Serikali haijui au imesahau umuhimu wa RUBADA

Danken Mbombo

JF-Expert Member
May 30, 2015
651
339
Rufiji Basin Development Authority (RUBADA) yaani Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la Mto Rufiji ni shirika la uma lililoundwa na serikali kwa sheria ya bunge ya waka 1975 kama sikosei.

Bonde la mto Rufiji linaazia mkoa wa Mbeya kupitia mikoa ya Iringa na Morogoro na kuishia mkoa wa Pwani. Hivyo basi mto Chimala, mto Ruaha, bwawa la Mtera, bwawa la Kidatu na mto Rufiji vipo katika ukanda wa bonde la mto Rufiji.

Lengo la serikali kuanzisha RUBADA ni kuhakikisha bonde la mto Rufiji linahifadhiwa na kuaendelea kuwepo bila kuharibiwa na shughuri zozote za kibinadamu.

Kazi za RUBADA ni kuendeleza na kudhibiti ndani ya bonde la mto Rufiji shughuri za kiuchumi kama: Kilimo,Uvuvi, Ufugaji, Uzalishaji umeme kwa kutumia nguvu za maji n.k

Waziri Januari Makamba ameunda kikosi kazi cha kunusuru kuharibika kwa bonde la mto Ruaha ambao ni moja ya maeneo yanayopitiwa na bonde la mto Rufiji. Timu iliyoundwa na waziri haijawashirikisha RUBADA.

Je? Serikali haijui au imesahau kazi na umuhimu wa RUBADA. Kama RUBADA ni shirika lililoundwa na serikali kufanya kazi ambazo sasa zimekabidhiwa kikosi kazi kilichoundwa na waziri Makamba, kwa nini serikali inaendelea kulipa mishahara kwa wafanyakazi wa RUBADA? Inawezekana zipo kazi nyingine pia zinazotakiwa kufanywa na RUBADA zimefaulishwa.

Serikali iingalie RUBADA kwa jicho la karibu, kama bado upo umuhimu wa kuendelea kuwepo. Kama hakuna tena umuhimu wa RUBADA basi ivunjwe mara moja ili serikali isiendelee kulipa gharama za uendeshaji wa shirika hilo pasipo faida yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…