Kuelekea 2025 Rais Samia: Bila CCM imara Tanzania itayumba

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
2,170
5,528

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewaomba Machifu kuhamasisha watu waowaongoza kuchagua vongozi kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika mwaka huu kwani chama hicho kimekuwa kikisimamia serikali vizuri.

Akizungumza na Machifu hao leo Jumamosi Julai 20 2024 Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma, Rais Samia amesema "ukweli ni kwamba na tulisema miaka mingi wazee wetu walituachia huo msemo kwamba bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, lakini bila CCM pia serikali itayumba"

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa sifa anazopata na maendeleo yanayopatikana nchini ni kutokana na usimamizi madhubuti wa chama hicho kwa serikali "mmemsifu sana Chifu Hangaya(Rais Samia) hapa nikawa namsikiliza Mpoto na Mwanamila na wote wamemsifu Chifu Hangaya jinsi serikali inavyokwenda na maendeleo yaliyopatikana na kazi inavyofanywa lakini yote kwa sababu CCM iko imara na inasimamia serikali yake na ndiyo maana yakatendeka"
 
ph_30468_111097.jpg

Bila CCM imara?! Au hamuoni Madaraka yamemifanya muwe Viziwi na Vipofu.
 
Back
Top Bottom