Safari ya South Africa ndio nimeanza

Safari njema. Vikwazo vitakuwa vingi lakini mtegemee mungu na ufanye bidii katika kazi utayoipata. Usiendekeze uhuni na anasa.
Pongezi sana kwa uthubutu. Kama utasikiiza mawazo ya kukatisha tamaa kutoka kwa walishindwa utafeli sana. Sikiliza moyo wako unataka nini. UTASHINDA!
 
Yap karibu ndugu kumbuka tu kitu kimoja timiza kile kinacho paswa kutimizika fuata taratibu maana nchi uendayo haina malipo ya viza kwa watu wa nchi ya ukarimu kuingia ni bure tu karibu mwana kwenye kitu cha matumaini
 
Kaka, hii safari niliipangia takribani miaka 10, kimsingi nina jitambua, nikikosa kazi hata ya kufagia ntarudi tu Tz nauri ninayo, Lakini pia kwa asili yangu mimi (kigoma) hatuogopagi kazi. Ili mradi iwe kazi njema
Mungu akulinde, amagambo ni bukebuke.. Nenda salama wakwetu.
 
Ndugu zanguni, wiki mbili zilizo pita nilileta uzi hum Jf lengo likiwa ni Kuomba /kuuliza namna ya kufika SA. Nilipata ushauri mwingi mno, mzuri, mbaya, wakunijenga, wakunikebehi Nk. Pamoja na hayo yote Mungu awabariki sana kwa ushauri wenu mzuri.

Safari nimeianza jana nikitokea Babati mtaa wa Nyunguu, leo ndio nimeanza safari tena nikitokea Dar. Nauli nimetoa elf 45 mpaka Tunduma. Kiukweli moyoni nina hofu yenye mchanganyiko na furaha, Johannesburg sijawahi kufika, ila najua Mungu atafanya tu.

Ombi langu kwenu kila mmoja asiogope kutoka. Mi leo nimethubutu, nikifika tu JoBeg Ntawapa picha, huko nimejipanga kufanya kazi yoyote ambayo ni halali, hata km ni kuosha vyombo hotelni. Mbarikiwe sana
Mola akutangulie...ujali pia usalama wako..
 
Back
Top Bottom