Rais Samia ana kitu cha ziada atafika mbali Sana

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
12,485
50,897
Mwanzo mimi ni moja ya watu ambao sikuamini kwamba Rais wetu mpendwa atatuvusha katika utawala wake.

Lakini baada ya kuzitazama tawala zote 6 toka tupate uhuru pengine Rais Samia kwa mtazamo wangu ni Rais mwadilifu baada ya Hayati julius Nyerere.

Ndiye rais ambaye hana makelele na hotuba za kujitetea yupo direct ikiwa nyeusi atakwambia nyeusi.

Akisema ni usiku hauna haja ya kutoka nje kama kipindi cha Kikwete na Magufuli kuchungulia kama kweli jua haliwaki.

Mwanzo nilikuwa na mashaka kwenye kodi lakini kwa Sasa serikali ndio inakusanya kodi kuliko wakati wowote tena bila kutumia nguvu.

Nikawa na wasiwasi kwenye ajira Sasa naona kila mwaka ajira zinazidi kumwagwa tu hata kama watu wanalipa kodi wanajua watoto na ndugu zao watapata ajira.

Transparent kwenye serikali yake watu wanasema pesa zinapotea Sana ukweli report za CAG toka miaka ya 1961 hakuna report ambayo serikali ilikuwa safi na pengine tunaona pesa zimepotea Sana kwa sababu ya uwazi wa mama ndani ya serikali yake ila toka utawala wa Nyerere pesa uwa zinapotea.

Mama apewe mitano tena 2025-2030 ana kitu na tutafika mbali sina ninachomdai.
 
Mkuu nakupongeza kwa Hoja yako ila mwombe atupatie KATIBA MPYA yenye kuunda Taasisi na Idara Imara ndani ya Serikali, kama Taasisi ya Uchaguzi; Idara ya Mahakama; n.k.

Aidha kwenye kupiga kura, yale box la kutumbukiza makaratasi ya kura zilizopigwa yawekwe mahali pa wazi na sio kule chemba ambako mpiga kura anaweza kujazia na makaratasi mengine yaliyopigwa tayari, maana hapo ndio penye wizi. Hakuna tofauti kati ya Wizi wa kura na Wizi wa fedha za Umaa.
 
Awamu ya 6 akili kubwa nguvu kidogo, hakuna mihemko wala kupaniki.

Kama kawaida yake alivyo jisemea yeye mwenyewe huwa anafoka kwa peni........
 
Kuna Waziri nimesikia amenunua Malori makubwa ya mizigo 50 kwa mkupuo.

Urefu wa kamba gani huo Madam?
 
Kuna Waziri nimesikia amenunua Malori makubwa ya mizigo 50 kwa mkupuo.

Urefu wa kamba gani huo Madam?
Kweli kwenye kufa kuna kufaana.

Hapo ni ajira za madereva 50 na utingo wao. Ukiachilia mbali kazi za service na ufundi garadge.
 
Hizo pesa alizoiba zingeajiri manesi madokta walinzi wangapi?
Pesa za malori 50 zinaajiri madokta wangapi? Zingeenda kwenye mafuta ya VX. Ma V8.
Mwizi aliyeiba mkate akamgawia mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom