Rais Samia, hili baraza la sasa siyo lako, ni la Magufuli akishauriana na Majaliwa, tengeneza baraza lako!

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
14,360
53,812
Ndugu rais

Kiungwana niseme kwamba nimefarijika angalau kidogo kwa wewe kuchukua hatua ya kurejea makato ya miamala na kutoa muongozo kuwa makato hayo yaangaliwe upya. Binafsi naona kwamba huo ni usikivu na ni ukomavu. Kwa sababu kiukweli kabisa hii kitu ilikuwa imetukalia vibaya sisi wananchi.

Ndugu rais napenda nikueleze mambo kadhaa ya msingi sana ambayo kama unataka mambo yaende vizuri lazima uyafanyie kazi, mambo yenyewe ni haya yafuatayo

1. Hili baraza ulilonalo si lako ni la Magufuli
Ni vigumu kuwatune watu waliokwishajiweka katka staili fulani ya uongozi, sasa ghafla bin vuup kwenda katika utawala mwingine wa mtu mwingine, mwenye hulka tofauti. Hawa wa sasa ndugu rais, asante yao iko kwa Magufuli na Majaliwa maana kikatiba ndo walikuwa na mamlaka ya kuunda serikali, Huenda wewe wanakuchukulia kama caretaker president wa kumalizia muhula wa Magufuli.
Mama vunja hilo baraza la mawaziri uliunde upya, usifanye reshuffle ndogo, piga ile kubwa ili tujue kuwa sasa Samia kaweka serikali yake inayotokana na yeye mwenyewe na siyo hii serikali iliyosheheni watu wa Magufuli

2. Usitawale kwa hulka za Magufuli kwa sababu haiba yako na Magufuli ni tofauti na historia zenu ni tofauti
Magufuli alikuwa ni mtu ambaye alipotaka jambo lake hakujali sheria wala kanuni za mchezo, hakuwa mtu wa haki pale alipoichukia haki na hakuwa mkweli pale alipoona ukweli unamchelewesha na kwa hulka yake ya ubabe hakujali chochote hata kama anaumiza watu namna gani.

Pamoja na hayo Magufuli alikuwa na historia inayombeba, watu walimjua na kumpenda Magufuli sana kabla hajawa rais, kwa hiyo kwa kiasi kikubwa wananchi walikuwa wanajua wana mtu mbabe ofisini anyway. Sasa wewe Rais wetu, wananchi hawana historia yako kubwa zaidi ya umakamu wako wa rais, na kwa haiba yako ni kuwa watu wanategemea kuona mtu muungwana, mstaarabu, mtenda haki. Sasa leo ukibadilika ukajifanya Magufuli wananchi wananusa ufeki.

Mama hiyo njia ya Magufuli wanaiweza watu wenye roho za Kimagufulimagufuli, wewe huiwezi hiyo kwa sababu wewe ni muungwana, una utu. Njia inayokufaa wewe ni kusimama kwenye Kuwaambia ukweli wananchi, hapa unaweza kuazima kwenye namna Mkapa alivyokuwa anawaengage wananchi kuwaeleza ukweli kuhusu utendaji wa serikali yake etc, kama hali ni ngumu waambie watu ukweli, Kama tunakopa hela nje waambie wananchi ukweli, Chagua hata mara moja kila baada ya miezi mitatu uongee na wananchi kama Mkapa alivyokuwa na kawaida ya kuongea na wananchi kila mwisho wa mwezi. Pia tenda HAKI heshimu haki za makundi yote ya kijamii, Kiufupi Simama vizuri kwenye kiapo chako.

3. Kuhusu katiba mpya, kama hofu yako ni kuogopa suala la serikali tatu na hivyo kudhani muungano kukufia mkononi hilo lisikuumize kichwa lete hizohizo mbili "zilizoboreshwa"
Suala la serikali mbili au tatu wananchi waliliona kama nyenzo tu ya kupata civil liberties zaidi, kutokomeza ufisadi zaidi, kuwa na uwakilishi huru na wa haki zaidi, kuyawekea udhibiti madaraka ya rais zaidi. Kwa hiyo kimsingi hili la serikali mbili au Tatu, Ongea na wananchi, waombe hili suala waliache kwanza ila wape Katiba yenye Kuthibiti Maadili ya viongozi ili kuzuia ufisadi, Katiba yenye Mahakama huru, Katiba yenye bunge huru, Katiba yenye tume huru ya uchaguzi, Katiba inayothibiti madaraka na mamlaka ya rais, Katiba yenye masuala yanayogusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Hii inaweza kuwa ni compromise nzuri sana baina ya wanaotaka katiba ya Warioba na wale wenye hofu ya katiba ya Warioba. Ili hili lifanikiwe, Simama sasa, beba hiyo ajenda, Washawishi wananchi wavute subira kwenye ushu ya serikali tatu, ila wape wananchi mengine mengi katika katiba mpya ambayo wanayadai kwa nguvu zote

4. Mama usiwasikilize wahafidhina ndani ya CCM, wengi wanalinda matumbo yao
Hao wanaokushauri uwe bandidu, uwakazie wapinzani, uwe kama Magufuli hawakupi ushauri mzuri, hao wana hofu kuwa ukiwa fair huenda ukawaempower wapinzani na hivyo kujikuta wana wakati mgumu wa kisiasa huko mbele, kwa hiyo wanataka waendelee kubebwa nabeleko ya dola.

Nakushauri utafute wazee wali9kuwa wanajua Kudeal na Wapinzani uwafanye washauri wako wa kisiasa, kuna watu kama Mzee Wassira, mtumie huyo mzee, ni mzuri kwenye crisis management, na haogopi kujibu hoja kwa hoja!

Vision nzuri zaidi ni ile uliyokuwa nayo day one ulipokula kiapo cha urais, vision ya kuwa mtenda haki, mchapakazi, mwanademokrasia, mjenga uchumi imara. Yeyote anayekwambia uachane na ideals values ulizokuwa nazo katika siku zako 100 za kwanza ofisini, huyo hakutakii mema, anataka kukubadili ufuate njia zao zilizojaa kuogopeshana badala ya njia za matumaini

5. Bila political reforms zinazokwenda sambamba na economic reforms mama hii nchi itakuwia ngumu sana
Nimekueleza mwenzio aliyekutangulia alishaamua lolote lile liwalo na liwe, kuumiza watu, kuonea watu, kutumia wasiojulikana, kubambikiza watu kesi, kuvuruga chaguzi, kununua wapinzani, kuwaweka kwenye payroll viongozi wa dini, na kufanya kila aina ya ubandidu ili kulazimisha ukimya ili yeye atawale. Sasa mama wewe hayo hata kama ungetaka kuyafanya, ukiyafanya yatabackfire sana. Ni heri sasa ukaanzisha political reforms ili kuituliza hii nchi, ongea na wapinzani, ruhusu mikutano yao ya siasa ambayo ni haki yao. Na wewe unda Timu yako ya CCM ambayo iko konki ikajibu hoja kwa hoja huko kwa wananchi. Tumia staili ya CCM ya Nape na Mzee Kinana, Kajibuni hoja kwa wananchi. Hapo wananchi wataiheshimu na kuipenda serikali yako, maana wataona ni Serikali inayojiamini.

Usipofanya hivyo utakutana na makundi powerful ya kijamii kama vile Kanisa Katoliki, Kanisa la Kilutheri, Asasi za Kiraia zitapaza sauti kuinyooshea kidole serikali yako na itajikuta katika wakati mgumu mbele ya wananchi, na ukishindwa kumanage political process inayoambatana na reforms za kiuchumi zenye kuwapa wananchi unafuu wa maisha utapambana na riots za mara kwa mara za wananchi.

Mwisho kabisa
Mama sisi tunakupenda sana, yaani tinataka ufanikiwe kwelikweli, tulifurahishwa mno na jinsi ulivyofanya mambo mazuri kwenye miezi yako mitatu ofisini. Sasa tunakuomba usisikilize zile sauti za kukutia hofu eti ukiwa fair kama katiba inavyokutaka uwe basi eti wapinzani watapata nguvu. Wapinzani watapata nguvu kama nyie hamkidhi matarajio ya wananchi, lakini iwapo mtatenda Haki, Mkajenga uchumi, Mkawa na utawala bora, Mkapiga vita ufisadi, Mkaheshimu haki za wananchi na kuwaheshimu wananchi mbona mtakubalika tu!
 
Huu ushauri mnampa mkidhani kuwa yeye ni malaika?

Hata kama amerithi baraza, nakuhakikiahia hakuna anayeweza kwenda kinyume na matakwa yake. Tuache uongo wa kusema eti wanamharibia.

Nakutolea mfano: hilohilo baraza kipindi Cha Magufuli walikuwa hawavai barakoa na wakiamini kuwa corona haipo
Alivyoibgia mama na kusema corona ipo wote umeona walivyobadili gia.

Hii inaonyesha kuwa mawaziri na watendaji wote wa serikali hufuata anayotaka boss wao.

Hivyo tuache kuhisi eti Hawa mawaziri wanafanya kwa kujiamria tu
 
Hata yeye Samia ni urithi wa Magufuri,kama anataka kuunda baraza lake la mawaziri,avunje bunge haitishe uchaguzi mpya,haone kama atatoboa,Samia kapata urais wa ndondokera awezi kubeza wenzake
 
Unataka kusema Rais amekosea kwasababu ya maamuzi ya kupitia upya tozo za simu na shutuma unatupia baraza la mawaziri, ukumbuke ni yeye ndie alieweka saini yake kuruhusu hizo tozo zianze kutumika na akatuambia zinatakiwa kwaajili ya kuendeleza barabara huko vijijini.
 
Huu ushauri mnampa mkidhani kuwa yeye ni malaika?
Hata kama amerithi baraza, nakuhakikiahia hakuna anayeweza kwenda kinyume na matakwa yake. Tuache uongo wa kusema eti wanamharibia...
Kila mtu huchagua timu kwa vigezo vyake.
Huyu kaikumbatia timu ya Magufuli akidhani itaenda na kasi yake kumbe inaanza kumzingua ndiyo maana

1. Waziri wa Mawasiliano Ndungulile alikukuja na bei za juu za bando, Mama akaingilia kati, lakini Ndungulile kauchuna utadhani hakuhusika

2. LNdungulile kwzunguuka kaja na masuala ya hela ya kuchaji laini

3. Mwigulu anatupiga sound kuwa hii kodi ya miamala ni. kodi nzuri sana ya uzalendo, baadae kelele za umma zinakuwa nyingi, Mwigulu anakuja na kiswahili kipya na bado yuko ofisini

4. Majuzi kwrnye umeme LUKU inazingua, na Waziri wa Nishati yuko. ofisini

5. Waziri wa michezo anaingilia mechi ya Simva na Yanga, wananchi wanalalamika na timu zinaingia hasara, Waziri bado yuko ofisini

6. Waziri wa Afya miezi michache iliyopita anatufundisha namna ya kujifukiza, barakoa alikuwa havai, lakinj leo kabadili stratergy

7. Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni tunaona miswada ya kuwaumiza wananchi inapita tu huko bungeni anashindwa kujali maslahi ya wananchi na kujua kuwa wananchi wataumia kwa hizi kodi.

Halafu eti kiusanii waziri mkuu atafanya kikao. na waziri wa fedha na waziri wa mawasiliano kujadili hizi tozo. Walikuwa wapi wakati hizi sheria zikipita huko bungeni?

Ndiyo maana tunasea ni. kuda sada Samia aunde serikali yake aisuke upya, Jii ya sasa ipo kwenye confusion mode, yaani kutoka kufanya kazi na mrawala mmoja kwenda kwa mwingine wenye haiba tofauti
 
Unataka kusema Rais amekosea kwasababu ya maamuzi ya kupitia upya tozo za simu na shutuma unatupia baraza la mawaziri, ukumbuke ni yeye ndie alieweka saini yake kuruhusu hizo tozo zianze kutumika na akatuambia zinatakiwa kwaajili ya kuendeleza barabara huko vijijini.
Kwa katiba yetu hii mbovu tunasema rais alishauriwa vibaya 😁
 
Kitendo cha kujadili upya budget ya serikali kuhusu Tozo inaonyesha bajeti yote imekosa sifa (ni ovyo Bunge linatakiwa kuvunjwa..
Wananchi wameigomea bajeti. Na wabunge ni wawakirishi tu. Sisi wananchi wenyewe tumeigomea serikali.

Je, sheria zinasemaje kwa mujibu wa sheria zenyewe..
 
Kila mtu huchagua timu kwa vigezo vyake.
Huyu kaikumbatia timu ya Magufuli akidhani itaenda na kasi yake kumbe inaanza kumzingua ndiyo maana

1. Waziri wa Mawasiliano Ndungulile alikukuja na bei za juu za bando, Mama akaingilia kati, lakini Ndungulile kauchuna utadhani hakuhusika

2. LNdungulile kwzunguuka kaja na masuala ya hela ya kuchaji laini

3. Mwigulu anatupiga sound kuwa hii kodi ya miamala ni. kodi nzuri sana ya uzalendo, baadae kelele za umma zinakuwa nyingi, Mwigulu anakuja na kiswahili kipya na bado yuko ofisini

4. Majuzi kwrnye umeme LUKU inazingua, na Waziri wa Nishati yuko. ofisini

5. Waziri wa michezo anaingilia mechi ya Simva na Yanga, wananchi wanalalamika na timu zinaingia hasara, Waziri bado yuko ofisini

6. Waziri wa Afya miezi michache iliyopita anatufundisha namna ya kujifukiza, barakoa alikuwa havai, lakinj leo kabadili stratergy

7. Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi mkuu wa shughuli za serikali bungeni tunaona miswada ya kuwaumiza wananchi inapita tu huko bungeni anashindwa kujali maslahi ya wananchi na kujua kuwa wananchi wataumia kwa hizi kodi.
Halafu eti kiusanii waziri mkuu atafanya kikao. na waziri wa fedha na waziri wa mawasiliano kujadili hizi tozo. Walikuwa wapi wakati hizi sheria zikipita huko bungeni?

Ndiyo maana tunasea ni. kuda sada Samia aunde serikali yake aisuke upya, Jii ya sasa ipo kwenye confusion mode, yaani kutoka kufanya kazi na mrawala mmoja kwenda kwa mwingine wenye haiba tofauti
Huna ulijualo ki.ma wewe, unadhani waziri anakurupuka tu sio? uko na ushahidi wa kwamba hili halijatoka kwa mama?
 
Yeye Samia ndio sio makini,yeye akiletewa kila anasahini pasipo kujilidhisha au kusoma Kwanza,alafu kila jambo linaanzia ktk baraza lake la mawaziri ambaye yeye ndiye Mwenyekiti wao.Tatizo la Samia nikuongoza Nchi kupitia mitandao,jambo lolote likipigiwa kelele tu kwenye mitandao basi anaona alifai, wakati anawashauli kibao kwenye ofisi yake,sio kila anayepiga kelele kwenye forms anauchungu na Nchi, wengine wanasubiri haaribikiwe waje kumcheka.
 
Ina maana unaunga mkono hizi tozo?
 
Sio lazima utamtaje JPM ili kujenga hoja yako ya kitoto. Wateuliwa wote wameapishwa na mama, mbele ya camera na kadamnasi.

Tumuombe mama asimame yeye kaka yeye, na atafanikiwa. Akiwaruhusu wasaka tonge karibu yake, amekwisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom