SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA KWA WAZIRI WA AFYA UMMY MWALIMU

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
SALAAM ZA RAMBIRAMBI KUTOKA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
-----
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kwa huzuni na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watoto 32, walimu 2 na dereva mmoja wa shule ya Lucky Vicent ya Arusha, vilivyosababishwa na ajali ya gari iliyotokea katika eneo la Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu - Arusha.

Tunasikitika sana kwa kuwa ajali hii imetokea wakati wazazi, walezi na walimu wakitekeleza wajibu wao wa msingi wa kumpatia mtoto haki ya kuendelezwa Kielimu.

Kufuatia msiba huu mkubwa, kwa niaba ya Wizara na kwa niaba yangu mwenyewe ninatoa pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa wanaandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali. Tunamuomba
Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.

Tunaziombea roho za watoto wetu wapendwa zipumzishwe mahali pema peponi, Amina. Ni maombi yetu pia kuwa Majeruhi waliopo hospitalini watapata nafuu ili waweze kuendelea na masomo.

"Nendeni salama watoto wetu! Malaika wema watakuwa pamoja nanyi"!

Ummy Mwalimu, Mb
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
07/05/2017
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…