Serikali ianzishe masomo maalum mashuleni ili kujenga mfumo ambao ni endelevu

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,697
3,263
wana JF. nimeona jitihada mbalimbali za serikali kutaka kurudisha taratibu na mifumo mbalimbali ambayo ilikuwa imepotea au kuharibiwa. mfano tabia ya usafi, uwajibikaji wa kulipa kodi kila eneo la biashara, maadili, utii wa sheria bila shuruti n.k
kwa hali ilivyo nchi yetu ilikwisha poteza uelekeo na kwa sababu asilimia kubwa ya wananchi walishaharibiwa na mifumo mbalimbali basi nashauri ili mifumo hii ihuishwe na kuwa endelevu sasa kwa manufaa ya nchi basi nashauri yaanzishwe masomo maalum kwa ajili hasa ya kulijenga taifa la kesho watoto wetu na wajukuu wetu. wakue wakijua taifa la kesho linatakiwa liwe la namna gani na hasa ukizingatia tunaelekea kwenye mifumo ya uchumi wa kati na mambo mengine meengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…