Naunga mkono hoja kwa 100%
Uchambuzi uliofanyika ni mzuri. Lakini conclusion yake haiwi supported na uchambuzi. Kwanini nasema hivi....
Ameonyesha mapungufu mengi yaliyopo Muhimbili (Muhas) lakini solution yake ni kwamba Chuo Kikuu cha Dar es salaam kiruhusiwe kuendesha Medicine pgm. Kwa maoni yangu hoja hapa ingekuwa MUHAS irejeshwe kuwa sehemu ya UDSM hapo uchambuzi ungekuwa umetimia sadakta.
Changamoto zinazoikabili Muhimbili leo ambazo mchambuzi amezitaja "upungufu wa waalimu, kujazana wanafunzi katika hospitali za kufundishia nk" utaikabili UDSM marafu. Kwani UDSM itapata waalimu kutoka wapi ambao Muhimbili imeshindwa kuwapata? Ikumbukwe vyuo vyote viwili mmiliki wake ni mmoja (Serikali), viwango vya mishahara havitofautiani sana...sasa comparable advantage iliyopo UDSM ni ipi kiasi kwamba iwe na uhakika wa kupata waalimu? Tukiangalia kuhusu tatizo la wingi wa wanafunzi kwenye hospitali za kufundishia....afadhali muhimbili Serikali imekopa pesa na kujenga Hospitali ya Mlongazila....hivyo wanafunzi watajifunzia kule, je UDSM wakiwa na pgm ya medicine wanafunzi watakwenda hospitali gani? Si ndio nao wataongeza mjazano kwenye hospitali nyingine za kufundishia?
Mchambuzi ameongelea kwa kina suala la idadi ya udahili na kuponda idadi kubwa ya udahili ya Muhimbili na akafanya comparison na vyuo vya marekani na Afrika ya kusini. Ni vizuri ili kufanya fair analysis ukaangalia takwimu za Doctor-Patient ratio za nchi hizo tatu zilizofanyiwa uchambuzi, pamoja na idadi ya vyuo vinavyozalisha madaktari katika nchi hizo. It is obvious kwamba Marekani na Afrika ya kusini ina vyuo vingi vinavyozalisha madaktari....kila jimbo lina chuo kikuu cha umma kinachoendesha programu ya Medicine achilia mbali vyuo vichache binafsi vinavyoendesha programu ya medicine....katika mazingira hayo, Chuo kama Harvard au MIT, au UC (ambavyo by the way sio sahihi kuvitumia kama benchmark ya masuala ya usaili) vinaweza ku afford kuwa na enrollment ndogo kabisa katika pgm zao za medicine...sababu wao ni IVY LEAGUE universities...sio chuo kila mwananchi anaweza kwenda kujiunga. Mchambuzi angefanya comparison na vyuo vya kawaida ambavyo wananchi wote wanaruhusiwa kusomea kwao....kama ilivyo UDSM na MUHAS ambavyo vipo kusaidia kusomesha wananchi wote na sio watu wachache kama Harvard.
Mchambuzi amesema kwamba ni kichekesho kwa vyuo binafsi kuruhusiwa kufundisha medicine...na Udsm kukataliwa. Hapa muhimu ni kuangalia contribution ya output ya vyuo hivyo....vinachangia kiasi gani kwenye safari ya nchi yetu kupunguza gap kubwa ya Doctor-Patient ratio. Na tunapofanya assessment hiyo tusiangalie changamoto za muda mfupi za madaktari 1400 kutokuwa na ajira leo hii. Hili ni tatizo la muda mfupi. Kwa kadri uchumi wa nchi unavyokuwa, mazingira yanavyozidi kuboreshwa mikoani, na uwekezaji wa mahospitali ya serikali kila wilaya na hospitali za binafsi, hao madaktari wote watamezwa katika soko la ajira na patakuwa na upungufu. And by the way yapo mambo ambayo pengine mchambuzi anayajua na hayasemi...iweje watoto wengi wa waalimu wa MUHAS na UDSM wanasomesha watoto wao medicine kwenye baadhi ya vyuo binafsi angali walifaulu vizuri sana kuweza kuingia MuHAS? Kuna cha kujifunza hapo..... hivi mchambuzi anafahamu baadhi ya vyuo binafsi kama Kairuki na Bugando wahitimu wake walifanyiwa tathmini na kubainika kuwa na ubora kiasi cha kufutiwa kigezo cha kufanya mitihani ya kusajili kwenye medical board ya nchi jirani kama Kenya na Rwanda? Na je mchambuzi anafahamu kwamba tathmini ya madaktari bingwa wanao supervise internship pale Hospitali ya Taifa inaonyesha kwamba madaktari waliotoka kwenye baadhi ya vyuo binafsi wanafanya vizuri zaidi kwenye vitendo (practical) kuliko wenzao wa vyuo vya umma?
Mwisho wa Yote, hakuna sababu ya ku undermine chuo kimoja dhidi ya kingine. Cha msingi ni kuweka vigezo vitakavyofuatwa na vyuo vyote katika utoaji wa mafunzo na ninakubaliana na wazo la kuwa na mtihani mmoja...maana hapo ndio ukweli utadhihirika wa nani hafunzwi sawa sawa. Na tutambue baadhi ya changamoto kama vile kuwa na upungufu wa waalimu ni changamoto za kitaifa na zinahitaji mikakati ya kitaifa kupata ufumbuzi. Haitoshi kuponda na kulalamika, tuje na mikakati ya kukabiliana nazo....kwasababu kama ni makosa yalishafanyika toka siku za nyuma ya kutofundisha wataalam wengi wa kutosha......jambo ambalo Muhimbili sasa wanalishughulikia, na mchambuzi wetu analiponda.