Safari ya South Africa ndio nimeanza

Mkuu ungekua unaenda Cape town ningekueleza chochote, but sio mwenyeji Sana kwa J'burg! By the way Mungu akutangulie, Una siku 4 mpaka 5 kufika J'burg! Kama Ni njia ya Lusaka!
 
Ndugu zanguni, wiki mbili zilizo pita nilileta uzi hum Jf lengo likiwa ni Kuomba /kuuliza namna ya kufika SA. Nilipata ushauri mwingi mno, mzuri, mbaya, wakunijenga, wakunikebehi Nk. Pamoja na hayo yote Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu mzuri.

Safari nimeianza jana nikitokea Babati mtaa wa Nyunguu, leo ndio nimeanza safari tena nikitokea Dar. Nauli nimetoa elf 45 mpaka Tunduma. Kiukweli moyoni nina hofu yenye mchanganyiko na furaha, Johannesburg sijawahi kufika, ila najua Mungu atafanya tu.

Ombi langu kwenu kila mmoja asiogope kutoka. Mi leo nimethubutu, nikifika tu JoBeg Ntawapa picha, huko nimejipanga kufanya kazi yoyote ambayo ni halali, hata km ni kuosha vyombo hotelni. Mbarikiwe sana
Nataka nikuulize utaepuka vipi vishawishi vya kuwa punda ukifika hapo Jozi ukakuta waya mkali? Wenzako wengi tu wameishia kufanya biashara hiyo
 
Kila la kheri kiongozi,mtangulize Mungu kwa Imani yako,fanyia kazi ushauri ulipoewa ila kikubwa usije ukashawishiwa kuingia kwenye biashara haramu yeyote utakuwa umepotea sana,ukishindwa plan zote karibu tena sweet Home Tanzania
 
Nataka nikuulize utaepuka vipi vishawishi vya kuwa punda ukifika hapo Jozi ukakuta waya mkali? Wenzako wengi tu wameishia kufanya biashara hiyo
Naomba nikujibu kaka, kila mtu anakuwa na vision zake, mimi nyumbani sijafukuzwa wala Mtaani, japo nilikuwa siishi na wazazi, nikiona hakuna chochote ninacho ona cha kufanya ntarudi Tz. Sio lazima eti kwakua wengi wanauza Hayo MA uchafu eti na mimi lazima niuze km wao, kwanza mimi nimeokoka, nina ujuzi wa kupiga mziki, ni It, nk nitaosha hata vyombo kwa mama Ntilie wa Ki-kabulu, haaaaaaaa ili mradi tu maisha yasonge.
 
Back
Top Bottom