Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,638
Haya vijana langu jicho.
Hii ilikuwa kambi ya wakimbizi..wa kihutu...1995.. jeshi lililokuwa..linaongozwa na General kagame kufanya mauaji...ya watu takribani laki moja ambao ni kutoka jamii hio ikiwemo watoto.. hio link ina picha na maelezo zaidi..na mpaka leo serikali yao wanatambua..338 tu...
tupo pamoja mkuu. nlikua na maana yangu kUsema PK ni bora. akilegeza kidogo tuu kwisha. ni bora wachache wafe kuliko mamia wafe.Simhukumu maana sikuwepo; ila unaelewa nini maana ya vita! Na unakubaliana na mimi kwamba bado vita ilikuwa inaendelea? Waasi wa FDLR unawajua? Labda kwa uelewa wangu nikujuze kidogo, il pia nikuombe ukafanye utafiti. Mi ni mnyarwanda halisi, wa kuzaliwa kabisa. Na wakati huu nilikuwa Rwanda. Mwaka 1959, kuna wanyarwanda walichomewa nyumba zao, kunyanganywa mali zao na kuliwa mifugo na jamii iliyokuwa inaitwa wahutu. Hawa walionusurika kufa walikimbilia Uganda. Wapo vijana wa kike na kiume, wakimbizi; miaka hiyo nadhani mtu Idi Amin alikuwa madarakani kama sikosei(historia hio siijui vizuli kama ntakosea utanikosoa). Hawa watu waliendelea kuzaliana, wakawa wanaongezeka, hivyo kuwa mzigo kwa taifa lililowapokea, baadhi walianza kujiunga na jeshi la Uganda kumsupport Museveni kumtoa Amin. Kilichotokea, badae walianza kufukuza hao wakimbizi, na vijana wao ndo walkuwa jeshini, sasa ilikuwa hawataki kunyanyasika. Kwao hawahitajiki, na walipo wanafukuzwa, swali; waende wapi? Badae walikuja kufukuzwa.Kufika mpakani jeshi la Rwanda enzi hizo halikuwaruhusu kuingia nchini.Na jeshi la Uganda halikuwahitaji kwenye ardhi yao. Unadhani walienda wapi? Kuna mto unaitwa"UMUYANJA" mpakani, walilala humo kwenye maji wamesimama. Jiulize adhabu hio mpaka kulikucha, watoto, wanawake na waume zao na vijana katika hali hio. Waliomba kurudi kwa mda, ampapo serikali ya Rwanda ilitamka kwamb"MAJI YAKIJAA GLASS,UKIONGEZA MENGINE YATAMWAGIKA. NCHI NI NDOGO NA SISI HAITUTOSHI, HIVYO HATUNA PA KUWAWEKA"Maneno hayo yalitamkwa na Rais Habyarimana.
Walirudi, ndo wakaanza kujipanga kuikomboa nchi ili na wao wapate pa kukaa.
Nakumbuka, kuna mashimo mengi yalichimbwa nchini, kwa madai ya kwamba wanatafuta maji. Ebu fikilia unakuwa na shimo la mita zaidi ya 100, na upana wa zaidi ya m5! Nani alijua lengo!? Madarasani. wanafunzi walikuwa wanatenganishwa zinatengenezwa orodha za kila kabila.Uraiani ilikuwa hivo.Watusti walikuwa wananyanyaswa, ukibahatisha umesoma, kazi ni ualimu tu.
Ni stori ndefu, ila niruke mpaka mwaka 1994. Wakati raisi anatoka Arusha, alikuwa hana ujanja tofauti na kusain imakubaliano ya Arusha, na hayo yalikuwa ya kuwapa haki sawa raia wote(kazini, jeshini, serikalini) sasa kuna watu wake walikuwa hawataki kabisa.Na inasemekana wao ndo walidungua ndege yake. Nani hapendi madalaka? Ile nafasi ya urais yawezekana ni tamu sana.
Mapanga yalikuwa yameagizwa kwa wingi, siraha ndo usiseme, vijana wamepewa mazowezi ya kijeshi kwa wingi. Kwa kifupi mauwaji yale yalikuwa yamepangwa siku nyingi.
Sasa ukisema kwamba Kagame ameuwa; walivyokuja unakubaliana na mimi kuna watu walikuwa bado wanaendelea kuuwawa? Wengi wao wakiwa na familia zao nchini humu? Unataka kuniambia kwamba utakuja ukute familia nzima imeteketezwa kinyama, utakaa utulie?
Haya, hio link uliyoiweka, baada ya nchi kuinia mikononi mwa RPF,ilikuwa inaitwa APR kipindi hicho, wanajeshi wa Habyarimana hawakuacha kuvamia nchi kwa lengo la kupigana na jeshi la APR na kurudisha nchi mikononi mwao. Walivyokuwa wakivamia, bado mauaji yaliendelea, mashuleni, ma hospitalini, barabarani magari yalikuwa yakitekwa; na kilichokuwepo ni wahutu pempendi, na watutsi kando, group mbili zionekane. Wakifanya hivyo, watutsi wanauliwa, wakigoma, wote wanauliwa, na makazi yao yalikuwa kambini si kwingine.
Kukomesha hilo, jeshi lililazimika kuwafata huko huko. Sasa ulitaka aache watu waendelee kuuwawa? Na mpaka leo hii navyoandika hivi, nikwambie kwamba kuna waasi bado wanaingia, na raia wanakamatwa kwa kuwa support! Hivyo akilegeza, bado kuna watu wako radhi damu imwagike tena. Yasikie kwa mwenzio sisi tunayajua vizuli kaka.
Samahani nimeandika mengi ila nadhani kuna uelewa furani utakuwa nao. Nakuomba kama uko interested utafute watu wanaoijua Rwanda wakuelee. Ukisema watu hawana uhuru wa kuongea, ni kweli, ila sasa, watu walioko jera leo hii unadhani familia zao zinafurahi? Na unadhani hata hao wafungwa kuna anaekubali kwamba aliua? sasa ukimpa uhuru wa kuongea, alieuliwa atatoa ya kwake, vita ianze upya, aliyeua nae atadai unamsingizia vita ianze upya! Acha tu wanyarwanda tunyamazishwe ni haki
tupo pamoja mkuu. nlikua na maana yangu kUsema PK ni bora. akilegeza kidogo tuu kwisha. ni bora wachache wafe kuliko mamia wafe.
ndo hivo mkuu.Nimekusoma, unajua wapo wengi wazuri kuongea bila uelewa