Rais Magufuli afichua njama ya Wabunge wa CCM kumng’oa Waziri Mkuu madarakani

Ni fundisho kwa wabunge wa chama kile. Kwamba ushabiki wenu mnapokuwa bungeni utawatokea puani siku si nyingi. UKAWA hawakuwaambia kwamba madaraka ya Rais kwenye Katiba ni Makubwa kuliko ya Mungu???? mnajifanya leo mmesahau mlivyowasaliti wananchi mkaamua ku-line up in tandem to support your nightmare political party??? mnavuna mlichopanda. I don't have sympathy for any one of you.
 
"Hata mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi."



ukimwaga mboga na mwaga ugali... Jino kwa jino... Hahaha... Safi sana...
Mmh!!
Kwa hilo nna wasi wasi. . .
 
Shida inayowakumba watumishi wa umma hapa nchini iko kwa wabunge pia, mikopo kila mahali, hawawezi kuwa na ujasiri wa kusema vunja Bunge twende kwenye uchaguzi wakihofia watalipaje mikopo.
 
Pengine hata hajui akivunja bunge nini kinafuata kwa upande wake. Alafu ni mwoga kama nini, ukiona mtu kutwa kucha anawatuhumu na kuwanyanyasa wengine huyo ni mtu dhaifu sana na kichwani hamna kitu. Watu wenye akili timamu na wanaojiamini hawalazimishi mambo, wanashawishi kwa hoja na utendaji.
 
Hana jipya Malaika Mkuu zaidi ya kukimbia kivuli chake na kubwabwaja. Anataka kushughulikia kero za wasanii lakini kero za wafanyakazi wa Serikali za nyongeza ya mishahara kauchuna, wanaodai mabilioni ya haki zao anaita madai hewa, ajira Serikalini kauchuna.

Nchi ilishamshinda siku nyingi huyu sasa anatafuta mchawi wakati mchawi ni yeye mwenyewe!

Wewe uko kwa wazungu utayajuaje ya huku wala si mwajiriwa wa serikali??
 
Pengine hata hajui akivunja bunge nini kinafuata kwa upande wake. Alafu ni mwoga kama nini, ukiona mtu kutwa kucha anawatuhumu na kuwanyanyasa wengine huyo ni mtu dhaifu sana na kichwani hamna kitu. Watu wenye akili timamu na wanaojiamini hawalazimishi mambo, wanashawishi kwa hoja na utendaji.

Rais asijue wewe ujue!!! Bogus kweli wewe!!
 
View attachment 480915
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa bado yupo mkoani Dodoma, jana alipata nafasi ya kufanya kikao na wabunge wa chama hicho ambapo alizungumza mambo mbalimbali ambayo hafurahishwi nayo kama kiongozi mkuu wa chama.

Rais Magufuli alikutana na wabunge hao katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza nao ni pamoja na kuwaambia kuwa anafahamu baadhi ya wabunge wanampinga Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Nafahamu baadhi yenu mnampinga Waziri Mkuu na mnataka aondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye, naomba niwaambie kuwa hamtafanikiwa. Mimi namuunga mkono msaidizi wangu huyuo kwa asilimia 100 kwa nimejionea mwenye namna anavyoweza kufanya kazi, alisema Rais Dkt Magufuli.

Hata mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi.

Mbali na hilo kiongozi huyo alitoa onyo kwa wabunge wa CCM ambao wanagawa muda wao wa kuzungumza na kuwapa wabunge wa upinzani pindi wanapokuwa kwenye vikao vya bunge. Kauli hii imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Boniface Getere kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba kutoka kwenye muda wake wa kuchangia ambao ni dakika 10.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Dkt Magufuli amewaambia kuwa anakerwa na baadhi ya wabunge kufifisha jitihada za serikali katika kupambana na dawa za kulevya huku akimtuhumu mbunge mmoja kutoa siri na kuzipeleka upinzani.

Kuhusu matangazo ya bunge kutokurushwa mubashara, Mwenyekiti wa CCM aliwaambia wabunge hao kuwa yeye ndio aliamua iwe hivyo kutokana na wabunge wengi kuwa wapiga porojo tu.

Kikao hicho kilichofanyika chini ya ulinzi mkali huku wabunge wakizuiwa kuingia na simu, kilihudhuriwa pia na Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula na Katibu Mkuu, Abdulrahman Kinana.

Chanzo: Swahili times
Pure dictatorship...
 
waziri mkuu hapingwi na bunge ukiona anapingwa itakuwa siyo yy anayepingwa ila kwa kuwa yy ndio mkuu wa serikali bungeni lazima abebe mzigo wa wengine,hasa kama makonda asipotii wito wa kwenda bungeni lazima mbuzi wa kafara itakuwa waziri mkuu japo si lengo !
 
Mmhh ntakuwa wa mwisho kuaminimambi hizi, it seems to be another fake news kama ile yaTBC.
 
Nimezaliwa Tanzania nimelelewa Tanzania na nimesoma Tanzania. Tanzania ni kwangu naweza kuongea chochote kile kuhusu nchi yangu nikiwa ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania na sijawahi hata siku moja kuandika uzushi. Usinipangie nini nastahili kuongea kuhusu nchi yangu.


Wewe uko kwa wazungu utayajuaje ya huku wala si mwajiriwa wa serikali??
 
Hana jipya Malaika Mkuu zaidi ya kukimbia kivuli chake na kubwabwaja. Anataka kushughulikia kero za wasanii lakini kero za wafanyakazi wa Serikali za nyongeza ya mishahara kauchuna, wanaodai mabilioni ya haki zao anaita madai hewa, ajira Serikalini kauchuna.

Nchi ilishamshinda siku nyingi huyu sasa anatafuta mchawi wakati mchawi ni yeye mwenyewe!
Na uhamisho umekuwa ngumu anataka wake zetu wachukuliwe
 
Rais asijue wewe ujue!!! Bogus kweli wewe!!
Kama unadhani mtu kua raisi ndio kujua kilakitu basi nawewe akili zako zipo kiwango sawa na zake. Maana matendo yake yanaashiria anajifanya mjuaji. Kuto kujua sio tatizo, tatizo ni kutokujua kua haujui!!!
 
Back
Top Bottom