Rais wa zamani wa Marekani John F. Kennedy akimkaribisha Mwalimu Nyerere Marekani, 1963

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487


Rais wa 35 wa Marekani, John F. Kennedy (JFK) akimkaribisha Mwalimu Nyerere Marekani, Julai 1963. Bonyeza chini kusikiliza. JFK aliuawa kwa kupigwa risasi huko Texas Marekani mwaka huo huo wa 1963, Novemba 22.
 
Nani alimbadilisha Mwalimu kiitikadi?! Ukimfuatilia Mwalimu kwa umakini utagundua ni kama mwanzoni alikuwa na mtazamo wa Kimagharibi-- namaanisha ubepari hadi mwaka 1968 alipoupa kisogo rasmi mfumo huo!

Maasi ya 1964 yanatoa uwezekano mwingine wa kwamba, baada ya uhuru, Mwalimu hakuwa mjamaa! Kama ilivyo ada kwamba unapokumbwa na janga utaomba msaada kwa yule unayeamini atakusaidia; baada ya Maasi ya 1964 Mwalimu aliomba msaada toka kwa bepari Uingereza!!

Unclassified CIA Files ambazo zilifichua siri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar nazo zinatoa uwezekano mwingine wa kwamba huenda, back then, Mwalimu alikuwa na mtazamo wa Kipebari!

If so, who "converted" him?! Can it be Abdulrahman Babu ambae hata kabla Zanzibar haijamtimua Sultan yeye na wenzake walishakuwa ma-communists yaliyokubuhu yaliyomtisha hata Karume? Ikumbukwe kwamba, struggles za Abdulrahman Babu zilikuwa na back up ya kutosha kutoka nchi za kikomumisti hususani China! Hata kabla ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari Babu alishakuwa amepeleka vijana wake Cuba kuchukuwa mafunzo ya Kijeshi kutoka Communist Cuba ili hatimae waje kumtoa Sultan!

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, Abdulrahman Babu alikuwa ndo Foreign Minister baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kabla ya kupata hicho cheo tayari alikuwa na connection kubwa na China pengine kuliko connection ambazo Mwalimu alikuwa nazo! Kwavile bado naamini Mwalimu hakuwa Mjamaa alipoingia Ikulu kwa mara ya kwanza; si kwamba ni huyu Babu ndie alimbadilisha? Don't forget, Babu nae wakati huo alikuwa ni msomi kama Mwalimu!

Na ikiwa hisia zangu (he wasn't a socialist from day one) ni sahihi na endapo asingekuwa TOTALLY "converted" lakini badala yake angeamua ku-practice mixed economy; am telling you, Mwalimu angeiacha Tanzania mbali sana kiuchumi. Ubepari unahitaji big brain na Mwalimu alikuwa nayo.

RIP Mwalimu.
 
Mmeanza tena
 
Moja Kati ya Watawala Waliowahi kutokea na Historia zao zikaandikwa na Wala haitafuka Kamwe

Alikuwa mzalendo wa kweli mwenye maono na hili linadhihilika silu hizi kwa hawa wa leo wanapopata matatizo kufanya hadidu za rejea kwenye hotuba zake alizotoa enzi ya uhai wake!!
 
miaka ya 1963 picha zilikuwa black and white sijui hii umeipataje au mambo ya technology
 
Alikuwa mzalendo wa kweli mwenye maono na hili linadhihilika silu hizi kwa hawa wa leo wanapopata matatizo kufanya hadidu za rejea kwenye hotuba zake alizotoa enzi ya uhai wake!!
Mkuu kuna msemo usemao zilongwa mbali zitendwa mbali...
 
Mkuu kuna msemo usemao zilongwa mbali zitendwa mbali

Huu msemo unawahusu hawa wa leo kama vile yule mkweree wa Msoga aliyetuongopea na misemo ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA kumbe hakuna lolote bali wizi tu!! Kambarage used to walk his talk!
 
alibadilishwa na MTU mmoja anaitwa Rwizandekwe ambaye historia inaonyesha kwamba ndo muasisi wa azimio LA arusha, Huyo mzee alikutana na mwalimu masomoni huko UK, kabla uhuru, baadaye alikuja kuwa waziri wa sheria, baadaye alitofautiana na mwalimu akaachana siasa, anaishi bukoba mkoani kagera,
 
OMG! Thanks man! Hilo jina ndo mara yangu ya kwanza kulisikia! Thanks God, nime-Google na kukutana na huyo mtu... wacha nipitie mawili matatu kumuhusu yeye ili nijiongezee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…