Ripoti ya CAG kwa mwaka ulioishia 30 Juni, 2017 imejaa madudu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema sheria mpya ya Madini haimpi ruhusa ya kufanya ukaguzi katika migodi. Aisihi Serikali ifanyie marekebisho.

Aidha, amesema mpaka sasa kuna vyama vya siasa 7 havikuwasilisha taarifa za mahesabu yao.

Pia, CAG amesema madeni ya matibabu nje ya nchi yamekuwa kubwa na yanatishia kusitishwa kwa huduma hiyo, hivyo ameishauri serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura..


===

YALIYOJIRI..

"Mapendekezo 201 ya mamlaka za serikali za mitaa yalitolewa na CAG katika ripoti zilizopita lakini ni 43 tu yaliotelekezwa.. Ofisi yangu inaona kuna utekelezaji duni wa mapendekezo yangu"- CAG Profesa Mussa Assad

"Tumetoa hati 527 mwaka 2016/17, hati chafu ziko 42... Kati yake 1 ya saba ni vya vyama vya siasa" CAG Profesa Mussa Assad

"Bado kuna tatizo kwenye mafuta yanayoingizwa nchini kwa kupewa msamaha wa kodi kwa ajili ya uchimbaji wa madini.. Hali hii inaikosesha serikali mabilioni ya shilingi" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna ongezeko la deni la matibabu ya ughaibuni la asilimia 60.2 kwa kipindi cha mwaka mmoja.. Serikali ilipe deni hili kwa hospitali za India" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna ongezeko la trilioni 5/- kwenye Deni la Taifa kutoka Juni 30,2016 hadi Juni 30,2017" CAG Profesa Mussa Assad

"Vyama tisa havikuwasilisha kabisa taarifa za hesabu zake kwa ajili ua ukaguzi" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna madeni ya watumishi, 4.6 ya madeni hayo hayakulipwa licha ya kuwa stahiki zao kutokana na kupandishwa daraja na sababu nyinginezo...Maoni ya ofisi yangu ni kwamba madeni yote yaingizwe katika bajeti ya mwaka mmoja na kulipwa yote" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna fedha zilikusanywa kwenye balozi za Tanzania ughaibuni lakini hazikufikishwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali kinyume cha taratibu" CAG Profesa Mussa Assad

"Serikali za mitaa hazikupeleka fedha za maendeleo kwa asilimia kubwa...Zaidi ya Sh. Bilioni 320 hazikupelekwa ikiwa ni zaidi ya nusu ya bajeti ya maendeleo ya serikali za mitaa" CAG Prosefa Mussa Assad

"Serikali ilikusanya fedha kwa asilimia 94.2, sasa inakuwaje bajeti haijatekelezwa? ..Wabunge wanapaswa kuhiji hili kwa sababu makusanyo yalipaswa kuakisi utekelezaji wa miradi' CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini kampuni za Bima hazijalipa MNH Sh. Bilioni 1.4" CAG Profesa Mussa Assad

"Sheria mpya ya madini haimpi mamlaka CAG kuingia na kufanya ukaguzi wa migodi. Tunaona kuna udhaifu wa kisheria hapo" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumefanya ukaguzi maalum baada ya kuombwa kwenye Chama cha walimu na kubaini kuna malipo ya mabilioni ya shilingi yamefanyika kinyume cha taratibu" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini @NIDA_Tanzania kuna ubadhilifu kwa kughushi ukubwa wa eneo lililokodishwa...Mamlaka vilevile ilikuwa inatumia viwango vya kubadilisha fedha kwa hesabu za benki za biashara badala ya BoT" CAG Profesa Mussa Assad

"Ukaguzi wetu TBC ulibaini vifaa vilivyoingizwa na StarTimes kwa msamaha wa kodi havikufungwa mahali popote nchini.. Huenda vimepelekwa mahali pengine ndani ya nchi au nje ya nchi" CAG Profesa Mussa Assad

"Udhaifu mwingine ni StarTimes kupata hasara kwa miaka yote na haikuchagia gaharama za ushirikiano wa mtaji unaofikia Dola 600,000" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna usimamizi duni katika uwekezaji wa alama za barabarani" CAG Profesa Mussa Assad

"Majengo mengi ya umma si salama kutokana na kutokuwa na vifaa vya uokoaji likiwamo jengo hili la Bunge" CAG Profesa Mussa Assad

"Kuna udhaifu katika kutathimini maeneo ya miradi kabla ya kutekelezwa kwa miradi husika..Mfano, kituo cha mabasi ya mwendokasi Dar kinafurika maji wakati wa masika" CAG Profesa Mussa Assad

"Tumebaini kuna udhaifu katika utekelezaji wa taka za kielekroniki nchini.. Hakuna mkakati wala bajeti ya udhibiti wa taka hizo nchini" CAG Profesa Mussa Assad

"Kazi ya CAG ina lawama. Tutazipitia taarifa zote na kutoa taarifa kwa Bunge zima.. CAG ametaja kila sehemu upotevu wa fedha. PAC tumejipanga kuhakikisha halitaachwa jiwe.Kipindi hiki tutatoa mapendekezo mazito zaidi" Mwenyekiti wa PAC Naghenjwa Kaboyoka

Mh. Abdallah Mtolea (Kwa niaba ya Mwenyekiti wa LAAC)

"Tutaanza kuziita Halmashauri mara moja zikiwamo zile zilizomficha CAG vitabu vya risiti"

"Kamati ya Bajeti ya Bunge ijibu au ihoji kwanini fedha zimekusanywa lakini hazionekani zilikokwenda" CAG Profesa Mussa Assad

"Vyama ambavyo havikuwasilisha hesabu zake kwa CAG ni pamoja na ACT-Wazalendo, CUF, Tadea, NCCR na UPDP" CAG Profesa Mussa Assad

=====

Wakati Rais John Magufuli akipambana dhidi ya ufisadi, uzembe na ukwepaji kodi na uovu mwingine dhidi ya mali za umma, ripoti mpya ya ukaguzi iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inaonyesha ana kazi kubwa zaidi kupata ushindi kwenye vita hiyo.

Ripoti hiyo ya mwaka 2014/ 2015 iliyowasilishwa bungeni jana na CAG Mussa Juma Assad imeibua uozo zaidi kwenye halmashauri, taasisi za Serikali na mashirika ya umma, ikibainisha kuwa nchi ina tatizo kubwa zaidi ya watu ambao wamekuwa wakishughulikiwa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Ripoti hiyo ya pili ya Professa Assad tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo mwaka juzi, imegusa taasisi zilizowahi kuwa chini ya Rais John Magufuli na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako na Balozi Asha Rose Migiro, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria na Katiba.

Ripoti hiyo pia inaonyesha ufisadi katika ununuzi na uingiaji mikataba uliofanywa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), matumizi yasiyo ya lazima kwenye Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jeshi la Wananchi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na mkoa wa Tabora.

Pia ripoti hiyo imebainisha kuwa mapendekezo mengi ambayo CAG amekuwa akiyatoa kwa takribani miaka saba sasa, hayatekelezwi.

Katika ripoti hiyo, CAG anaonyesha dosari kwenye utendaji wa Wakala wa Huduma za Ufundi na Umeme (Temesa), na Wakala wa Barabara (Tanroads), taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi ambayo wakati huo ilikuwa ikioongozwa na Dk Magufuli.

Profesa Ndalichako alikuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), wakati NEC imeguswa na ripoti hiyo katika suala la mchakato wa kuandika Katiba upya ulioongozwa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Ripoti hiyo ya Profesa Assad pia imebainisha kuwa Deni la Taifa, ambalo hutokana na fedha zinazopowa kutoka ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kugharimia matumizi ya Serikali, limekuwa kwa tofauti ya Sh7 trilioni.

Tangu aingie madarakani Novemba 5 mwaka jana, Dk Magufuli amekuwa akitumia ripoti zilizopita za CAG kusimamisha kazi au kutengua uteuzi wa watumishi wa umma wanaotuhumiwa kujihusisha na ufisadi, lakini amekuwa akikosolewa kuwa hajaweka mfumo wa kukabiliana na hali hiyo.

Katika ripoti hiyo, CAG anasema Temesa ilinunua kivuko chenye kasi ndogo kuliko ilivyotarajiwa na hadi ulipokuwa unafanyika ukaguzi Agosti 2015, chombo hicho kilikuwa hakifanyi kazi kwa zaidi ya mwaka.

“Kuhusu dosari katika ununuzi wa kivuko chenye thamani ya Sh7,916,955,000, Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Umeme, mitambo na ufundi (Temesa) iliingia mkatabana M/s Johs.Gram-Hanssen Bergensgade 10, DK 2100 Copenhagen Oe Denmark wa ununuzi wa kivuko cha Dar es Salaam –Bagamoyo chenye thamani ya Dola za Marekani 4,980,000 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),” anasema CAG.

“Dosari zifuatazo zilibainika katika manunuzi hayo. Kasi ya kivuko haikuzingatia matakwa ya mnunuzi. Ripoti ya mtaalamu wa ukaguzi ilibainisha kwamba kiwango cha juu na chini cha kasi ya kivuko wakati wa majaribio kilikuwa na kiwango kati ya knots 19.45 na knots 17.25 kinyume na makubaliano yaliyoainishwa kwenye mkataba wa kasi ya kiwango cha 20,” anafafanua.

“Pili kivuko kilikabidhiwa bila hati ya makabidhiano Novemba 17, 2014 baada ya ucheleweshwaji wa siku 16; Pia nilibaini kwamba mpaka wakati wa ukaguzi, Agosti 2015, hati ya makabidhiano ilikuwa haijatolewa na mzabuni.”

Ununuzi wa feri hiyo uliwahi kuzua sakata bungeni huku wabunge wa upinzani wakilalamika kwamba kilikuwa bomu kwani kinatumia zaidi ya saa tatu kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo badala ya dakika 45 za gari.

Eneo jingine lililoguswa na CAG ni la malipo yaliyofanywa na Tanroads kwa makandarasi waliomaliza kazi zao. Kwamba moja ya matatizo makubwa ya taasisi hiyo ni udhaifu katika menejimenti.

“Wakala wa Barabara (Tanroads) iliingia mikataba mbalimbali ya ujenzi wa barabara na madaraja. Wakati wa ukaguzi nilibaini kwamba baadhi ya mikataba haikukamilika kwa muda uliopangwa kutokana na kuchelewa kwa ulipaji wa fedha. Pia, nilibaini kwamba ucheleweshwajiwa malipo ya kati ya mikataba 16 ulisababisha ulipaji wa riba kiasi cha Sh 5,616,652,022 na Dola za Marekani 686,174.86,” alisisitiza CAG.

Profesa Assad amezungumzia pia ukaguzi maalumu alioufanya kuhakiki fedha zilizowahi kutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa taasisi mbalimbali zilizoko chini yake.

Ukaguzi huo ulifanywa kutokana na ombi lililowasilishwa na katibu wa Bunge kwa barua yenye Kumb. NaCBC.155/188/01/26 ya Desemba 19, 2013. Bunge lilitaka kujua kama fedha zilizotolewa na wizara hiyo kwenda idara na taasisi zilizo chini yake zilipokewa na kutumiwa na wahusika kama ilivyopangwa.

Katika ukaguzi huo, CAG alibaini kasoro katika vitabu vya akaunti za fedha vya Necta mwaka 2010, Sekretarieti ya Elimu ya Jumuiya ya Madola, Chuo Kikuu Huria (OUT), na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Adem).

“Udanganyifu wa malipo ya Sh185,350,000 yaliyolipwa Necta. Aprili 2010 kiasi cha 185,350,000 kilitumwa Necta kama matumizi ya kawaida. Wakati wa ukaguzi ilibainika kuwa kiasi hiki cha fedha hakikuandikwa kwenye vitabu vya uhasibu vya Necta. Hata hivyo, ilibainika kuwa stakabadhi ya mapokezi ya fedha hizo iliyotolewa na watumishi wasio waaminifu wa Necta ilikuwa ya kugushi,” anasema.

“Kuhusu fedha zilizopelekwa OUT ni kwamba kati ya mwaka 2009/2010 Wizara ilihamisha Sh90,000,000 kwenda Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, ni kiasi cha Sh40,734,000 ambacho kilipokewa huku Sh49,266,000 hakijulikani.

“Pia katika mwaka wa fedha 2010/2011 Wizara ilipeleka OUT Sh10,486,252,913 lakini ni Sh10,427,109,020 tu zinazoonekana kwenye vitabu huku Sh59,143,893 zikiwa hazimo kwenye vitabu.”

Vilevile, CAG amesema katika ukaguzi huo Sh188, 838,528 zilizopelekwa Adem mwaka 2009/2010 zimeyeyuka. Mwaka huo Wizara ilipeleka Sh712,798,788 kwa taasisi hiyo, lakini vitabu vinaonyesha Sh523,960,260 zilipokewa na kurekodiwa, huku Sh188, 838,528 zikikosekana kwenye vitabu.

Mbali ya CAG kuonyesha madudu katika matumizi ya fedha, pia ameonyesha matumizi mabaya ya Sh7,080 milioni katika mchakato wa uchapaji Katiba Inayopendekezwa.

“Katika ukaguzi wangu nilibaini kuwa Wizara ya Katiba na Sheria ilipokea fedha kiasi cha Sh7,125 milioni kwa ajili ya kulipia gharama za kuchapisha vitabu vya Katiba Inayopendekezwa. Kutokana na ufinyu wa muda, Wizara iliomba na kupewa kibali na Wakala wa Huduma za Manunuzi Serikalini kufanya manunuzi kwa njia ya dharura kupitia barua yenye kumbukumbu Na CAD.124/318/01/25 ya Desemba 11, 2014,” anasema CAG.

“Katika ukaguzi wangu nilibaini vitabu vya katiba vilipokelewa kabla ya kuingia mkataba. Nilibaini kuwa mkataba ulisainiwa Februari 2, 2015, lakini vitabu vya katiba vilipokelewa Januari 26, 2015.”

Ukaguzi uliofanywa Oktoba Mosi, 2015 umebaini kuwa nakala 158,003 za Katiba Inayopendekezwa zenye thamani ya Sh559,330,620 bado viko stoo au havijatumwa kwa wananchi ili vitumike kwa uhamasishaji.

“Kwa hiyo, haikuwa rahisi kujua kama thamani halisi ya fedha ilipatikana na lini vitabu hivi vitasambazwa kwa walengwa. Pia, ilibainika kuwa vitabu hivyo havikujumuishwa kwenye Taarifa za Fedha za Mwaka husika,” anasema.

Katika ripoti hiyo ya mwaka 2015/16, CAG Assad anasema ukaguzi wake umebaini matumizi ya mabilioni ya fedha katika ununuzi wa vitu visivyokuwa vya lazima au bila kuonyesha ushahidi wa malipo husika.

Alibainisha matumizi ya zaidi ya Sh53 bilioni zilizotumiwa na taasisi sita pamoja na Sekretarieti mbili za mikoa katika mambo ambayo hayakuwa ya lazima, kama faini za kuchelewa kulipa kodi ya pango.

Taasisi hizo ni Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Afya, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na Mkoa wa Tabora.

CAG Assad amebainisha matumizi ya ziada ya Sh109,722, 539 kwa ajili ya ununuzi wa gari aina ya Toyota Land Cruiser VX V8 kwa Sh297.5 milioni kutoka kampuni ya Toyota (T) badala ya kutumia mfumo wa ununuzi wa pamoja ambao ungefanya gari hilo lipatikane kwa Sh187.8 milioni.

Alisema katika kipindi hicho, wizara 17, balozi mbili na sekretarieti za mikoa 11 zilitumia zaidi ya Sh11.3 bilioni bila kuwapo vielelezo vyovyote, hivyo kusababisha ashindwe kujua uhalali wa malipo hayo.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa Magufuli ana kazi nzito ya kuiweka nchi “kwenye mstari”.

Maoni ya wadau

“Anachofanya Rais Magufuli kwa sasa ndicho kitu sahihi kinachotakiwa kufanya,” alisema Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu (Duce) alipoongea na Mwananchi jana baada ya ripoti hiyo ya CAG kutoka.

“Ingawa ni ukweli usiopingika kuwa uozo huo unasababishwa na mfumo, lakini anachofanya sasa ndiyo hasa kilipaswa kufanywa kwa muda mrefu kwa kuwa mfumo huo umewekwa na watu.

“Hata hivyo, ili Rais afanikiwe katika mikakati yake, hana budi hatua anazochukua zifuate mifumo ya sheria badala ya utashi wa kisiasa.”

Profesa Kitilya, ambaye ni pia ni mwanachama wa ACT- Wazalendo, alisema CAG amekuwa akitoa ripoti, lakini uozo unazidi kwa kuwa awali hapakuwa na kiongozi aliyekuwa ana utashi kama alionao Rais Magufuli.

Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Tija la Taifa (NIP), Profesa Samuel Wangwe alisema sababu kubwa ya kuendelea kwa vitendo vya kifisadi nchini licha ya ripoti ya CAG kumulika taa ni kutokuwepo kwa mfumo madhubuti wa kusimiamia utendaji kazi wa kila mmoja.

Kwa mujibu wa Profesa Wangwe, ambaye awali alishawahi kuwa mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Utafiti na Kupunguza Umaskini (Repoa), sehemu kubwa ya mabadiliko hayo inawezwa kufanywa na Rais na watu wake kwani yeye mwenyewe akiamua hakuna kitakachoshindikana.

“Ni lazima kuweka utaratibu wa ufuatialiaji,” alisema Profesa Wangwe.

“Rais akiamua kuweka mfumo madhubuti wa kuwawajibisha wote wanaopatikana na hatia katika kuhujumu mali za umma, haya yote yatapungua.”

Hata hivyo, Profesa Wangwe alisema Katiba mpya itasaidia kubadili mfumo mzima ulioota mizizi.

Chanzo: Mtanzania

Ripoti kamili ya Ukaguzi imeambatanishwa kwenye faili hapo chini (PDF) au Bonyeza HAPA

Ripoti ya Serikali kuu soma HAPA
 

Attachments

  • press-release-2018-_2.pdf
    889.1 KB · Views: 117
  • RIPOTI-KUU-YA-SERIKALI-KUU.pdf
    6.1 MB · Views: 268
ameishauri serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura..


Tulipe deni ili kuepuka tatizo ikitokea dharura, dharura ya nani, Spika Ndugai akizidiwa akumbizwe India?

Kwa nini Watanzania tunakubali kutoa kodi zetu zikatibu watu nje ya nchi watu ambao wana mishahara na mavumba makubwa kuliko sisi raia ? Kwa nini mtu unathamini maisha ya kiongozi kuliko ya kwako?

Asituzingue huyu CAG na aache undumilakuwili, juzi kasema deni linastahimilika.

MKE wa Magufuli anatibiwa Muhimbili, huyu CAG anataka zilipwe hela za kwenda kuwatibu wao kina CAG India, Mzee Magu mtumbue huyu mtu fasta!
 
Jamaa wanachota tu! Si huyu jiwe aliudanganya umma kwamba matibabu ya nje yamesitishwa? Kumbe ulikuwa uongo mwingine!

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema sheria mpya ya Madini haimpi ruhusa ya kufanya ukaguzi katika migodi. Aisihi Serikali ifanyie marekebisho.

Aidha, amesema mpaka sasa kuna vyama vya siasa 7 havikuwasilisha taarifa za mahesabu yao.

Pia, CAG amesema madeni ya matibabu nje ya nchi yamekuwa kubwa na yanatishia kusitishwa kwa huduma hiyo, hivyo ameishauri serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura..
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Prof. Mussa Assad amesema sheria mpya ya Madini haimpi ruhusa ya kufanya ukaguzi katika migodi. Aisihi Serikali ifanyie marekebisho.

Aidha, amesema mpaka sasa kuna vyama vya siasa 7 havikuwasilisha taarifa za mahesabu yao.

Pia, CAG amesema madeni ya matibabu nje ya nchi yamekuwa kubwa na yanatishia kusitishwa kwa huduma hiyo, hivyo ameishauri serikali kulipa haraka madeni hayo ili kuepuka matatizo ikitokea dharura..
kesho ataambiwa akunushe
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Asaad amesema kwamba ''Kama tulivyotoa taarifa zetu hivi karibuni, bado tunasisitiza deni la taifa ni himilivu, ila lazima tuwe makini kwenye ukopaji wetu"
 
Sasa wakiendelea kwenda unadhani wanalipa cash? Si wanaongeza hilo deni? Na hiyo kauli ya kuzuia matibabu ya nje jiwe alisema pia.

Unaelewa maana ya neno Madeni? Linaweza kuwa la leo au la miaka 20 uliyopita
 
Ni kweli kabisa ndo maana mpaka walishindwa kutoa gharama za matibabu kwa Mbunge wa Singida Tundu Lissu lakini huku Spika anaenda India kila wiki kwenye vipimo
 
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Juma Asaad amesema kwamba ''Kama tulivyotoa taarifa zetu hivi karibuni, bado tunasisitiza deni la taifa ni himilivu, ila lazima tuwe makini kwenye ukopaji wetu"
Huyu sasa anahitaji kupigwa vijembe na pogba, shauri yake
 
Hivi bajeti ya kununua wapinzani CAG huwa anaikagua kama imetumika kiusahihi? Maana. Naona miaka hii miwili kama tume overspend hivi!!
 
Back
Top Bottom