Serikali/TRA yazitaka Benki kutopandisha viwango vya tozo/ VAT katika miamala yake

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Habari wanaJF,

Nimepenyezewa hii taarifa,

=====================

Kwakifupi ni kwamba Serikali imezuia Benki kupandisha viwango vya tozo katika miamala yake na kuelekeza gharama hizo kwa wateja wao.

Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa asilimia 18 ya VAT mpya iliyopitishwa kwenye miamala ya benki inahusisha gharama zilizokuwa zikitozwa na benki hizo kwa wateja wao lakini serikali ilikuwa haipati chochote.

Kidata amesema kuwa Benki Kuu imeelekezwa kudhibiti benki hizo kwa kufanya ujanja wa kuongeza makato kwenye miamala ya wateja wao wakati wakijua fika kuwa hilo si lengo la kodi hiyo mpya.

Ameelekeza kuwa kiwango cha kodi kinachotozwa kwenye miamala hiyo kinatakiwa kubaki kama mwanzo lakini serikali itakata kodi yake ya asilimia 18 na kodi nyingine zilizopo kwa mujibu wa sheria.

==========

UPDATES:


==========

Mamlaka ya mapato Tanzania 'TRA' imetoa ufafanuzi kuhusu kodi ya ongezeko la thamani kwenye huduma za kifedha kuwa marekebisho ya sheria ya mwaka 2014 yaliyopitishwa na bunge yanayolenga kutoza kodi la ongezeko la thamani kwa kiwango cha 18% kwenye ada ambazo benki inatoza wateja wake kwenye huduma mbalimbali zitolewazo na benki au taasisi za fedha.

TRA wamesema taasisi za fedha wanapoongeza makato ya miamala ya fedha wanakosea kwa kupandishia wananchi kwa kuwa sheria hiyo inahusu fedha ambayo mwanachi alikuwa anakatwa na taasisi hizo ambayo hapo mwanzoni zilikuwa azilipiwi kodi kwa hiyo hizo ndizo zitakazokatwa 18%.

Mfano kama umetoa fedha ukakatwa 1000 na taasisi ya fedha ilikuwa haikatwi kodi lakini kwa sheria hiyo ada hiyo ndio itakatwa 18% na sio mwananchi kuongezewa makato kama ilivyofanyika kwa baadhi ya taasisi za fedha.



 
wakati unasema hivyo leo nimelia, zimeondoka kama elfu ishirini hivi
 
Duuh mugu ajaalie tetesi iwe kweri maana roho zilishatoka mahala pake
 
Duh....mbona kama kuna sheria zinzsiginwa hapa!?
 
Hii tetesi kama ni kweli basi kuna uwezekano mkubwa swala likafika mahakamani. Mabenki sidhani yatakubali. VAT kwa uelewa wangu ni kodi ya mlaji (consumption tax) na hata siku moja hailipwi na mfanyabiashara/mtoa huduma. Labda wataalamu waje watusaidie.
 
Na iwe hivyo maana napanga kuachana kabsa na huduma za kibenki hasa nikikumbuka ile tetesi ya kukatwa 18% kwenye pesa ya mteja
 
Hiki nacho kilikuwa kipimo kwa serikali kama ina nia njema na sisi wananchi. Kulipa kodi wajibu wangu raia.

Lakini Raia masikini kuilipia benk kodi sio sawa.

Kama benk walipata kipato bila kukilipia kodi. Sasa serikali ikahitaji kodi yake kutoka kwenye hicho kipato. Badala ya benk kulipa hiyo kodi kama mimi ninavyolipa kodi cha ajabu leo Benk inakuja kuchukua hiyo Pesa kwangu tena niilipie.

Ni kujitengenezea ugumu wa maisha wa kujitakia. Hata kama ni Tetesi naomba iwe hivyo vinginevyo ilikuwa haina maana vya budget kusomwa Live, alafu tuilipie benk kodi na serikali ibaki inaangalia. Kama sielewi maana ya hii 18% naomba na mimi nielimishwe.
 
Ila nakumbuka lengo la Serikali ilikua kwamba kinacho kusanywa na bank kama service charge ndicho kilipiwe kodi na bank zenyewe na sio mwananchi kulipishwa liba juu ya service charge kama mabenki yanavyotaka iwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…