VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Wewe jamaa ni kati ya vijana wa lumumba mnaoongeaa ukweli na siasa kuweka pembeniMara kwa mara umekuwa ukilaamu kuhusu Serikali kupitia kwa DPP na AG kushindwa kesi mahakamani. Hata jana, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini, umeligusia hilo na kuonesha kukerwa nalo. Unatamani Serikali ishinde kila kesi yake mahakamani!
Hilo haliwezekani. Haliwezekani kikatiba,kisheria na hata kimahakama. Nimekuwa Wakili kwa miaka 20 (kwasasa nimepumzika na nipo kisiasa zaidi) na siamini kuwa ni lazima kushinda kila kesi mahakamani. Mahakama ndiyo inayotoa uamuzi baada ya pande husika kusikilizwa.
Kazi ya Mawakili, ima wa Serikali au binafsi, ni kuishawishi Mahakama kuamua kwa upande wake. Mahakama hushawishiwa kwa kutafrisiwa sheria na kesi zilizokwishaamuliwa na mahakama katika jambo kama hilo. Mawakili si waamuzi, Mahakama ndiyo kila kitu. Ndiyo maana asiyeridhika hukata rufaa.
Kusemasema kwa kukereka juu ya kushindwa kesi kwa Serikali ni kuiweka Mahakama katika wakati mgumu. Ni kuishurutisha Mahakama 'indirectly'. Pia, hakutakuwa na mantiki wala maana ya kuwa na Mawakili wa kujenga hoja kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Hakutakuwa na haja kwakuwa mshindi 'atalazimishwa' kushinda.
Ingawa Mawakili jana walicheka uliposema vile, walipaswa kupenyeza maelezo kama haya ili ujue kuwa Mawakili wana mwisho wake katika kesi. Kinachotakiwa kwa Mawakili wa Serikali na wengineo ni kujiandaa na kupambana ipasavyo. Kushinda na kushindwa kuwe matokeo tu. Serikali nayo hushinda kesi za kutosha Mahakamani!
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Tumbo ni kiungo kibaya sana mwilini.Mkuu waliokuwepo pale wengi wao wana ugonjwa ule wa kusifu na kuabudu ndiomaana vicheko vilitawala.japo nategemea kuona vilio vyao mbele ya Safiri.Ngoja niombe uzima.
Hasa likiwa halina kitu ndani ni hatari.Tumbo ni kiungo kibaya sana mwilini.
Ndiyo kinachowasumbua wasomi wetu.Hasa likiwa halina kitu ndani ni hatari.
Mara kwa mara umekuwa ukilaamu kuhusu Serikali kupitia kwa DPP na AG kushindwa kesi mahakamani. Hata jana, wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini, umeligusia hilo na kuonesha kukerwa nalo. Unatamani Serikali ishinde kila kesi yake mahakamani!
Hilo haliwezekani. Haliwezekani kikatiba,kisheria na hata kimahakama. Nimekuwa Wakili kwa miaka 20 (kwasasa nimepumzika na nipo kisiasa zaidi) na siamini kuwa ni lazima kushinda kila kesi mahakamani. Mahakama ndiyo inayotoa uamuzi baada ya pande husika kusikilizwa.
Kazi ya Mawakili, ima wa Serikali au binafsi, ni kuishawishi Mahakama kuamua kwa upande wake. Mahakama hushawishiwa kwa kutafrisiwa sheria na kesi zilizokwishaamuliwa na mahakama katika jambo kama hilo. Mawakili si waamuzi, Mahakama ndiyo kila kitu. Ndiyo maana asiyeridhika hukata rufaa.
Kusemasema kwa kukereka juu ya kushindwa kesi kwa Serikali ni kuiweka Mahakama katika wakati mgumu. Ni kuishurutisha Mahakama 'indirectly'. Pia, hakutakuwa na mantiki wala maana ya kuwa na Mawakili wa kujenga hoja kwa ajili ya kutolewa uamuzi. Hakutakuwa na haja kwakuwa mshindi 'atalazimishwa' kushinda.
Ingawa Mawakili jana walicheka uliposema vile, walipaswa kupenyeza maelezo kama haya ili ujue kuwa Mawakili wana mwisho wake katika kesi. Kinachotakiwa kwa Mawakili wa Serikali na wengineo ni kujiandaa na kupambana ipasavyo. Kushinda na kushindwa kuwe matokeo tu. Serikali nayo hushinda kesi za kutosha Mahakamani!
Mwafaaaaa!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Literally upo sahihi!
Liberally haupo sahihi na ninaamini unajua Hilo!
Mawakili wa Serikali huwa wanashirikiana na Washtakiwa wanaoshtakiwa na Jamhuri kuziharibu kesi zao ili washindwe kwa ahadi ya Rushwa. Kama Wewe ni kweli ni Wakili kwa miongo miwili utakuwa unalifahamu!
Sio tu Mawakili Bali hata Mahakimu na Majaji pia Wana Michezo hiyo!
Ofisi ya DPP ina ulazima gani wa kupeleka kesi Mahakamni Kama hawana ushahidi toshelezi.
Rais kaongelea Abnormality ya kupeleka kesi zote 28 na zote Serikali imeshindwa ingekuwa ajabu sana Kama Rais angechukulia kawaida hiyo issue!
Ndiyo kinachowasumbua wasomi wetu.
HahahaHasa likiwa halina kitu ndani ni hatari.
Bado anayetoa HUKUMU na HAKIMU na si WAKILI.Wapeni Mahakimu stahiki zao acheni Longo longo
Lakini ni nyinyi kwa Unafiki wenu mtakuja kuanzisha Mada hapa kuwa Mahakama na Ofisi ya DPP zimejaa Rushwa ndio sababu Mafisadi na wahalifu hawafungwi!
Na kwambia hivi hapo issue siyo wakili ni DPP,AG na HAKIMU,Mawakili ni mbuzi ya kafara tu
Kwa kuwa lengo lako ni kumkosoa Rais umeamua this time kuwa upande wa Mahakama kujifanya huoni wala husikii Kilio cha Rushwa kwa Mawakili na Mahakimu Ila nafasi yako inashuhudia unafiki uliokithiri lakin sitoshangaa kesho nikikuona kwny thread nyingine ukimuunga Mkono Tundu Lissu akisema Mahakama zimejaa Rushwa!