Serikali ije na namna ya kuwabana waandaji wa Marathon kuchangia Maendeleo ya nchi!

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
12,247
13,910
Kwanza napenda ku declare interest kwamba mimi ni mmoja wa wakimbiaji kwenye club mojawapo mkoani (social runner), nimeona kuna mwanya serikali inapoteza mapato!!!

Back to the topic,
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi la waandaaji wengi wa mbio mbalimbali ukiacha ile maarufu kama Kilimanjaro Marathon inayofanyika kila mwaka Moshi- Kilimanjaro.

Mbio hiyo ni kongwe na imekuwa ikitoza gharama za kushiriki ya Tsh. 20,000 au chini ya hapo ukiwahi zaidi. Hata hivyo naamini serikali inapata pato kwa maana ya kodi kutokana mbio hizo.

Hivi karibuni kumekuwa na waandaaji wa mbio mbalimbali, shida ninayoiona hapa ni namna ambavyo serikali inaweza kupata kodi kwenye mbio hzo ambazo nyingi zimekuwa zikitoza kiingilio cha ushiriki kikubwa sana zaidi hata ya zile.mbio kubwa za Kili Marathon (mfano 25,000-60,000)

Sasa kwa hili naomba kuishauri serikali yafuatayo;

1. Kuwe na gharama elekezi kwa mbio zote, siyo kila muandaaji anakuja na gharama zake, ghrama ziwe reasonable na zenye kushawishi wengi kushiriki mazoezi. (Mfano Full marathon 25,000/=, Half Marathon 20,000) etc...

2. Serikali iangalie utaratibu ambao kutakuwa na tozo kwa maana ya %ya kila mshiriki iingie ili kuchangia maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi.

3. Serikali ihakikishe na ihamasishe kila club ya Jogging inakuwa registered na kila ada ya mwanamchama anakatwa % inaingia katika mfuko maalum kuchangia maendeleo ya nchi.

Najua kwa idadi ya mbio zilizopo kwa mwaka, na idadi ya clubs za Jogging zilizopo kila wilaya au mkoa serikali ikiweza kuratibu hili vema itapata fedha walau za kuchangia kwenye maendeleo ya nchi. Kikubwa ni kusaidia club hizo ziwe active na kuwa na member wa kutosha.
 
Mazoezi ni kwa afya.. sio starehe... bora waongeze kodi kwenye bia na sigara.. sio marathons.. watu wataacha kukimbia afya zitaharibika taifa litapoteza nguvukazi
 
Nadhani serikali ingechochea kuwa na marathon zaidi.

Ingependeza tukawa taifa la michezo.

Ihakikishe inapunguza viingilio na kuhamasisha watu binafsi na taasisi kushiriki.
 
Nakuunga mkono maana wanatoza pesa kubwa ambayo hailingani na ushiriki yaam mfano kili marathon kiingilio let say 20000 washiriki 10000 unapata jumla ya pesa ni 200,000,000 na zile medali zile medali ziko vile vile miaka yote hawaziongez hata hadhi kidogo maana kamba za medali wanapewa tigo maji wanapewa na kampuni ya coca na hospital zinatoa watu wa huduma za afya lakin hata wakipewa 30000 hata wakiwa 1000 kwa siku moja hata haipunguzi kitu hata watu wa usafibwakipewa 2m bado hela inabaki ya kutosha wasaniii wakipewa 15m faida inakuwepo tu, mgeni rasmi akipewa 500k wala hata sumbua askari wakipewa hata 2m ulinzi unakuwa wa kutosha uwanja wa ujikodishwa hata kwa 20m hakuna hasara yoyote.
Sasa bora serikali iingilie kati au medali ziendane na gharama za kiingilio maana week hiyo ya kili marathon bar zote moshi zinajaa lodge nzur zote zinafurika
 
Hukusikia hesabu za kodi walizopelekewa waandaji wa Kill Marathon mpk wakataka kususa sio?
Kwa Kili its ok, lkn zipo Marathon nyingi tu katika Mwaka wa Calendar...nikiangalia calebdar ya marathon hapa kuna zaidi ya Marathon 27.

Naongea kwa nia njema.
 
Mazoezi ni kwa afya.. sio starehe... bora waongeze kodi kwenye bia na sigara.. sio marathons.. watu wataacha kukimbia afya zitaharibika taifa litapoteza nguvukazi
Mkuu, kama ni mtu wa mazoezi huwezi subir hadi Marathon ndipo ufanye mazoezi.
 
Kwanza napenda ku declare interest kwamba mimi ni mmoja wa wakimbiaji kwenye club mojawapo mkoani (social runner), nimeona kuna mwanya serikali inapoteza mapato!!!

Back to the topic,
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi la waandaaji wengi wa mbio mbalimbali ukiacha ile maarufu kama Kilimanjaro Marathon inayofanyika kila mwaka Moshi- Kilimanjaro.

Mbio hiyo ni kongwe na imekuwa ikitoza gharama za kushiriki ya Tsh. 20,000 au chini ya hapo ukiwahi zaidi. Hata hivyo naamini serikali inapata pato kwa maana ya kodi kutokana mbio hizo.

Hivi karibuni kumekuwa na waandaaji wa mbio mbalimbali, shida ninayoiona hapa ni namna ambavyo serikali inaweza kupata kodi kwenye mbio hzo ambazo nyingi zimekuwa zikitoza kiingilio cha ushiriki kikubwa sana zaidi hata ya zile.mbio kubwa za Kili Marathon (mfano 25,000-60,000)

Sasa kwa hili naomba kuishauri serikali yafuatayo;

1. Kuwe na gharama elekezi kwa mbio zote, siyo kila muandaaji anakuja na gharama zake, ghrama ziwe reasonable na zenye kushawishi wengi kushiriki mazoezi. (Mfano Full marathon 25,000/=, Half Marathon 20,000) etc...

2. Serikali iangalie utaratibu ambao kutakuwa na tozo kwa maana ya %ya kila mshiriki iingie ili kuchangia maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi.

3. Serikali ihakikishe na ihamasishe kila club ya Jogging inakuwa registered na kila ada ya mwanamchama anakatwa % inaingia katika mfuko maalum kuchangia maendeleo ya nchi.

Najua kwa idadi ya mbio zilizopo kwa mwaka, na idadi ya clubs za Jogging zilizopo kila wilaya au mkoa serikali ikiweza kuratibu hili vema itapata fedha walau za kuchangia kwenye maendeleo ya nchi. Kikubwa ni kusaidia club hizo ziwe active na kuwa na member wa kutosha.
Mh! Hujatafiti! 30,000/= na 25,000/= ni ada kubwa! Mbio za nchi nyingine Kenya, South Africa na Nigeria mfano ambako makampuni makubwa makubwa yanatoa udhamini mkubwa wa mbio hizo za barabarani shilingi ngapi ada!!!
Natazama mtandaoni mbio za ulaya na marekani ni hadi USD $ 250 sawa na shilingi laki tano na elfu 75(575,000/=) south africa mbio kushiriki ada dola 100 hadi 150. Na hapo kumbuka kuna wadhamini wakubwa wakubwa.
kuandaa mbio gharama kubwa sana elfu 25 si bei ya kukodi gesti ya kawaida tu. Mbio ulipie ada chama cha riadha, uwalipe watu wa chama wapime njia waje kusimamia, uwalipe wasimamizi vituoni, uandae maji soda glucose magari ya ambulance, utangaze mbio gazetini redioni, ktk bado zawadi za washindi takataka kibaoooo na wewe upate faida mana siyo kazi ya bure ulipe TRA kodi.
Wanariadha wa Usangi unawaowaita kuchangiwa na waandaaji na washiriki binafsi wa mbio wkt serikali na wizara ya michezo zipo si sahihi.
hicho kibano unachopendekeza nia ni.kuua mbio za barabarani kabisaaaaaaa watu wakose chanzo kizuri cha hamasa ya mazoezi. Watu wengi wanazidi kuanza mazoezi ya mbio sababu ya mbio hizi za barabarani. Hoja yako itaua mchezo wa mbio za barabarani.
 
Mazoezi ni kwa afya.. sio starehe... bora waongeze kodi kwenye bia na sigara.. sio marathons.. watu wataacha kukimbia afya zitaharibika taifa litapoteza nguvukazi
Achaa Mambo ya ajabu wewee.....kwanini kwenye bia ndo Kodi iongezwee....huko kwenye marthon Kuna asilimia kubwa Kuna wawindaji wa papuchii na wadangaji
 
Kwanza napenda ku declare interest kwamba mimi ni mmoja wa wakimbiaji kwenye club mojawapo mkoani (social runner), nimeona kuna mwanya serikali inapoteza mapato!!!

Back to the topic,
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka wimbi la waandaaji wengi wa mbio mbalimbali ukiacha ile maarufu kama Kilimanjaro Marathon inayofanyika kila mwaka Moshi- Kilimanjaro.

Mbio hiyo ni kongwe na imekuwa ikitoza gharama za kushiriki ya Tsh. 20,000 au chini ya hapo ukiwahi zaidi. Hata hivyo naamini serikali inapata pato kwa maana ya kodi kutokana mbio hizo.

Hivi karibuni kumekuwa na waandaaji wa mbio mbalimbali, shida ninayoiona hapa ni namna ambavyo serikali inaweza kupata kodi kwenye mbio hzo ambazo nyingi zimekuwa zikitoza kiingilio cha ushiriki kikubwa sana zaidi hata ya zile.mbio kubwa za Kili Marathon (mfano 25,000-60,000)

Sasa kwa hili naomba kuishauri serikali yafuatayo;

1. Kuwe na gharama elekezi kwa mbio zote, siyo kila muandaaji anakuja na gharama zake, ghrama ziwe reasonable na zenye kushawishi wengi kushiriki mazoezi. (Mfano Full marathon 25,000/=, Half Marathon 20,000) etc...

2. Serikali iangalie utaratibu ambao kutakuwa na tozo kwa maana ya %ya kila mshiriki iingie ili kuchangia maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi.

3. Serikali ihakikishe na ihamasishe kila club ya Jogging inakuwa registered na kila ada ya mwanamchama anakatwa % inaingia katika mfuko maalum kuchangia maendeleo ya nchi.

Najua kwa idadi ya mbio zilizopo kwa mwaka, na idadi ya clubs za Jogging zilizopo kila wilaya au mkoa serikali ikiweza kuratibu hili vema itapata fedha walau za kuchangia kwenye maendeleo ya nchi. Kikubwa ni kusaidia club hizo ziwe active na kuwa na member wa kutosha.
Nilikuwa natamani sana kuzungumzia hili suala hasa katika kipindi hiki cha tozo nyingi - 2022! Sehemu nyingine ya kuongeza pato la taifa ni hapa na si kuendelea kuwabana wananchi na tozo nyingi zisizo na msingi wala mantiki. Wimbi la Marathon miaka miwili baadae baada ya ndugu yangu hapa kutoa mawazo yake limeendelea kukua kwa kasi. Jicho litupiwe humu..........
 
Back
Top Bottom