Rais Magufuli kuwa fair kwenye utumbuaji majipu

Mnasihi

JF-Expert Member
Oct 9, 2013
7,754
7,091
Nakiri kufuatilia kwa makini utendaji wa mh. Magufuli rais wa JMT katika kuurejesha uadilifu kwa baadhi ya watendaji wa umma.
Katika kupigana na ufisadi, aanzie miaka 20 iliyopita ili kuleta msawazo utakaokubalika kwa wote na kujenga pamoja na kumuimarisha rais.
Namshauri hivi kwa sababu baadhi ya marais waliopita wanatajwa waziwazi kufisidi nchi wakiwa madarakani na ushahidi upo sio wa kutafutiza.
Kama hivi ndivyo basi rais waondolee kinga ili wakajibu kwenye vyombo vya kisheria ili isijeonekana kuwa hutumbui majipu bali ni usanii wa kuvikuna vipele tu. Kuwa sawa kwa wote bila kujali mhusika aliwahi kuwa nani kwani wote ni raia na tuna haki sawa mbele ya sheria.
Changieni mjadala bila jazba. Karibuni.
 
Mwakyembe , kitwanga na January Makamba wamemshinda sembuse Marais wasitaafu ?
 
Mkuu, kwa kweli na mimi naona wanasiasa wa kitumbuliwa ni wengi sana, ila hilo halifanyiki, sema watumishi wa umma ndo wana immediate impact kwenye maisha yetu labda ndo maana kaamua kuanza na hao
 
Haya sasa magoli... mbona hata miezi sita haijapita jamani.. mnafikiri kweli Rais angetakiwa kufanya mambo yote yanayotusumbua tangu kabla ya uhuru? Tuwe fair kwake.. mwendo wake mzuri
 
Haya sasa magoli... mbona hata miezi sita haijapita jamani.. mnafikiri kweli Rais angetakiwa kufanya mambo yote yanayotusumbua tangu kabla ya uhuru? Tuwe fair kwake.. mwendo wake mzuri
Kwahiyo kwa akili zako timamu Magufuli atafanya yote yanayotusumbua toka uhuru?
 
Mkuu, kwa kweli na mimi naona wanasiasa wa kitumbuliwa ni wengi sana, ila hilo halifanyiki, sema watumishi wa umma ndo wana immediate impact kwenye maisha yetu labda ndo maana kaamua kuanza na hao

Afadhali angeacha wote na kuanza sasa. Lakini kumtumbua Mkurugenzi fulani kwa kosa la awamu ya nne bila kumtumbua au kuwafikisha mabosi wake walio shiriki naye ama kuubaliki ufisadi huo, ni uonevu wa hali ya juu sana maana unyonge wao ndio unasababisha watumbuliwe.

Lakini jibu ni wao kujitokeza kuuambia uuma nini haswa kilijili. Lakini hii haina maana tunawatetea, watumbuliwe tu, walizidi kwa nini hawakukataa wakati ule kweli!
 
richmond ni ya lowasa pesa alizoiibia nchi ndio anakula na Chadema
Umekariri maneno yaliyotingwa na Membe, January na Nape kisha mkalishwa mmekariri hadi Leo , zinduka kwanza kaulize wapo Wapi waliokula pesa za Escrow, NIDA , kivuko, mabehewa , ATC, Chenji ya Rada, Chenji ya Bunge la katiba, bomba la Gesi , Lugumi, kutapeli wazungu ( mtaliano ) Kwa kivuli cha ikulu .
 
Mkuu, kwa kweli na mimi naona wanasiasa wa kitumbuliwa ni wengi sana, ila hilo halifanyiki, sema watumishi wa umma ndo wana immediate impact kwenye maisha yetu labda ndo maana kaamua kuanza na hao
Magufuli anachagua Majipu ya kutumbua akiona JIPU ni Hatari analikumbia , mfano Lugumi kapiga Dili Wizara zingine kibao wamebuni mbinu ya kuzituliza kamati za Bunge kimya kimya zisiongeze Tuhuma zingine huko kwenye mawizara mengine italeta nguvu Kwa Ukawa na huenda ingeonyesha kuwa vita ya Majipu imefeli , kutumbua Majipu Sugu kunahitajika mtu mwenye ujasiri wa kweli Kama marehemu Sokoinne .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…