Sababu zipi zilizokufanya uyachukie mapenzi?

Daah

Kiukweli nachukia hadi kupandwa na hasira kwakweli ..hadi sura inabadilika kutokana na nilichokipitia kwa mtu niliyejitoa kwake kwa hali na mali lakini yeye hata wazo kwake la kunipenda halikuwepo yaani nilitamani hata ninywe pombe lakini sijui kunywa nilitamani hata niwe naenda klabu lakini nilishindwa nilitamani niwe naenda kukaa bar lakini nafsi iliniambia hayo sio maisha yangui sistahili ili angalao nipate furaha…Moyo ulikuwa umefuraha mithili ya Simba aliyekosa kitoweo kwa wiki nzima..Niliona kama dunia imeniacha peke yangu…marafiki walinikimbia wakanicheka kuwa nimeshindwa kumweka mwanaume kwenye kiganja,,,sitakaa nisahau hii nitakuja kuhadithia hata wanangu Mungu akinijalia..Nililia kwakweli kazini niliomba likizo nikapumzike ..Dada yangu alikuwa faraja yangu kwa maneno yake..Yaani Engineer wa Kipare alinifanya niamini kuwa ukipendwa na mwanaume moyo wako ukimkubali anakupenda kweli kumbe ndivyo sivyo..nilikumbuka wanaume wote walionitongoza nikawakataa kwa sababu yake eti kuwa mwaminifu kwake….SITAKAA NISAHAU…Namshukuru nilikuwa simtegemei kifedha yaan..hapo ikabidi nijikubali tu nisahau nianze maisha mapya ya mimi kama mimi..

Aiisee, Pole sana. umeandika kwa hisia kali sana.
 
Uongo ndo unasababisha.
Watu wawe wakweli ili mtu awe huru kufanya maamuzi.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Bado Sana kuchukia mapenzi, haimaanishi sijawahi kuwa heart broken
 
Back
Top Bottom