Sijaelewa kidogo hapa WAKUU, kwa hiyo mtu natakiwa awe ana sticker ya fire pamoja na ya week ya kwenda kwa usalama? Au ukishapewa hiyo sticker ya fire inatosha? na zinapatikana wapi? mwenye maelezo ya uhakika msaada please!
ndugu yangu.....sticker ya fire uwe nayo....ya usalama mubarabara uwe nayo....road licence uwe nayo.....insurance uwe nayo....zebra cross uwe nayo....fuel pump iwepo sticker yake.....na ya mwisho mwendo kasi sticker.....
Wana JF,
Ni mara yangu ya kuingia hapa Jamvini, nabisha hodi.
Leo nikiwa njiani kwenda kazini kwangu nimesimamishwa na askari wa usalama barabarani mara nne, na wote walikuwa wanalikagua gari. Wa. Kwanza aliangalia tu bima na motor vehicle akaniruhusu kuondoka, wa alinisimamisha km 4 mbele. Akaniuliza kama gari ni zima, nikamjibu liko zima, akenda kuangalia bima na motor vehicle akaniruhusu. Wa tatu alinisimamisha baada ya. Km chache mbele, huyu akaniambia weka hazard, nikaweka akaenda nyuma ya gari, the akaja akasema weka reverse gia, nikaeka, akenda nyuma ya gari akaja akasema nipe kadi ya gari, nikampa, akasema lete lesenii, nikampa. Mwisho hasira ikaanza kunijia maana kila ninachompa harudishi. Akanimbia nipe kifaa cha kuzimia moto, ndipo nikamwambia nipe list ya vitu unavyovitaka nikupe badala ya kunichelewesha. Akasema mbona una kauli mbaya wewe. Nikamwuliza kauli mbaya anamaanisha nini. Mwishowe nilijikuta akiniuliza vitu vingi. Baada ya kuona amekosa kosa akaniambia una kosa la kuendesha gari na open shoes. Tukabishana akaniachia. Wakati narudi nyumbani nilikaguliwa tena.
Hoja yangu ni kuwa kwa nini hawa ndugu wasiwe na stika wakishakukagua wakuwee ili kuwaonyesha walio mbele kwamba umeshakaguliwa. Usumbufu ni mkubwa ndugu zangu. Na wanakutafuta makosa,
Nisaidieni
Pole sana hii ndiyo karaha ya nchi yetu, tena mara nyingine akikosa kosa anakupiga mzinga, unajua leo sijapata chai...ukiangalia hilo tumbo; mbaya zaidi hawa ni matajiri wana magari ya biashara, nyumba lakini ukishakuwa polisi wewe ni ombaomba maishani mwako hata kama ni tajiri lakini kama uko barabarani kazi ni kuomba tu. RTO wa Arusha ndiye polisi clean niliyewahi kukutana naye, una kosa mara moja faini na ukicheza unawekwa rumande haombi hata senti moja yako lakini huku mikoani ni matatizo
Hapa Arusha KUNA TRAFFIC ana daladala zaidi ya tano zinaenda Usa, zimeandikwa NDESSA, kuna dada Traffic anaitwa Anna anna NOAH zaidi ya nne zinaenda Namanga,,shangaa Mshahara wao ni Laki mbili kwa mwezi!