Rais Magufuli awakilishwa na Makamu wake, mkutano wa wakuu wa nchi za ACP

Kumbuka JPM anaposema yupo ktk kubana matumizi huwa anamaanisha anachosema.

Hivi ile ahadi ya kuuza mashangingi akiingia madarakani imeishia wapi vile? Na zile beamers and benzs za Ikulu zimeshapigwa mnada? Siku akitekeleza haya nifahamishe braza kaka.

Ni mtu mzalendo kwa nchi yake. Anawapenda watu wake. Anapenda maendeleo ya Tz yawe ya kasi zaidi. Kwa hiyo ni vzr kila mtu akaelewa ni kitu gani Rais anasimamia.
Oh! Alivyowaambia watu wapige mbizi kama hawana nauli ya Ferry ndiyo upendo unaousema? Tena akawapiga kwa kuwaletea Ferry mbovu kwa kuinunua kwa bei zaidi ya Ferry mpya. Huku akiuza nyumba za serikali kwa bei za kutupwa. Kama huo upendo umeanza ghafla leo, basi sawa.

Na huyu jamaa JPM siyo mnafiki hata kdg. Anaamini ktk anachokisema. Anasimamia ktk kile anachokiamini ili mradi tu kina manufaa kwa nchi na taifa kwa ujumla.
Ataje mshahara wake na aonyeshe salary slips kama alivyotuahidi.
Kwa hiyo yeye akiamini jambo lina maslahi ya taifa ndiyo inakuwa imekuwa? Hii ni trait mojawapo ya dikteta; hakuna deliberation wala mfano wake. Ndiyo maana kapiga kimya kuchukua maamuzi ya kashfa kama za Escrow, EPA, Lugumi n.k., kwani anaamini kufanya hivyo ni kwa maslahi ya taifa.
 
Rais Magufuli anatumia vema dhana ya kuwa madaraka si mtu mmoja. Anawashirikisha ipasavyo watu walio chini yake
I concur with you ... Urais ni taasisi ... Naomba Mh rais apige Kazi hakuna Tija ya kuzunguka dunia ... Aachane Na watu wanafiki Na vigeu geu
 
Rais Magufuli anatumia vema dhana ya kuwa madaraka si mtu mmoja. Anawashirikisha ipasavyo watu walio chini yake
Hilo linaeleweka lakini sasa kuna mikutano mingine ni vizuri ahudhurie yeye mwenyewe. Ukimtuma muwakilishi mda mwingine kwa baadhi ya vikao haileti uzito mkubwa. Kama huu mkutano wa wakuu wa nchi za ACP naona ni wa muhimu sana kwa yeye kuwepo kwanza kutokana na agenda zinazojadiliwa na pia kwa kuwa unashirikisha maraisi karibu wote wa Africa.
 
Ameamua kusafiri kupitia mlango wa nyuma, make juzi rais was Zanzibar kamuwakilisha Comoros,juzi kati majaliwa kamwakilisha London, mtondogoo kikwete kamuwakilisha China, leo makamu kamuwakilisha Papua new Guinea.
 
Nahisi kuna jambo limejificha.
 
Tuachane na cheap politics, KWANINI VIKAO VINGI LUGHA MALKIA INAPOTUMIKA MZEE HATAKI KWENDA YEYE??
hili swali ni la kijinga. lugha ndio nini. lugha inakuletea hela? ? au lugha inakusaidia kuimarisha uchumi.? mbona wachina na wafaransa na wengine wanaongea lugha zao.hili swali sio la mtu mzalendo .
 
Tuachane na cheap politics, KWANINI VIKAO VINGI LUGHA MALKIA INAPOTUMIKA MZEE HATAKI KWENDA YEYE??
Acha kutuchekesha wewe na elimu ya hapa na pale unataka kijilinganisha na PhD holder kwa kuongea kiingereza kwaiyo na wewe unaamni kabisa rais hajui kiingereza
 
Mie naanza kuchukia sasa. Hatueleweki twataka nini. Aliyesafiri sana akaitwa vasco dagama watu waka kokotoa kiasi cha gharama inchi inaingia. Huyu mwingine anafanya the opposite kubana matumizi bado watu mnalalama. Ebwana tunataka nini sasa?
 
Nahisi uhusiano wake na "mabakamabaka" si mzuri ndo maana hajakagua gwaride Lao. Akichomoka wata-Nkurunzinza hahahahahahaaa.
 
Siku hizi jamii forum imejazwa na vilaza sana great thinkers wachache sishangai kuona nchi yetu ni moja kati ya nchi ambazo raia wake wengi wana IQ ndogo sana . Kwenye hili swala there's something beyond kubana matumizi .
 
Hebu jaribuni kugoogle SOCIAL ANXIETY DISORDER someni kwa undani muelewe .
 
Mie naanza kuchukia sasa. Hatueleweki twataka nini. Aliyesafiri sana akaitwa vasco dagama watu waka kokotoa kiasi cha gharama inchi inaingia. Huyu mwingine anafanya the opposite kubana matumizi bado watu mnalalama. Ebwana tunataka nini sasa?
Mkuu hujaelewa mada..Raisi kubana matumizi naunga mkono 100% lakini linapokuja swala la diplomasia na Raisi anatakiwa awe mstari wa mbele. Kuna mikutano kama hii ni ya muhimu kwa yeye kwenda kuiwakilisha nchi.
 
Back
Top Bottom