Hivi karibuni waziri mwenye zamana amesikika akitangaza paranja la watumishi wote wa uma kupeleka vyeti vyao vya kidato cha nne na sita katika baraza la mitihani la taifa NECTA kwa ajiri ya ukaguzi kitu ambacho kimefanya wataalam na wadau mbalimbali kutoka katika kila kona ya dunia kumwaga sifa zao zikiambatana na pungezi kwa waziri huyo, hongera za dhati kwako muheshimiwa waziri kwa kuligundua hili kwani jambo hili limekuepo kwa muda mrefu sana na kwa vipindi tofauti tofauti kufuatana na utawala husika.
Leo hii nipo hapa kwa ajiri ya kumpa ushauri wa dhati kabisa muheshimiwa waziri..,kua katika sakata hili la uhakiki ni vema akajua kua kuna makundi mawili tofauti.
kundi la kwanza ni la wale wenye vyeti feki vya kidato cha nne na sita na hawa ndio muheshimiwa waziri atakao wa pata kiurahisi kupitia balaza la mitihani la taifa NECTA na kwa sasa hawa sio wengi sana katika secta za uma kwani wengi wao wameshakimbia mara tu serikali ilipo anza kutanganza mchakato wa ukaguzi wa vyeti feki
Kundi la pili ambalo ndio bado lipo kwa 89% katika secta mbali mbali hasa likiitafuna secta ya afya kwa asilimia 40% kati ya watumishi wote wa secta ya afya ni lahawa watumishi ambao wao hua wana vyeti halisi vya kidato cha nne or cha sita isipokua wana vyeti feki vya taaluma,hii inasambishwa na watumishi wengi kufanya vibaya wanapo kua vyuoni na matokeo yake huishia kudisco kitu ambacho husababisha kugushi vyeti vyao vya taaluma "wao wanaita kudownload" na mwisho wa siku hutumia njia wanazo zijua wao na matokeo yake hujipatia ajira za serikali kundi hili ni hatari sana hasa katika secta ya afya maana wengi wao hawana taaluma ya kutosha matokeo yake huhatalisha maishi ya watu na kuighatim serikali kwakua tayari hawa hawana taalumu ya kazi husika..
labda nimpe mfano muheshimiwa waziri kua nilipo kua chuoni (medicine) kuna wanachuo zaidi ya 40% walidisco katika vipindi tofauti tofauti vya masomo lakini cha ajabu watu hao wapo makazini na wanafanya kazi haliyakua hawaku maliza masomo yao kutoka na kufeli kitu ambacho ni hatari sana kwa watanzania maana wanatibiwa na madactari wasio na sifa.
Mwisho mimi naona kundi la pili ni hatari zaidi kuliko kundi la kwanza maana hawa hawana sifa za taaluma husika afadhari ya kundi la kwanza maana hawa wamefoji vyeti vya kidato cha nne na sita halafu wameenda vyuoni kusomea taaluma husika na matokeo yake wamehitim mafuzo yao na kupewa vyeti vya taaluma, hivyo basi wanajua wachokifanya katika maeneo yao ya kazi...