Rapper John Woka apata ajali ya kulipukiwa na gesi, yupo ICU Muhimbili

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Rapper anayejulikana kwa kurap kama mlevi, John Woka, amepata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Walikuwa wanahangaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.


Chanzo: Bongo 5
 
Get well soon. Wizara yao ya Wasanii imsaidie msanii huyu kw kuhakikisha anapata huduma stahiki
 
Pole sana John Walker,poleni sana ndugu,jamaa na marafiki maombi yangu kwa Mungu ni uponyaji.Tukilihifadhi neno la Mungu lenye nguvu ya uponyaji ndani ya mioyo tunajua hakika kwamba "...kwakupigwa kwake(Yesu Kristo) sisi tumepona" Isaya 53:5 Tuwe na tumaini
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…