Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,709
- 13,461
Rais Samia Suluhu Hassan amewasili katika Viwanja vya Makazi ya Rais (Bogor Presidential Palace) Jijini Jakarta, Indonesia na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Joko Widodo ikiwa ni sehemu ya ziara ya siku mbili nchini hapo.
Rais Joko Widodo ambaye alifanya ziara Nchini Tanzania, Agosti 2023 amempa mwaliko Rais Samia ikiwa ni mwendelezo wa ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Nchi hizo.
Viongozi hao wawili wameshuhudia Mabadilishano ya Hati za Makubaliano (4) na Barua ya Kusudio (1) vikiwa zinagusa Sekta za Uchumi wa Buluu, Kilimo, Madini, Diplomasia na Uwekezaji.
HATI ZA MAKUBALIANO ZILIZOSAINIWA
- Rasimu ya Hati ya Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika Nyanja ya Uchumi wa Buluu
- Hati ya Makubaliano kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Kilimo
- Hati ya makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Indonesia kuhusu Ushirikiano katika Sekta ya Madini.
- Hati ya Makubaliano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje Tanzania and Wizara ya Mambo ya Nje Indonesia kuhusu Ushirikiano wa Kujengeana Uwezo katika Masuala ya Kidiplomasia.
- Rasimu ya Barua ya Kusudio kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Indonesia kuhusu kukuza na kuwezesha Uwekezaji
- Hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTDADE) na PT Perusahaan Perdagangan Indonesia
- Hati ya Makubaliano kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Teknolojia cha Bangung
HATI ZA MAKUBALIANO ZA SEKTA BINAFSI (PRIVATE SECTOR MoU’s)
- Hati ya Makubaliano kati ya Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo ya Tanzania, Chemba ya Taifa ya Biashara ya Zanzibar na Chemba ya Biashara na Viwanda ya Indonesia.
KUTOA NENO KWA WANAHABARI
Rais Samia akizungumza na Waandishi wa Habari amesema makubaliano hayo yataimarisha miaka 60 ya kidiplomasia na uchumi.
Miongoni mwa masuala waliojadili viongozi hao ni namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji ambapo Tanzania ipo tayari kuwa mwenyeji wa mkutano wa kwanza wa tume ya Makubaliano ya ushirikiano.
Pia kumekuwa na majadiliano ya namna ya kuendeleza ushirikiano katika uwekezaji kwenye sekta ya mafuta na gesi huku kampuni ya Indonesia ya Pertamina ikiongeza hisa Mnazi Bay, Mtwara.
Mbali na kujenga uwezo kwa wafanyakazi wa TPDC, pia Indonesia ina nia ya kampuni yake ya ESSA kuwekeza kwenye kilimo hususan mbolea na Medco Energi kwenye upande wa nishati.
Upande wa sekta ya dawa, kipaumbele hasa ni Indonesia kuiuzia Tanzania dawa ambapo kwa kuanzia zitakuwa za saratani.
Aidha, kutokana na viongozi hao kushiriki kupanda mti, Rais Samia amesema hiyo ni ishara ya kuonesha kujali na kulinda mazingira.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha wageni mashuhuri mara baada ya kuweka shada la maua kwenye mnara wa kumbukumbu ya Makaburi ya Mashujaa ya Kalibata wakati wa ziara yake ya Kitaifa Jakarta nchini Indonesia tarehe 25 Januari,2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Waandishi wa Habari pamoja na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace nchini humo tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo kabla ya kwenda kupanda mti wa kumbukumbu katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo wakati akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kupokewa Rasmi katika viwanja vya Makazi ya Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo Rasmi na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo pamoja na ujumbe wake katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo katika Ofisi za Rais huyo Bogor Presidential Palace tarehe 25 Januari, 2024.
Pia soma: