MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Kila kukicha Paul Makonda anazidi kuimarika zaidi huku maamuzi ya Jukwaa la wahariri nchini Tanzania na pia umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania yakizidi kudhoofika.
Wataalam wa crisis management wanabainisha ili kuwepo na mafanikio katika utatuzi wa tatizo/matatizo kunahitaji uwepo wa taarifa sahihi, mpangilio sahihi, maamuzi sahihi na wakati mwingine uwepo kile kinaitwa, ‘’ ngekewa/kismati’’.
Kitu kingine muhimu sana kinachochagiza maamuzi kuwa sahihi ni uwezo wa mtoa maamuzi katika kupambana na shinikizo la ndani au nje ili kutoathiri utoaji wa maamuzi sahihi.
Utaratibu mzuri wa kuchukua maamuzi sahihi mara nyingi huingiliwa pia na uwezo kifikra, kuukataa ukweli, uchanganuzi wa mantiki, maamuzi jumla(overgeneralization) na fikra hisia(emotional reasoning).
Kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye ili kuchunguza kuhusu tukio lililofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam haikufanya maamuzi sahihi kwa sababu sio kwamba hawakuwa na uwezo kifikra bali waliongozwa na fikra hisia na kuukataa ukweli wa mazingira ya tukio kwa sababu ya shinikizo. Kwa mantiki hiyo, hata maamuzi yao yakakosa mpangilio sahihi katika utoaji hukumu.
Wataalam wa Coercive diplomacy wanabainisha kuwa ili kikwazo/vikwazo vifanikiwe inatakiwa kwanza litolewe onyo kali linalobeba ukweli na uwezo wa kutekelezeka ambao mpatiwa onyo akitafakari lazima atafikia maamuzi ya kufanya lolote linalowezekana ili asikumbwe na kikwazo/vikwazo.
Ukosefu wa mpangilio sahihi uliofanywa na kamati ya Nape Nnauye ulipelekea hata Jukwaa la wahariri nchini Tanzania na pia umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania kutoa hukumu ambayo haitekelezeki kwa muda mrefu hasa kwa sababu haikuwa na mapitio ya muda mfupi na mrefu. Hukumu waliyotoa ilikuwa haimfanyi Paul Makonda apate kikwazo kinachopelekea kushindwa kufanya kazi kama Mkuu wa Mkoa na hatimaye kupoteza kazi yake.
Kumfungia kutotangaza habari zake ilikuwa ni kumsaidia badala ya kumwangamiza kwa sababu alipata fursa ya kuondoka kwenye heading hasi za vyombo vya habari na kwa mantiki hiyo hata shinikizo la kutaka afukuzwe kazi likapungua.
Kwa sasa vyombo mbali mbali vya habari vimeanza kuipuuza hukumu. Kupuuzwa kwa hukumu kunamfanya by default Paul Makonda aimarike zaidi kisiasa na kijamii.
Walianza TBC na vyombo vyake (TBC1, TBC FM, TBC TAIFA) wakafuata Star TV , Radio Free Africa (RFA), E-FM Radio, Times FM, Magic FM na sasa kituo cha Channel 10 achilia mbali Televisions za kwenye mitandao kupitia YouTube and still counting...
Kelele za kutaka afukuzwe kazi au ajiuzulu zimeanza kufifia kwa haraka. Hata jina ‘’Daudi Albert Bashite’’ limeanza kupotea taratibu.
Tukio la Paul Makonda na CLOUDS MEDIA linanikumbusha maneno ya Mwl. Nyerere wakati akiongea na Press Club mwaka 1995. Jambo moja aliloligusia ni rushwa ambapo alisema ‘’serikali corrupt inatumwa na wenye mali, inawafanyika kazi wenye mali, serikali corrupt imwambiaje mwenye mali? Kwamba utalipa kodi na usipolita utakiona? Mwenye mali atacheka tu na kusema unaniambia hivyo wewe? Kesho siji basi’’.
Kwa kutumia mantiki ya Mwl. Nyerere, CLOUDS MEDIA ni ‘’corrupt institution’’ huku Paul Makonda akiwa ‘’tajiri wao’’ ambaye alikuwa anawatuma wamfanyie kazi zake kiasi kwamba alikuwa anaingia sehemu yoyote ndani ya studio za CLOUDS na kutoka kama anavyopenda. CLOUDS walifikia hatua ya kumpa meza na akaweka komputa ndani ya studio ili imsaidie katika kazi zake. Hii ni sifa ya corrupt institution and influential person.
Hata walipomtaka Paul Makonda awaombe msamaha, alicheka tu na kuwaambia unaniambia mimi nikuombe msamaha? Sikuombi na kuanzia sasa siji basi kwenye studio zako!
Siwezi kushangaa pale nitawaona CLOUDS MEDIA wanaanza tena kujipendekeza/kujikomba kwa ‘’tajiri wao’’ Paul Makonda ili mambo yao yawanyokee!
Hawa wamefikia wapi na mbio zao za kumpeleka mahakamani?
LINK>>Tanganyika Law Society(TLS) kumburuza Mahakamani RC Makonda
LINK>>Meya wa Ubungo kufungua kesi ya jinai dhidi ya Paul Makonda
LINK>>Mbowe afungua Kesi Mahakama Kuu dhidi ya RC Makonda, RPC Sirro na ZCO Wambura
Ama kweli hawakukosea waliosema, ‘’ if you can't beat them, join them’’.