Rais Samia naskia upo JamiiForums, basi pitia hapa

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,431
12,292
Mama ili Nchi iendelee inatakiwa watu walipe kodi ila lazima uangalie namna unavyowakamua wananchi wako namna unavyowaumiza na sio kuwadai kodi kwa mabavu

Mama mtu anaagiza mzigo China ukifika Bandarini analimwa kodi kubwa alatu mtu huyo huyo akifikisha mzigo wake store bado mnataka alipe kodi nyingine, mtu huyo huyo akiuza huo mzigo mnataka tena alipe kodi nyingine na anaenunua huo mzigo akifikisha dukani kwake nae anatakiwa atoe risiti tena.

Hapo hapo mauziano ya hizo mali zote ni lazima kuwe na miamala ya kipesa kutokea Bank au mitandao ya simu na huko mama umeweka Tozo juu, yaani manunuzi ya mali 1 yana kodi 10 kidogo kwa mwendo huu ni lazima wafanyabiashara watakwepa kulipa kodi sababu sio Rafiki kwao.

Mtu anaagiza Gari Japan kwa milioni 10 likifika bandarini kodi ni kama pesa aliyonunulia hadi likafika hapa hivi mama Hata wewe ukikaa huoni kama wananchi wako unawabana sana.

Watu wanaoagiza Vitenge ndio imefika mahali wengine wanasema vitenge vimeshakuwa kama mihadarati yaani kodi ya kuchomoa kontena la vitenge Bandarini unaweza ukakimbia sasa sijui Serikali inamkomoa nani.

TRA imeweka Task force Kariakoo kwa ajili ya kupambana watu walipe kodi matokeo yake Task Force imegeuka Chimbo ya Watu wa Tra kusaka Rushwa yaani hawaisaidii Serikali bali wanajishibisha matumbo yao wenyewe kwa Rushwa sasa hakuna maana ya kuweka Rundo la matapeli mjini badala ya kumuelimisha mtu alipe kodi wao wanakamata mizigo na wanadai rushwa iachiwe.
 
Kodi tumekuwa tukilipa miaka nenda miaka rudi, ila ni muhimu hizi kodi zikapunguzwa.

Kumekuwa na msululu wa kodi nyingi ambazo zimekuwa zikimuumiza mfanyabishara pamoja na Mlaji wa mwisho.
 
Inauma sana nguvu mtu anayotumia kutafuta mtaji, au anakopa kwa masharti magumu halafu unakutana na kodi hazina formula, kichwa wala miguu, halafu kuna hizi dogii za bandari na TRA hazina huruma na wafanyabiashara. Mtafanya watu wajinyonge kwa stress.
 
TRA wamepewa nguvu zisizo stahili, kiasi kwamba hata kama upo sahihi, wanauwezo wa kukufanyia wanacho taka na hamna pakwenda
 
Mtapiga kelele Sana tra wanasimamia tu Sheria hiyo itekelezele ukaguzi wa wa store gown yote hayo ni Sheria ndo inyotaka na imetungwa na bunge Cha msingi na sekondari ni kupeleka bungen mabadiliko ya Sheria za Kodi hicho kinachoonekana hakiko sw lakin kelele zote wako baadh ya watu wakubwa tu wanabiashara pale kariakoo ikumbukwe ukusanyaji Kodi ndo maendeleo ya taifa mukhari ukizidi tunaenda kuwa taifa maskin siku si nyingi dunian
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…