crome20
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 1,168
- 779
Sababu zake zinajulikana. Na kauli mbio yake inaeleweka "Tutawasha Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike mpaka nje ya mipaka yetu, ulete matumaini pale pasipo na matumaini, ..." Haya yanaweza kuhamasishwa bila gharama kubwa kama kukimbiza mwenge nchi nzima, au ikafanyika mara moja kwa miaka mitano. Tunaweza pia kuweka vipindi maalum kwenye radio za TV za TAIFA kuhusu kuhamasisha uzalendo n.k. Kwamba ulianzishwa na akina Nyerere haimaanishi hatuwezi kubadisha mfumo bila kupoteza maudhui. Usimdhalilishe mwalimu aliyekufundisha kwa kukalili tu matukio.Ifike wakati tuanze kuulizana vyeti vya kuzaliwa maana wenzetu wengine uraia wenu unatia mashaka sana haya mwenge nao umekukosea nini; hivi umewahi kujiuliza sababu zake kwanza za kuanzisha mbio za mwenge au unadhani akina nyerere walikuwa hawana akili timamu. Watu tu wanaacha kuweka symbolism muhimu katika hizi ritual ndio maana wengine mnaleta madharau.