunaa tunaaa akiba ya Kutosha ghalani! sasa mbona hajafungulia hicho chakula kiuzwe kwa bei nafuu kutoka ghalani ili kushusha bei sokoni?
Hiyu ni Mwanasiasa sio Anaendesha Mambo kisiasa!
Imagine:
Kanda ya Ziwa Victoria,Shinyanga Salawe wanalima sana Mchele palitakiwa Kuwe na Kilimo cha aumwagiliaji toka Ziwa victoria sababu maji yanafika pale na Ni karibu mazao yangekuwa mengi mnooo!
uje Nyanda za juu kusini Mbeya! na Nyasa Kulitakiwa kuwe pia na Kilimo cha Umwagiliaji
Morogoro pia.
Lakini watu wanajali Matumbo yao tuu oia ni wabinafsi hawataki kudikiliza Ushauri wa Wataalam.
huyo Baashe kisiasa ni Mzuri alipaswa kuendelea kuwa naibu wwaziri tuu!
kitu Cha Kwanza maadui hutafuta nchini kwako ni kuhakikisha usiweze kujitosheleza kwa chakula.
na wanapitia kwa mawaziri kam hawa kina Bashe!
Namuonea Huruma Raisi Mama Samia Suluhu Hassan!
 
Back
Top Bottom