Samia Suluhu: Wapinzani wako makini, CCM acheni kurusha vijembe!

Wabunge wa upinzani wanaoisaidia nchi ndiyo hawa wanaopinga kwa nguvu zote utumbuaji majipu?
Utafiti uliofanyika Uingereza ulionyesha Watz tunaongoza kwa kuwa wazito kuelewa.
Sasa kama wao ndio walionyesha ufisadi uko wapi na unawakera iweje wapinge kutumbua?
Hamuelewi kuwa wanachofanya ni kumsaidia Magu utumbuaji wake usiingie dosari kama issue zitapelekwa mahakamani. Huo ndio umakini aliosema Suluhu, lakini wa ccm wao ni makofi na bora liende
 
Vice President watch out your words remember what happened to Dr Omary Juma a decade ago. In Lumumba street there's no freedom of expression.
Hivi kifo cha jamaa kina mkono wa Wanaadam?
 
Tunataka Mbowe atusomee report ya mapato na matumizi wakati Wa kampeni.
Haiwezekani watu wazalendo kwa chama wanajitolea kuchangia chama alafu hatusomewi matumizi.!!!
Inaonyesha hela nyingi zilichangwa lkn cha ajabu mawakala Wa chadema hawajalipwa hela zao hadi Leo!!!
Hatuwezi kuhubiri mabadiliko huku matendo yetu ni mabovu afadhali ya ccm.!!!
Mbowe tunaomba report ya matumizi ya hela zetu.

kumbe sio bungeni tu hata humu ndani vilaza mmejazana
 
Nadhani huenda mama Samia Suluhu alijisahau akadhani yuko kwenye kikao cha siri cha ndani cha CCM, Kumbe kikao cha wazi, hivyo hakuna siri tena.

CCM wanajua kabisa, wabunge wa upinzani ni warevu na makini sana, ndio maana serikali inapiga marufuku hata bunge kuruka Live, maana wananchi huwa tunaona wenyewe mbichi na mbivu. Facts zinazungumzwa na wabunge wa upinzani zaidi, wakati wabunge wa CCM kazi yao ni ngonjera, Mipasho, kejeli tu.
 
Katika hali isiyotarajiwa makamu wa rais Samia Suluhu Hassan amekiri kwamba vyama vya upinzani vina wabunge makini wenye hoja za kuibana serikari. Amesema jinsi ya kupambana nao si kwa wabunge wa Ccm wa Ccm kurusha vijembe.

Katika mafunzo ya UWT kwa madiwani na wabunge yanayofanyika Dodoma Samia amekita Ccm kuandaa mafunzo maalum kwa wabunge wa wake kukabiliana na nguvu ya wabunge wa upinzani. Makamu huyo wa rais pia amekiri kwamba uchaguzi uliopita walikumbana na nguvu kubwa kutoka vyama vya Ukawa.

Chanzo: Mwananchi
Sio viongozi tu ni makini lakini hata anayeiunga mko chadema ni makini ana hoja,maswali,majibu na mifano ambayo hakika hata raisi hawezi kujibu wa kujitetea wakisimamishwa pamoja, vi vyema Magufuli akawatumia hawa ili kujenga Tanzania.
 
Utafiti uliofanyika Uingereza ulionyesha Watz tunaongoza kwa kuwa wazito kuelewa.
Sasa kama wao ndio walionyesha ufisadi uko wapi na unawakera iweje wapinge kutumbua?
Hamuelewi kuwa wanachofanya ni kumsaidia Magu utumbuaji wake usiingie dosari kama issue zitapelekwa mahakamani. Huo ndio umakini aliosema Suluhu, lakini wa ccm wao ni makofi na bora liende

Unapojibu kwa majivuno wapinzani ndiyo walionesha ufisadi iweje wapinge kuutumbua, UNAJIDANGANYA! Wasikilize viongozi wako wakiongozwa na Mbowe, kwa maana sisi tumewasikia na tumewaona wakipinga kwa nguvu zote utumbuaji majipu halafu kwa nini utumbuaji uingie dosari kama unavyodhania? Huoni baadhi wameshafikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua?
 
hahhahhahaha umenikumbusha lile tangazo la tigo la TUMEFIKA...joti anaulizwa umefikaje huko anasema nimejikuta tu npo huku........................
Taratibu watasema kila kitu na mwisho kabisa watasema jinsi walivyoiba kura
 
Kuna wabunge wanawapotosha wenzao...kuwa wapinzani wakitoa hoja nzito wewe toa Pumba ili kuidhoofisha ile hoja! Hawajui kuwa ndio wanajipoteza wenyewe! Sasa hata wakuu wao wameshaona wabunge wao hawajielewi!
Ndiyo maana hatuonyeshi bunge kwa sababu pale hatuna Mbunge hata mmoja anayeweza ku-raise na kuijadili hoja yake kisawasawa zaidi ya mipasho
 
Huyu naye watampora kiti chake maana wale wenzake hawapendi kauli za ukweli kama hii aliyoitoa
 
Fact samia. Mama kajaliwa diplomasia ya hali juu na ni mtu strategic sana kweny mmb yake na uongeaji sake..#RespectSamiaSuluhu
 
Tunataka Mbowe atusomee report ya mapato na matumizi wakati Wa kampeni.
Haiwezekani watu wazalendo kwa chama wanajitolea kuchangia chama alafu hatusomewi matumizi.!!!
Inaonyesha hela nyingi zilichangwa lkn cha ajabu mawakala Wa chadema hawajalipwa hela zao hadi Leo!!!
Hatuwezi kuhubiri mabadiliko huku matendo yetu ni mabovu afadhali ya ccm.!!!
Mbowe tunaomba report ya matumizi ya hela zetu.
Wewe nani hata kumuamrisha mbowe?
 
Hapo ndio u
Hebu naomba nieleweshwe!wabunge wa CCM wanaelekezwa wakapambane na upinzani au wakaisimamie serikali kwa niaba ya wananchi?
jiongeze ,ukiingia ndani ya wodi na kuona wagonjwa waliolazwa usijidanganye kuwa huyu kapona eti kwasababu anatabasamu au anamsaidia mwenzake jua wote ni wagonjwa ila yeye ana nafuu.ccm ni ile ile na inawenyewe.
 
Eti wanataka waitwe Waheshimiwa kwa mambo yepi wanayoyafanya zaidi ya kutukana ovyo Bungeni...
 
Heri wewe Simon Baryona, maana mwili na damu havikufunuliwa hili
 
Back
Top Bottom