zimmerman
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 1,641
- 3,169
Mama Samia mimi bado nakupenda na nataka ufanikiwe katika miaka yako hii minne iliyobaki, na kama ukifanya vizuri njia nyeupe kwako 2025 - 2030.
Ni kweli kwamba kuhairishwa muda kwa mechi ya Simba na Yanga kwa kisingizio cha ajabu kabisa kumetia doa urais wako, tena mapema sana katika awamu yako. Lakini mambo hayajaharibika kihivyo, bado kuna nafasi ya kuzima hasira za watu, kutengeneza na kukonga nyoyo za watu. Naomba mashauri haya katika kulituliza na kulisongesha jahazi.
Moja, jifunze kutoka kwa mtangulizi wako Hayati Dkt. Magufuli. Mtangulizi wako ashawahi kupitia katika kipindi kama hiki ambacho watu walimpa pressure kweli kweli kuhusu Bashite na vyeti feki vyake. Mtangulizi wako alikuwa na ngozi ngumu hasa na ninakushauri na wewe katika kikpindi kama hiki ujitahidi uvae ngozi ngumu -- uwe thick-skinned, wangereza wanasema. Usikurupuke kufanya maamuzi, kama umeshakosea, umeshakosea. Jipe muda, litafakari hili suala, kama kuna la kujifunza kwamba makosa kama haya yasirudie, basi chukua funzo na lisijirudie tena. Kipindi kama hiki si kipindi cha kupaniki, si wakati wa kumtafuta mchawi. Kuna watu bado wanahisi kuna ombwe la uongozi hasa baada ya JPM na hivyo ukikurupuka kusema chochote au kufanya lolote katika kipindi hiki utaharibu zaidi badala ya kujenga maana watu bado wana machungu mengi.
Pili, baada ya upepo kutulia (na kutulia utatulia tu) naamini utakuwa umeshalitafakuri hili suala na utakuwa na statement ya kutoa. Hii statement usiitoe kwa muktadha wa mechi ya Simba na Yanga tu. Hii inapaswa kuwa statement ya hadhi ya urais, yenye kuonyesha kwamba wewe kama Rais wa Tanzania utatumia nafasi yako kuboost sekta ya mpira (pengine na michezo kwa ujumla). Mtangulizi wako alikuwa na aina yake ya kujiconnect na sekta ya mpira na michezo, na wewe tafuta ya kwako pia. Si lazima uwe mwanamichezo kindakindaki, lakini ukiweza kugusa sekta ya michezo/mpira kwa namna moja au nyingine, utaweza kuwagusa sehemu kubwa ya watu wa Tanzania. Nakushauri wewe binafsi usipange kukosa mechi ijayo ya Simba na Yanga. Tafuta namna uwepo uwanjani.
Mwisho, kama nilivyokwisha kudokeza, kuna watu wa kutosha tu katika nchi hii ambao bado wana mashaka kama unaweza au hauwezi. Sasa jionyeshe kuwa unaweza. Na hii sentensi iko loaded, lakini naamini umenielewa. Mama achana na vispeech speech, fanya maamuzi magumu. Toa agizo. Tembelea. Fuatilia. Tekeleza. Kuna sababu kwanini Hayati Magufuli alikuwa effective, na baadhi ya sababu hizo zinapaswa kuwa sababu zako, na mengi ya mambo ya Hayati Magufuli kuwa mambo yako.
Asante.