MUSHEKY
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 2,812
- 2,761
Kwanza nianze kukubaliana na walio wengi kuhusu kupanda kwa gharama za maisha kupita kiasi kutokana na sababu mbali mbali hasa zile za kiulimwengi hususani tokea mlipuko wa corona na sasa vita vya Russia na Ukraine
Ikumbukwe pia baada tu ya kutangazwa bei mpya za mafuta bei za vitu pamoja na nauli za mabasi ziliongezeka ghafla na mzigo huu mzito wananchi tukaubeba kwa kua sisi ndio "wanyamwezi"
Lengo la kuandika haya ni hujuma wanazofanya watendaji wa kituo hiki cha mabasi hususani wale wanaokaa mlangoni kukusanya mapato wanapomlipisha abiria kwa mara ya pili pindi anapoingia getini kupanda gari hata kama amekata risiti ya basi anayo mkononi
Ikumbukwe utaratibu wa awali ilikua kwa abiria mwenye tiketi mkononi anaingia kwa kutumia tiketi yake kwa kua dhahili inafahamika anachokwenda kukifanya ni safari kwa mujibu wa tiketi yake ambalo ndio lengo kuu la kituo chenyewe "kusafirisha abiria''
Aidha kumlipisha abiria mlangoni hata kama kashika tiketi ya basi "yenye machungu ya nauli iliyopanda" ni kumkosanisha mheshimiwa rais na wapigakura wake kwa kua ukiachilia mbali kupanda kwa gharama za maisha kiasili, zipo pia sababu za kiuzembe kama hizi ambazo naamini mamlaka za juu hazijabariki unyonyaji huu zaidi ya kua ni utashi wa kifisadi wa baadhi ya watendaji huku wakiamini hawatafanywa lolote
Kilichonishangaza baada ya kuwakomalia kwa nini nilipe wakati nina tiketi ya gari mkononi eti wananiambia kwa sababu hiyo tiketi ya gari sio za kielectroniki!! Sasa hilo ni kosa langu?
Na je kama sio za kielekteoniki leo miaka yote ya nyuma zilikua za kielektroniki?
Naamini mheshmiwa rais utatupia jicho kwenye kituo hiki kikubwa cha mabasi na kuuondoa mzigo huu mpya ambao wananchi wako tumebebeshwa tena
Ahsanteni