Rais Mh. Dr. John Pombe Magufuli unamanisha nini katika hili?

yeye hachukii vyombo vya habari anachotaka mujaze masifa tu hapa,mkifanya hivyo anaweza kuifanya jamii forum wizara ya serikali kabisa
Kuna watu walizoea kumsifia mpaka akasifiwa na feki news! tabia za kusifiwa ni za kik,e mwanaume hapendi sifa bwana,
 
Hotuba za mkuu wetu kila siku ni afadhali ya jana.Zinaogofya ,kuvunja umoja na uzalendo.
 
Sikuwa na imani na ushindi wake lakini niliamini ataendelea kuliunganisha taifa na kuendelea kubaki kitu kimoja..

Ninachoona na kusikia kwa sasa ni tofauti kabisa.. Mihemuko, chuki, mahasira kwa watu wanaomkosoa sio vya kawaida kabisa..

Mtu anataka kugeuka hata mhariri wa vyombo vya habari!
Anawachukia Wapinzani ,makabila yao, majimbo yao na Mafanikio yao. Sijapata kuona Mpenzi wa sisiemu kama huyu! Hata muasisi wake aliyewapenda wanae wabunge wa Upinzani hamfikii. Chuki Chuki hadi zinakera.
 
Mimi sina kadi yoyote ya chama. Hivyo naomba mnisikilize. Wamaziri na Bunge inabidi wajikaze wamwambie ukweli. Kuwa kuwa un mazuri unayofanya. Shirikiana na wananchi wote. Taifa siyo chama. Milioni 8 waliopiga kura siyo wote wanachama. Mimi sikumpigia lakini ni raia wake.Utupende wote. Aache chuki,ubaguzi,unafiki,aeleze ni kwa nini anainda bashite. Kuna uhusiano wa aina gani.kuna tetesi:
Bashite amegushi cheti
Bashite ameanbush Clouds
Bashite ni mla rushwa kwani mali aliyonayo siyo halali
Yote umeyafungia macho bila maelezo.
Please watu wapate majibu!!!
 
Sikuwa na imani na ushindi wake lakini niliamini ataendelea kuliunganisha taifa na kuendelea kubaki kitu kimoja..

Ninachoona na kusikia kwa sasa ni tofauti kabisa.. Mihemuko, chuki, mahasira kwa watu wanaomkosoa sio vya kawaida kabisa..

Mtu anataka kugeuka hata mhariri wa vyombo vya habari!
Mkitaka taifa liwe kitu kimoja lifikirie kitu kimoja tukubali kuviondoa vyama vya upinzani..ila kwa nchi yenye upinzani usitegemee hayo unayoongea..maana serikali iliyopita ililaumiwa na upinzani kwa kuwaacha wafanyakazi wazembe..ilipoingia hii ikawatumbua..upinzani as usual wakapiga tena kelele..jpm akaacha..wanalia tena makonda atumbuliwe khaa..kwa akili hizo mnakuwaje kitu kimoja??
 
Zambia na malawi Marais walifia ikulu wapo watu wanatamani siku moja muujiza utokee Tanzania ingawa wengine wanatamani kile kikundi cha Uchakachuaji wa kura kisambalatike ili 2020 apate shida akose kura katiba ibadilike iwe na kipengere cha kumshitaki Rais mstaafu kwa mabaya aliyotenda akiwa madarakani.
Tukikuuliza ni lipi baya kalitenda utatuambia??
 
Wadau,mimi siangalii kauli tuuu,ziwe za sasa au za nyuma,bali naangali na kufuatilia mienendo.
Mienendo ya mambo mengi sana,mfano
Upangaji wa safu zake za kiuongozi.
Pangua pangua zake,zinafanyikaje,kwa watu gani,wakati gani na kwa namna gani
Naangalia hisia zake katika kila jambo analofanya.
Naangalia mausiano yake na wazee,viongozi wa kichama,viongozi wa kidini,viongozi wa kimataifa.

Najaribu kufupisha,kiukweli NAOGOPA,naogopa sana.
Sioni hali ya kuridhisha.
Mfano kauli ya jana,ilihitimisha chambuzi zangu,pale alipo sema nanukuu"kunawatu wanataka taifa hili liangamie" Swali nililo jiuliza KWA NINI AKILI YAKE ILIWAZA VITA????
 
Bila shaka wanajamvi mko salama, kwakweli nimefuatilia sana kauli za mkuu wetu wa nchi kwa muda mrefu na leo naomba niongee yafuatayo. Hakuna ubishi kua tangu Mh. Magufuli tangu uapishwe kua rais wa nchi hii na badae mwenyekiti wetu wa CCM kuna mambo umefanya vizuri lakini kuna mengi kweli umeharibu sana.

Leo naomba nijikite kwenye kauli zako ambazo unatamka dhidi ya watanzania wenzako ingawa ata huku nyuma uliwai kutamka tu nyingi. Sina haja ya kuzirudia zote kama kule Kagera ila kauli uliyotoa Zanzibar na jana kuhusu vyombo vya habari zimetuangusha sana kama Taifa mbele ya majirani na marafiki zetu. Sikuona haja ya Mh. Rais kutoa kauli yenye vitisho dhidi ya raia wako uliowaomba kura ili uwatumikie.Unaposema kuwa hamna freedom ya hivyo moja kwa moja kumbuka unaivunja katiba ya nchi yetu ambayo uliapa kuwa utailinda ingawa mpaka leo bado una imani kuwa katiba sio kitu mbele yako.

Mh. Rais kuna mambo ambayo unabidi ujikumbushe au ukumbuke ....mfano vyombo hivi hivi vya habari ndivyo vimetumika kukutafutia kura na kukunadi wewe lakini vyombo hivi hivi ndio njia rahisi unayo itumia kupeleka ujumbe kwa watanzania.

Kumbuka pia sio rahisi na jambo hili haliwezekani kuwa kila siku habari iwe ni wewe tu au mawazo na habari unazo zipenda wewe...hata DJ ana miziki anayoipenda yeye lakini akiwa kazini analazimika kucheza miziki inayopendwa na wataje.

Mwisho Mh. Rais nakukumbusha kua Taifa ili ni zaidi yako na mimi .Tusifanye au kutamka kauli za kuliangusha Taifa maana limejengwa kwa nguvu kubwa.Badirika mkuu kwa maslahi ya Taifa ili Tanzania.
tapatalk_1490437105033.jpeg

Nimeweka picha ili iongee.
Sitaki kuitwa mchochezi mie....
 
Mkitaka taifa liwe kitu kimoja lifikirie kitu kimoja tukubali kuviondoa vyama vya upinzani..ila kwa nchi yenye upinzani usitegemee hayo unayoongea..maana serikali iliyopita ililaumiwa na upinzani kwa kuwaacha wafanyakazi wazembe..ilipoingia hii ikawatumbua..upinzani as usual wakapiga tena kelele..jpm akaacha..wanalia tena makonda atumbuliwe khaa..kwa akili hizo mnakuwaje kitu kimoja??
Kuna uwezekano mkubwa sana kichwa chako kikawa hakiko sawa..

Vyama vya siasa haviawahi kututenganisha hata siku moja.. Kukosoana sio kuchukiana na ninapozungumzia kuliunganisha taifa sina maana ya kuacha kukosoana pale tunapokosea..

Ni mwenyekiti gani wa chama cha siasa uliwahi kumsikia anawashutumu wanachama wake kuwa ni wasaliti kwa kutaka tu kwenda kumuona mtanzania mwenzao aliyepatwa na matatizo kisa tu eti ni wakutoka chama pinzani?
 
Kuna uwezekano mkubwa sana kichwa chako kikawa hakiko sawa..

Vyama vya siasa haviawahi kututenganisha hata siku moja.. Kukosoana sio kuchukiana na ninapozungumzia kuliunganisha taifa sina maana ya kuacha kukosoana pale tunapokosea..

Ni mwenyekiti gani wa chama cha siasa uliwahi kumsikia anawashutumu wanachama wake kuwa ni wasaliti kwa kutaka tu kwenda kumuona mtanzania mwenzao aliyepatwa na matatizo kisa tu eti ni wakutoka chama pinzani?
Vipi chadema walipogoma kusalimiana na wabunge wa ccm kwa sababu ya tofauti za kiitikadi bungeni?? Vipi maalim seif alipogoma kumpa mkono dr shein kwa sababu za kisiasa?? Vipi mbowe alipotaka lowasa achomwe moto badala ya kuachwa mtaani huku vibaka wakichomwa moto?? Vipi wabunge wachadema wanapotoka bungeni pindi rais anapokwenda kuhutubia bunge..?? Huyo sio utengano wa kitaifa..that's y nakueleza panapokuwa na upinzani usitegemee hayo unayoyataka wewe..
 
Ndio mkome kukabidhi nchi kwa mtu mmoja watu wanashangaa sasa lakini hawakumbuki kwenye kampeni 2015 alikuwa anasema serikali ya magufuli itafanya hivi ama vile mlijua anaiokoa ccm tuu ehh kwa taarifa yenu aliichukua na nchi nzima mikononi mwake kazi mnayo kuirudisha tena kwa wananchi maana kwa sasa ni ONE MAN SHOW anaamua kuteua ama kufukuza tuu apendavyo mambo ya uchumi na njaa zenu haimuhusu
 
Mheshimiwa Rais naona wa Tz wanatumia muda mwingi sana mitandaoni kuliko "hapa kazi tu".
Uliliwekea msimamo la muda wa kunywa pombe,na hili la mitandaoni liwekewe muda.
Tumeshaji-tune kwa la muda wa kwenda bar,tusaidie na hili pia la ku-like mitandaoni. Linataka kuwa out of hand sawa na la viroba lilivyo kuwa.
Hebu Mpe assignment waziri na watendaji wake. Muda unaotumika mitandaoni ni mwingi mno. Hata ufanisi pia ktk majukumu ya wanaoitumia unashuka.

Mtu akianzisha topic mitandaoni wanaoichangia ni wengi mno kwa muda mfupi.

Wakifungiliwa access baadae ya SAA za kazi tu tutakuwa na michango mizuri pia itakuwa ni mbadala wa kulewa pombe bar hivyo kutumia muda vizuri baada ya kazi.

Nimetoa mawazo yangu kwa nia njema kwa nchi yangu.
We unadhani kila mtu anafanya kazi muda ambao wewe na wenzako mnakuwa kazini?
Kwa kifupi tunatofautiana muda wa kwenda kazini.
Wengine kazi zao ni za kuwatukana watu mitandaoni.
 
Back
Top Bottom