Uzima Tele
JF-Expert Member
- Jan 20, 2023
- 1,270
- 2,820
Mchungaji ☝️☝️na mwimbaji wa injili ndugu Mbarikiwa Mwakipesile
Mtoto ☝️☝️wa Mch Mbarikiwa Mwakipesile anayedaiwa kuuliwa na aliyekuwa mkuu wa TISS akishirikiana na RSO wa Mbeya..
==================================================
Huyu mchungaji ni kiongozi wa huduma ya kutangaza injili (Neno la Mungu) inayojulikana kwa jina la Kikosi Kazi Cha Injili..
Kwa sasa ni miongoni mwa watu maarufu sana Tanganyika. Kabla ya hapo binafsi sikuwa namjua kwa jinsi ninavyomjua sasa kupitia sakata hili..
Kupitia YouTube channel yake inayojulikana kama Kikosi Kazi Cha Injili Tv na kwa mahubiri na maelezo yanayorushwa kila siku kupitia channel hii, inaonekana wazi kuwa kuna ugomvi mkubwa kati ya serikali/polisi na mtu huyu..
Ni wazi kuwa mahubiri yake ni ya tofauti sana na wahubiri wengine. Yake wakati wote ni kukemea UOVU wa viongozi wa serikali na kusisitiza watu na hususani viongozi wa serikali kutenda HAKI kwa watu wanaowaongoza...
Hili limemletea shida na ugomvi mkubwa na mbaya sana na baadhi ya viongozi wa serikali. Na viongozi hawa wa serikali kwa kulitumia jeshi la polisi na mamlaka zingine za kiserikali, wamekuwa wakimwandama na kujaribu kumtafutia jinai ili pengine wamfunge au wamnyamazishe kabisa..
Yeye kaapa Kwa jina la Mungu wake kuwa, hatanyamaza mpaka aidha CCM na serikali yake ianguke na kutoweka kabisa au wamuue yeye. Na hata wakimuua watakaobaki hai wataendeleza mapambano haya..
Na kuthibitisha kuwa yuko very serious, maombi ya kuombea kusudi hili (kuanguka kwa utawala wa CCM) yanaendelea kufanyika kila siku kanisani kwake ili ijulikane ni Mungu yupi wa kweli atawalaye kati ya wanadamu na Tanganyika aidha wa Samia Suluhu Hassan na CCM yake au ni wa Mch Mbarikiwa Mwakipesile..
Hii inanikumbusha tukio la ugomvi kama huu lililorekediwa kwenye Biblia kati ya nabii Eliya aliyeamua kumkabili Mfalme (Rais) Ahabu na mkewe mchawi Malkia Yezebel waabudu miungu ya Mabaali..
Yaani hapa ni sawa na kusema Mungu ashindane na kiumbe chake alichokiumba mwenyewe... Ni ajabu eeh..!!??
(Soma kisa hiki chote kwenye Biblia yako kutoka kitabu cha 1 Wafalme 18: 1 - 46)
Turudi kwenye kisa cha Mch Mbarikiwa Mwakipesile. Anasema amefungiwa mlango kila mlango wa ofisi ya serikali alikoenda kupata msaada au huduma:
Mfano, anasema:
1. Serikali imekataa kuipa usajili kamili huduma na kanisa lake. Kwa maelezo yake, hapewi sababu ya kwanini kanisa lake lisisajiliwe hata baada ya kuwasilisha nyaraka zote zinazohitajika kisheria na mara zote ni kuambiwa njoo kesho na akienda anakumbana na kizingiti kingine..
Kwa hulka yake ya kutonyamazia uonevu wowote, hili limekuwa ajenda kuu ktk mahubiri yake na Kila anapopata nafasi ya kuongea kupitia YouTube channels yake huku akiwatuhumu viongozi wa mamlaka husika kwa figisu figisu wanazomfanyia hata kukataa au kuendelea kuchelewesha kutoa usajili wa kanisa lake. Hata hivyo hiyo haijamzuia kumwabudu Mungu wake..
Kwa sababu hii serikali ikamfungilia mashitaka na kesi iko mahakamani huko Mbeya..
2. Kwa maelezo yake ni kwamba, kuna dalili na ishara zote zinazoonesha kuwa huko mahakamani amewashinda pia..
Lakini Kwa sababu ya mfumo wa uovu unaotawala serikalini, watesi wake wameshaingia hata huko mahakamani kuhakikisha kuwa hapati haki yake anayoitafuta.
Naye kama ilivyo hulka yake, hanyamazi bali nje ya mahakama huendelea kushusha tuhuma na huku sasa na mahakama au mahakimu wanaosimamia shauri lake nao wameshaingia kwenye 18 zake. Vita imekuwa kali, watawala wakitumia fedha na mamlaka za kiserikali kama silaha yao kupingana, huku Mch Mbarikiwa Mwakipesile alitumia silaha ya Neno la Mungu a.k.a upanga wa roho..
Hili likiwa linaendelea binti yake akafa ktk mazingira ya kutatanisha na anayetuhumiwa kumuua huyo binti ni RSO wa Mbeya akitekeleza maagizo ya aliyekuwa mkuu wa TISS ambaye sasa ni balozi nchi fulani. Na kwa maelezo ya Mch Mbarikiwa Mwakipesile ni kuwa, ana ushahidi wa kauli ya mkuu wa TISS akijigamba kuwa ni lazima afanye hivyo (amuulie mtoto wake) ili aweze kutosha kwenye nafasi yake..
Ugomvi sasa umekuwa mkubwa na inaelekea ni kama wanaotuhumiwa (polisi & viongozi wanasiasa wa serikali) wameshashindwa kumnyamazisha. Badala yake wameanza kukamata na kuwatia ndani baadhi ya waumini wa mchungaji huyu kwa makosa mbalimbali..
Mmoja aliyekamatwa na kuwekwa ndani kwa siku 4 sasa bila kufikishwa mahakamani ni Binti mdogo aitwaye Sifa Boniventure mshirika na mwimbaji wa nyimbo za injili toka kanisani kwa mchungaji huyu akituhumiwa kurekodi na kuimba wimbo wenye maudhui ya uchochezi kwa mujibu wa polisi hawa Mbeya..
Polisi wameenda mbali zaidi, wanadai wanatilia shaka uraia wa binti huyu maana inawezekana si Mtanzania kwa sababu tu ya kuimba wimbo kuikosoa serikali kuhusu mkataba wa bandari, vurugu za kuhamishwa kwa lazima wamasai wa Loliondo na Ngorongoro, kukatikatika kwa umeme, polisi kuua mtoto wa mchungaji wake na pasipo hatua za kisheria kuchukuliwa kwa waliohusika..
Na katika wimbo wake huyu binti anadhani pengine viongozi wa serikaliBhii wanawaona wananchi wanaonyanyasika na kutendewa mabaya yote haya kama vile manyani (Kwa maana ya wanyama) tu na sio binadamu..!
Kwa maneno haya polisi wanasema kuwa HUO NI UCHOCHEZI DHIDI YA SERIKALI ILI ICHUKIWE NA WANANCHI.!!
Sasa Mimi binafsi najiuliza ni hili tu au kuna kitu kingine wanakitafuta toka kwa mchungaji huyu? Na Je, kupitia wimbo huu kweli Kuna uchochezi hapo?
Na Je, sio kweli kuwa serikali yenyewe kupitia matendo ya viongozi wake ndiyo inayojichochea na kutaka ICHUKIWE na wananchi?
==================================================
UPDATES.
SIFA BONIVENTURE BUJUNI na HEZEKIA WAACHIWA HURU TOKA MAHABUSU YA POLISI KWA DHAMANA LEO TAREHE 20/9/2023
Ni baada ya kukaa mahabusu ya polisi kati Mbeya kwa siku zaidi ya 5 bila kupelekwa mahakamani kinyume kabisa sha sheria Kwa kosa linalodhaniwa kuwa ni la uchochezi..