Rais Magufuli na mtikisiko wa siasa za upinzani Tanzania

Faru John II

Senior Member
Dec 27, 2016
134
135
Siasa za Upinzani zilianza kujipatia nguvu punde tu baada ya udhaifu uliojidhihilisha wazi wakati wa Utawala wa Rais Nyerere ikiwa ni matokeo ya kushindwa kwa Azimio la Arusha na Sera ya Ujamaa na kujitegemea, vita vya Kagera, Ukame pamoja na mtikisiko wa Uchumi duniani hali iliyoipelekea serikali ya Mwalimu kukimbilia katika mikopo Benki ya dunia(WB) na shirika la fedha duniani (IMF) ambapo mkopo huu haukuwezekana mpaka masharti kadha wa kadha yatekelezwe hali iliyopelekea Kung'atuka.

Ugumu wa maisha, kudhorota kwa huduma muhimu za binadamu kama Afya, elimu na miundombinu ya maji na barabara, kushindwa kulipa mishahara hali iliyopelekea baadae kuanzishwa Sera ya kubana matumizi wakati wa awamu ya pili ambapo watumishi wengi walipumzishwa kazi. Busara za Mwalimu zilimpelekea kutoa funzo kubwa kwa viongozi wote wa Afrika na dunia kwa ujumla kuwa KARAMA YA UONGOZI HAINA HATI MILIKI HIVYO WENGI WANAYO PIA, akaamua Kung'atuka akiamini kuwa kwa vyovyote vile hakuna anayeweza kuivusha Tanzania katika dhoruba ile ispokuwa ALI HASSAN MWINYI jambo ambalo halikumshusha heshima Mwalimu ispokuwa limemfanya awe nembo muhimu ya Uongozi Afrika na dunia kwa Ujumla.

Rais Mwinyi naye kwa kuenzi busara za mtangulizi wake alienda mbali zaidi na kuanzisha na kuongoza harakati za kuruhusu Upinzani Tanzania akiwa ni mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Nani kama miamba hii ya Uongozi Afrika? Tunajifunza kitu hapa? Waliona viongozi hawa kuwa hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu hivyo ili tufanikiwe tunahitaji kuyaona mapungufu yetu kwa kujikosoa na kukosolewa hali iliyotia tashididi ya kuanza kwa siasa za Vyama vingi (Multipartism).

Vyama vingi baada ya kuanzishwa tu watu walipata uhuru wa kuisema na kuikosoa serikali hadharani japokuwa uhuru huu haukuwa mkubwa kwa kuwa sheria bado ilibinya uhuru huu.

Uwazi katika ofisi za Umma haukuwepo hali iliyozuia kushamili kwa siasa za Vyama vingi kwani wapinzani hawakuwa na data za kutosha kuisema serikali. Matukio ya vitisho, kumwagiwa tindikali yalishamili hali iliyopelekea Wananchi wengi kuogopa siasa za Upinzani na wengine kuhisi kuwa Upinzani ni madhambi.

Kuingia kwa Uongozi wa JK kumeimarisha kwa kiwango kikubwa mno Upinzani wa Tanzania kwa kuimarisha Uhuru wa habari, kubadili baadhi ya sheria kandamizi, kuimarisha bunge na kulifanya liwe na makali, kuhamasisha kamati muhimu ziongozwe na Upinzani hali iliyoibua Uozo mwingi serikalini ikiwemo EPA, RICHMOND, MEREMETA, BUZWAGI, RADAR, ESCROW, nk

Kuingia kwa Dr. Magufuli na mlengo wa siasa za kazi tu na vitendo kuliko maneno kumenyima hoja Upinzani wa Tanzania kwa kiasi kikubwa kwani Watanzania tulijijengea Utamaduni wa kusema sema tu na kutuhumu watu bila ithbati ya tafiti, udhaifu ambao ndio ulikuwa ndani ya kambi rasmi ya Upinzani ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 CHADEMA ilikiri kuwa ilimtuhuma Edward Lowassa kimakosa katika kashfa ya RICHMOND, hatua hii inanipa nguvu kuamini kuwa siasa za maneno matupu zinatupotezea muda na siasa za HAPA KAZI TU ndio suluhisho la kudumu kufikia UCHUMI ZA VIWANDA. Napongeza uamuzi wa MOSES MACHARI kukataa kuwa mnafiki na kukiri wazi kabisa kuwa Upinzani umeishiwa pumzi ya kumkimbiza Rais Magufuli.

Wito wangu kwa Wapinzani wa Tanzania ni kuwa Wabadilike na Wahamie siasa za Vitendo. Kama Tanzania imefaulu kuzima mitambo ya Analogy na kuhamia digital wao wanashindwa wapi tuwasaidie?

Msimamo wa Mwandishi ni kuwa Hana chama wala hajawahi na hatarajii kuwa na chama mpaka atakapoliona kaburi.

Mwandishi ni

Adnan Mahmoud (Prof Kasongi S. M)

MSc. Health systems Management
 
 




Aise umenena sana big up .
 
Atapata kwani sasa hivi Rais yupo juu ya kila kitu hata Katiba.Akazane sana
 
Kazana hizi ndizo hoja anaOzipenda Mtukufu sana Rais wa Malaika.Kazana zimebaki nafasi mbili unaweza kupata moja.
 
Hao waliotangulia ndio waliopandisha nchi sasa ninainyoosha. Msinipigie kelele. Unafikiri kupata PhD ya kemia ni mchezo? Jaribuni muone
 
Lakini mkumbushe ni vya wanawake sasa.
Mpwa watu wana roho ngumu! Kama mtu anaweza kuandika namna hiyo kitu ambacho hata yeye hakiamini atashindwa kuvaa gauni ili apitishwe kama mwanamke? Sijui!
 
Upinzani imaraa tanzaniaa imaraa,,, mfanoo ccm. Wamewaambiaa wanannch wenyee njaa serikali hainaa shambaa,,,, baadaa YA upinzaanii kujaa juuu wanasemaa wanachakulaa cha kutoshaaaa VP upnzan ucngee kuwapoo,,,,,,????? Tatzooo mnafikiliaa pafupii sanaaaa
 
Ni mjinga tu anaweza kudhani upinzani umetetereka... Upinzani kwa sasa umepata nguvu maradufu kutokana na yanayoendelea. Watch this space
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…