Rais Dr. Magufuli ashiriki kikao cha kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM

Utaritibu uliotukuka wa kuachiana madaraka. Tangu enzi hizo kuna vyama unakuta viongozi wake ni hao hao tu, wanakuwa wao ndio chama na chama ndio wao.
na ukionyesha nia ya kuutaka uenyekiti utaundiwa zengwe na kuitwa msaliti katika chama
 
Labda linamjadili Naibu spika kurejesha fedha serekalini huku bunge likigubikwa na ukata mkubwa, na spika kutokuwa na taarifa za uamuzi huo.
MSIGWA mzee wa kulia lia njoo hapa! rais kwa nini anatumia pesa? Rais kwanini ananunua madawati kwa fedha za bunge wakati walitugomea kuongeza posho ya gari la mbunge kutoka 90,000,000/= to 120,000,000/= kwa kisingizio cha kukosa pesa? kwa nini apeleke hela kwenye barabara...? wabunge tunafanya kazi muhimu tunatakiwa tutumie helicopter kama za CHADOMO...mbona hao wameweza!
 
Obama amewahi kusikika akisema kwamba, pamoja na baadhi ya wamarekani kutaka kumuona akiendelea kuwa rais, yeye anaamini katika ukomo wa muda wa awamu mbili za urais. Na ndivyo ambavyo taasisi kubwa zinapaswa kuongozwa, haiwezekani mtu mmoja akawa na haki ya kuzaliwa ya kuwa kiongozi mpaka siku anayokwenda kaburini.
Vyama vya siasa vinalo jambo la maana sana la kujifunza, hakuna binadamu mwenye uwezo mkubwa ambao eti hauwezi kupata mbadala kutoka kwingineko.
Ujumbe Huu umfikie Mmawia pamoja na mkuu Freeland
 
Utaritibu uliotukuka wa kuachiana madaraka. Tangu enzi hizo kuna vyama unakuta viongozi wake ni hao hao tu, wanakuwa wao ndio chama na chama ndio wao.
Nadhani unamaanisha CHADEMA mkuu..usimung'unye maneno hizo zama zilishapita!Nyeupe tuuite nyeupe na si nyekundu..Chadema wajipange!
 
Nadhani unamaanisha CHADEMA mkuu..usimung'unye maneno hizo zama zilishapita!Nyeupe tuuite nyeupe na si nyekundu..Chadema wajipange!
Siyo Chadema ila Vipo vingi mkuu, na orodha ni ndefu, NKAFU ni Sefu na Nsefu ndio NKAFU, long time ago kuna jamaa alijulikana kama Jiduramabambasi, sasa huyo jamaa na wenzake akaamua kumpindua mwenyekiti wao, then yule na wenzake wakaambiwa "out", walipotoka out basi hicho chama kimemfia huyo chair mikononi, kwa kweli ninaamini kama yale mapinduzi yangefanikiwa hiki chama kingekuwa tishio balaa na chair angekuwa anakula shushu kama mzee Mtei anavyokula matunda ya NGO yake.
 
Alafu kuna chama Fulani ,hakijawahi wala hakina kamati kuu , hakina mkutano mkuu ,

Mgombea wake anapatikana kwa kubadili gia angani.

Eti hicho chama ndio kitaitoa ccm madarakani
Kweli kabisa, ni sawa na Chama Cha Majipu (CCM) kuchafua damu kisha kikaanza kuyatumbua ili hali damu bado chafu. Wadhani yataisha?
 
Utaritibu uliotukuka wa kuachiana madaraka. Tangu enzi hizo kuna vyama unakuta viongozi wake ni hao hao tu, wanakuwa wao ndio chama na chama ndio wao.
Tehetehe halafu haohao wanataka demokrasia ilihali wenyewe hawataki kuachia madaraka ya uenyekiti..
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Alafu kuna chama Fulani ,hakijawahi wala hakina kamati kuu , hakina mkutano mkuu ,

Mgombea wake anapatikana kwa kubadili gia angani.

Eti hicho chama ndio kitaitoa ccm madarakani
Ccm haiwezi kung'olewa na vyama vidogovidogo.. Safi sana viongozi wetu wa Ccm
 
Wanafuata katiba ya chama mkuu
Mkuu, katiba haisemi haya ya kupokezana!!

Wamerithi tu toka kwa Nyerere. Kwa vile Nyerere alifanya vile, Mwinyi akafanya basi kila mmoja lazima afanye mpaka siku yatuharibikie!!
 
Hebu chukua hicho chama. Wanyime hela ndo watakusanya ada na viingilio na mikutano kwenye matawi itaitishwa.
Mimi ni mwanachama na tukiwahi kuandaa daftari la wanachama lakini sijui wanakutana lini na wapi.
Sasa hivi wanachama wasio na hela ni takataka tu
 
Mkuu, katiba haisemi haya ya kupokezana!!

Wamerithi tu toka kwa Nyerere. Kwa vile Nyerere alifanya vile, Mwinyi akafanya basi kila mmoja lazima afanye mpaka siku yatuharibikie!!
Kwa hio huo utaratibu wa kupokezeana unaona ni utaratibu mbaya? And ulitaka utaratibu uweje?
 
Back
Top Bottom