BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,810
Kwa mujibu wa Afisa Elimu Mkoa, Samson Hango, Idadi hiyo ni kati ya Wanafunzi 300,000 waliopo Darasa la Kwanza hadi la 7 kutoka Shule za Msingi za Mkoa wote.
Takwimu hizo zilikusanywa Desemba 2022 kupitia Mpango wa Serikali wa 'Shule Bora' unaofadhiliwa na UK Aid kwenye mikoa 9 ya Tanzania Bara unaolenga kupunguza idadi ya Wanafunzi wanaomaliza Elimu ya Msingi bila kumudu Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Katibu Tawala Mkoa, Rashid Mchatta, amesema Mkoa huo umekuwa haifanyi vizuri Katika Elimu kwa ngazi zote kuanzia Awali, Msingi na Sekondari, huku akitaja sababu kuwa ni Mwamko Mdogo wa Wadau katika kuunga mkono Sekta ya Elimu".
===================
Zaidi ya wanafunzi 24,000 kati ya 300,000 wa darasa la kwanza mpaka la saba wa shule za msingi mkoani Rukwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
Ofisa Elimu Mkoa wa Rukwa, Samson Hango, alisema hayo wakati wa kikao kilichoandaliwa na Cambridge Education Tanzania kwa waandishi wa habari, maofisa habari wa halmashauri na viongozi wa radio za kijamii mkoani humo, kilichofanyika Namanyere wilayani Nkasi.
Alisema takwimu hizo zilikusanywa Desemba mwaka jana, kupitia mradi huo ambao ni mpango wa serikali unaofadhiliwa na UK Aid kwenye mikoa tisa Tanzania Bara ili kupunguza idadi ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi bila kumudu KKK.
"Tunaishukuru serikali kwa kuanzisha Mradi wa Shule Bora, natamani sana mradi huu pamoja na kutekeleza afua nyingine, hii ya kuwezesha wanafunzi kumudu KKK tuimalize, tumepewa maagizo na wizara ya TAMISEMI ya kuondoa tatizo hilo, tunapambana kulimaliza ili tuweze pia kupata tuzo za serikali," alisema Hango.
Katibu Tawala mkoa huo, Rashid Mchatta, alisema; "Kimsingi mkoa wetu bado haufanyi vizuri katika elimu kwa ngazi zote kuanzia elimu ya awali, msingi na sekondari, haki hii inachangiwa na mwamko mdogo katika kuunga mkono sekta ya elimu na sababu mbalimbali."
Mchatta alisema juhudi zinahitajika kwa vyombo vya habari vya umma na binafsi kuutangaza mradi ufahamike kwa jamii kwa kuwa umekuwa ni mkombozi mkubwa wa kuimarisha taaluma katika shule za msingi na kuinua elimu.
Mratibu wa Mradi kutoka Cambridge Education Tanzania, John Shindika, alisema wataalamu wa mradi huo na serikali walishirikiana, kupitia na kubaini afua 10 ambazo zilikubaliwa kutekelezwa kwa pamoja.
"Mradi umeiwezesha Ofisi ya Rais, TAMISEMI kuratibu mafunzo endelevu kazini kwa walimu yanayozingatia mwongozo wa mpango endelevu wa walimu kazini - MEWAKA, ambayo yatafanyika kwa awamu tatu katika Halmashauri za Nkasi na Sumbawanga Manispaa," alisema.
Shindika alifafanua mafunzo yatahusisha maofisa elimu kata 47, walimu wakuu 169, walimu wa taaluma 169, walimu mahiri waelimishaji rika 338 na maofisa udhibiti ubora wa shule (2), maofisa taaluma msingi (2) na katibu tume ya utumishi wa walimu (2).
Mradi huo unatekelezwa kwa miaka sita kuanzia Aprili 2021 hadi 2027 katika mikoa ya Tanga, Pwani, Mara, Simiyu, Singida, Dodoma Kigoma, Rukwa na Katavi kwa ushauri wa Kitaalum kutoka Cambridge Education ikishirikiana na Action for Disability and Development (ADD) International, International Rescue Committee na Plan International.
NIPASHE